Barua ya Siri: Papa alijua kuhusu njama za Wanazi za kuwaua Wayahudi

AZ\

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Papa Pius XII

Barua iliyoibuliwa hivi karibuni huko Vatican inafichua mengi kuhusu Wajerumani na Papa Pius XII.

Barua iligunduliwa na mtunza kumbukumbu wa Vatican, Giovanni Cocco. Ilichapishwa Jumapili katika gazeti la Italia, Corriere della Sera chini ya kichwa cha habari "Pius XII alijua."

Barua ya tarehe 14 Disemba 1942, iliandikwa na Padri Lothar König, aliyepinga Wanazi huko Ujerumani, kwa Padri Robert Lieber, katibu binafsi wa Papa katika Vatican.

Inataja kambi tatu za Nazi; Belzec, Auschwitz na Dachau. Pia, inaaminika kuna barua nyingine kati ya Koenig na Leiber, lakini huenda zimetoweka au bado hazijafichuliwa.

Cocco anaamini baru hiyo ni ya kweli kutokana na mambo yaliyotajwa, na kwa msingi huo anahitimisha kwamba Kanisa Katoliki nchini Ujerumani lilimtumia Pius XII habari sahihi na kamili kuhusu uhalifu dhidi ya Wayahudi na Vatican ilikuwa na habari kuhusu kambi za mateso na mauji.

Mwanahistoria na mwandishi David Kerzer anaeleza kuhusu Papa Pius Owens: "Imefichuliwa na mtu wa Vatican, hivyo inaonekana kuna jaribio la kukiri historia hii katika Vatican au katika baadhi ya maeneo ya Vatican."

Nyaraka ambazo hazijachapishwa

aZ

Chanzo cha picha, Getty Images

Coco anaamini barua hii ni mojawapo ya barua ambazo hazijapatiwa ufumbuzi katika Sekretarieti ya Jimbo la Vatican.

Suzanne Brown-Fleming, mkurugenzi wa programu katika Jumba la Makumbusho ya Holocaust la Marekani mjini Washington, amesema kutolewa kwa barua hiyo kunaonyesha Vatican inachukulia kwa uzito kauli ya Papa Francis kwamba "Kanisa haliogopi historia."

2019, Papa Francis aliamuru kufunguliwa kwa kumbukumbu za wakati wa vita.

"Baada ya miaka mitatu ya kufungua na kuchunguza kumbukumbu za Vatican, nyaraka zinaonyesha Papa alifahamishwa kuhusu juhudi za Wanazi za kuwaangamiza Wayahudi wa Ulaya tangu mwanzo," Kerzer aliambia BBC.

Utata juu ya Heshima ya Pius XII

wes

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Papa Pius

Barua iliyofichuliwa huenda ikachochea mjadala juu ya urithi wa Pius XII na kampeni yenye utata ya kumtangaza kuwa mtakatifu.

Wafuasi wake wanadai alifanya kazi kisiri ili kuwasaidia Wayahudi, na hakufichua ukweli ili kuzuia kuzorota zaidi kwa hali ya Wakatoliki wa Ulaya iliyokuwa ikikaliwa na Nazi.

Wapinzani wanasema hakuwa na ujasiri wa kusambaza habari aliyokuwa nayo, licha ya maombi kutoka kwa washirika waliopigana dhidi ya Ujerumani.

Katika kitabu kilichoandikwa na Kerzer, kulikuwa na mijadala mirefu ya siri kati ya Hitler na Pius XII kuhusu mapatano ya kusimamisha mapigano.

Ushahidi unaonyesha jukumu la Pius XII wakati wa Vita vya Pili vya Dunia lilikuwa na utata. Ingawa aliona Unazi kuwa harakati ya kisiasa ya kipagani ambayo ilisumbua Wakatoliki.

Hakushutumu waziwazi mauaji ya Wayahudi, licha ya kujua unyama uliokuwa ukiendelea.