Adolf Hitler: Fahamu njama za kumuua Mnazi huyo ilivyopangwa na kugonga mwamba

C

Chanzo cha picha, Getty Images

Dikteta wa Nazi Adolf Hitler anaaminika kuhusika na vifo vya maelfu ya watu. Lakini sio kwamba maisha ya Hitler hayakuwa hatarini wakati huo. Yalikuwa na mashambulizi hatari lakini mashambulizi haya hayakufanikiwa.

Kanali Claus von Stauffenberg, afisa wa zamani katika jeshi la Ujerumani, alihusika kwenye njama za kumuua Hitler. Akandaa vyema kuitekeleza. Hiltler alikuwa amejenga kituo kimoja kwa jina Wolf's Lair msituni huko East Prussia na mfumo wake wa ulinzi ulikuwa wa hali ya juu. Jaribio lilifanywa kumuua Hitler kwenye kituo hiki lakini likatibuka dakika za mwisho.

Tarehe 20 Julai 1944, akiwa na umri wa miaka 36 Claus von Stauffenberg aliwasili katika kituo cha Wolf's Lair. Lengo lake lilikuwa ni kumuua Hitler. Hilter alikuwa akifanya mikutano ya kila siku na maafisa wa kijeshi na hivyo Stuffenberg naye alihudhuria.

Kwenye mahojiano ya mwaka 1967 na BBC, afisa wa zamani katika jeshi la Ujerumani Walter Warlimont anakumbuka kisa hicho akisema, "tulikuwa tumesimama huko na mkutano ukaanza baada ya Hitler kuingia." Anasema, "kisha mlango ukafunguka ghafla tena. Nikageuka na kuona Kanali akiingia. Alikuwa akifahamika kwa sababu jicho lake la kulia lilikuwa limefunikwa na mkono mmoja ulikuwa umekatwa."

S

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hitler alinusurika kuuawa na bomu lakini nguo yake ilichanwachanwa na msukosuko wa bomu hilo

Hitler akageuka na kumtazama kanali bila huruma. Kisha jenerali Keitel akamtambulisha kanali kwa Hitler. Mtoto wa kiume wa Stuffenberg ambaye sasa na umri wa miaka 80 anasema babake alikuwa afisa wa jeshi mkatoliki. "Kila mtu alikuwa anasema baba yangu alikuwa na sura nzuri sana, mrefu, nywele nyeusi na macho ya rangi ya bluu.

Njama za kumuua

Stuffenberg aliumia vibaya wakati alitumwa nchini Tunisia mwaka 1943, akapoteza jicho moja, mkono wake wa kulia na vidole viwili kwenye mkono wake wa kushoto. Wakati Stuffenberg alipopona majeraha yake, alitafutwa na shirika lililoongozwa na Jenerali Henning Treskov. Lengo la shirika hilo likuwa ni kumuua Hitler na kupindua utawala wa Nazi.

Mwaka 1994, Stauffenberg akateuliwa mkuu wa majeshi katika jeshi la mbadala la Ujerumani. Sasa ingekuwa rahisi akutane na Hitler na atekeleze njama hiyo ya kumuua.

Kama sehemu ya mpango huo, Stuffenberg angevunja safu ya ulinzi ya Hitler na abebe bomu kwenye mkoba na kuliweka karibu na Hitler wakati wa mikutano ya kila siku. Baada ya hilo angeondoka chumba cha mkutano. Baada ya mlipuko, Stauffenberg angerudi Berlin ambapo jeshi mbadala lingetwaa madaraka.

Julai 20 ilikuwa ni siku ya Alhamisi. Stuffenberg alifika Wolf's Lair - mkutano ungefanyika mwendo wa saa 12:30. Kulikuwa na vizuizi wakati wa kulitega bomu na angebeba kilipuzi kimoja tu. Vallimont alisema mwaka 1967, " ninakumbuka akija na mkoba mweusi. 'Lakini sikuwa makini naye. Ndio sababu niliuweka mkoba ule chini ya meza na sikuona akiondoka chumba cha mkutano baada ya hapo."

Kwa nini njama zilifeli

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini kabla ya mlipuko, mkoba wa Stuffenberg uliondolewa na kuwekwa nyuma ya meza. Bomu lililipuka lakini halikulenga vizuri. Licha ya kuwa watu wanne waliuawa Hitler alifanikiwa kutoroka.

Stuffenberg na washirika wengine baadaye walikamatwa na kupigwa risasi mjini Berlin.

Mama yake Berthold, bibi, babu walikamatwa nao, Berthold na ndugu zake wakapelekwa makao ya watoto. Baadaye Berthold akaja kuwa jenereli katika jeshi la Ujerumani Magharibi.

Hadi leo hii anaishi katika kijiji cha nyumbani kwao asilia.