Ubongo wa binadamu una nini kinachotufanya kuwa na akili kuliko viumbe wengine?

Emmanuel Stamatakis, Andrea Luppi na David Menon, The Conversation

Brain

Chanzo cha picha, Getty Images

Binadamu hana mpinzani katika eneo la utambuzi. Hakuna kiumbe mwingine yoyote anayefanya uchunguzi kwenye sayari nyingine, kuzalisha chanjo za kuokoa maisha, au kutunga mashairi.

Jinsi habari inavyochakatwa katika ubongo wa mwanadamu ili kufanya hili liwezekane ni swali ambalo limeleta mvuto usio na kikomo, lakini halina majibu ya uhakika.

Uelewa wetu wa kazi ya ubongo umebadilika kwa miaka sasa. Lakini mifano ya sasa ya kinadharia inaelezea ubongo kama "mfumo wa usindikaji wa taarifa unaosambazwa."

Hii ina maana kwamba ina vitu tofauti, ambavyo vinaunganishwa kwa karibu kupitia mfumo wa umme wa ubongo. Ili kuingiliana na kuwasiliana na kila mmoja, hubadilishana taarifa kupitia mfumo wa ishara unaoingiza na kutoa.

Hata hivyo, hii ni sehemu ndogo tu ya taswira ngumu zaidi kuhusu akili. Katika utafiti uliochapishwa kwenye jarida la Nature Neuroscience, kwa kutumia ushahidi kutoka kwa spishi tofauti na taaluma nyingi za neuroscientific, unaonyesha kwamba hakuna aina moja ya uchakataji wa taarifa katika ubongo.

Jinsi maelezo au taarifa zinvyochakatwa pia hutofautiana kati ya binadamu na viumbe wengine, ambapo inaweza kueleza kwa nini uwezo wa utambuzi wa spishi zetu ni bora zaidi. Tuligundua kuwepo kwa maeneo tofauti ya ubongo, yanayotumia namna ama mikakati tofauti kuingiliana.

Mifumo na mikakati mbalimbali ya Ubongo

Baadhi ya maeneo ya ubongo hubadilishana taarifa na maeneo mengine kwa njia iliyozoeleka sana, kwa kutumia njia ya kutoa na kupokea. Hii inahakikisha kwamba mawimbi yanapitishwa kwa njia ya kuzaliana na ya uhakika.

Brain

Chanzo cha picha, Getty Images

Fikiria suala la macho, kwa mfano, ambayo hutuma ishara ya taarifa kwenye ubongo kwa kwa ajili ya uchakataji. Taarifa nyingi zinazotumwa ni nakala, zikitumwa na kila jicho. Nusu ya taarifa hizi, kwa maneno mengine, hazihitajiki. Kwa hivyo tunaita aina hii ya uchakataji wa taarifa hizi zisizohitajika kitaalamu "input-output information processing'.

Uchakataji unaoitwa 'synergistic'

Uchakataji wa taarifa wa ushirikiano wa kimfumo umeenea zaidi katika maeneo ya ubongo ambayo yanasaidia utendaji wa maeneo changamano zaidi ya utambuzi, kama vile umakini, kujifunza, kumbukumbu ya kufanya kazi, utambuzi wa kijamii na namba.

Sio ngumu, kwa maana kwamba inaweza kubadilika kwa kukabiliana na uzoefu wa mtu, kuunganisha mitandao tofauti kwa njia tofauti. Hii inawezesha kupata mchanganyiko wa taarifa.

Brain

Chanzo cha picha, Getty Images

Je, hili ndilo inayotufanya kuwa wa kipekee?

Tulitaka kujua ikiwa uwezo huu wa kukusanya na kutoa taarifa kupitia mifumo ya kimtandao unaoingiliana katika ubongo ni tofauti kati ya binadamu na viumbe wengine kama nyani, ambao wanafanana kibaiolojia.

Ili kujua, tuliangalia data ya picha za ubongo na uchambuzi wa maumbile kutoka kwa spishi tofauti. Tuligundua kwamba mwingiliano huchangia sehemu kubwa ya mtiririko wa taarifa katika ubongo wa binadamu kuliko katika ubongo wa nyani.

Hata hivyo, akili za spishi zote mbili ni sawa katika suala la ni kiasi gani wanategemea taarifa zisizohitajika.

Pia tumesoma uchambuzi wa kinasaba wa binadamu. Imetuonyesha kuwa maeneo ya ubongo yanayohusishwa na uchakataji wa taarifa shirikishi kuna uwezekano mkubwa wa kueleza jeni ambazo ni za kipekee za binadamu na zinazohusiana na ukuaji na utendaji kazi wa ubongo, kama vile akili.

Hii ilituongoza kwenye hitimisho kwamba tishu za ziada za ubongo wa binadamu, zilizopatikana kama matokeo ya mageuzi, zinaweza kujitolea hasa kwa ushirikiano.

Brain

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwsiho, kazi yetu inafichua jinsi ubongo wa mwanadamu unavyoognoza kwenye uaminifu na ujumuishaji wa taarifa: tunahitaji vyote viwili. Muhimu zaidi, mfumo tuliounda unaahidi maarifa mapya muhimu katika anuwai ya maswali ya kisayansi ya neva, kutoka kwa yale yanayohusiana na utambuzi wa jumla ikiwemo ulemavu.