Nenda kwa yaliyomo

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo (pia unajulikana kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mavalane, hapo awali ulijulikana kama uwanja wa ndege wa Lourenço Marques [1]; IATA: LUM) ni uwanja wa ndege unaopatikana kilomita 3 Kaskazini-magharibi mwa Maputo, jiji kubwa na mji mkuu wa Msumbiji.

Ni uwanja wa ndege mkubwa zaidi nchini Msumbiji, na kitovu cha mashirika ya ndege ya LAM Msumbiji na Mashirika ya ndege ya Kaya. Sehemu nyingi zinazohudumiwa na uwanja wa ndege huu zipo Afrika, lakini kuna huduma chache za katika mabara mengine.

Marejeo

  1. "Lourenço Marques Airport Archived 25 Oktoba 2012 at the Wayback Machine.." Aviation Safety Network. Retrieved on 3 October 2009.