Tende : Mashambulizi ya Houthi yatatiza upatikanaji kabla ya Ramadhan 2024

Maelezo ya video, Ukosefu wa usalama wa Bahari ya Shamu waathiri ugavi kabla ya Ramadhani
Tende : Mashambulizi ya Houthi yatatiza upatikanaji kabla ya Ramadhan 2024

Mashambulizi ya waasi wa Houthi dhidi ya meli katika Bahari ya Shamu yametatiza uwasilishaji wa bidhaa katika maeneo ya Afrika Mashariki.

Hali hiyo inatishia ongezeko la bei za bidhaa, ikiwemo vyakula muhimu katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa Waislamu.

Mwandishi wa BBC Peter Mwangangi ametembelea mji wa Mombasa Pwani ya Kenya , ambapo anaangazia hali ilivyo miezi miwili baada ya mashambulio ya Houthi kuanza katika Bahari ya Shamu.