Nenda kwa yaliyomo

Daniel Thioune

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Daniel Moustapha Thioune (amezaliwa 21 Julai 1974) ni meneja wa Mpira wa miguu wa Ujerumani na mchezaji wa zamani ambaye ni kocha mkuu wa klabu ya HSV (Hamburger SV) iliyopo katika daraja la pili la Bundesliga.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Thioune alizaliwa nchini Ujerumani na baba wa Senegal na mama Mjerumani, akishikilia uraia wa pande zote mbili. Yeye ndiye meneja wa kwanza mweusi wa mpira wa miguu huko Ujerumani. [1]

Akiwa kijana alisoma Shule ya Upili ya Graf-Stauffenberg huko Osnabrück. [2] Thioune alisoma michezo na ualimu kwenye Chuo Kikuu cha Vechta na kupata shahada ya kwanza mwaka 2019. [3] [4]

Amemwoa Claudia Thioune wakiwa na watoto Hanna (*1998) na Joshua (*2004). [5]

Thioune alicheza miaka mingi kwenye klabu ya VfL Osnabrück, ambapo alijiimarisha kama mfungaji bora kutoka kwa uwanja wa kati. Alipostaafu mnamo 2010 baada ya kucheza kwa pande nyingi za chini za ligi, alianza kufundisha timu mbalimbali kwenye Chuo cha Soka cha VfL Osnabrück kabla ya kuteuliwa kama mkufunzi wa timu ya kwanza mnamo 2017. Aliajiriwa kama kocha mkuu wa Hamburger SV mnamo 2020. [6] [7]

Mchezaji[hariri | hariri chanzo]

Thioune alianza kuichezea klabu ya Raspo Osnabrück akiwa na umri wa miaka sita, wakati wazazi wake walikaa jirani na uwanja wa klabu ile. Aliendelea katika timu ya vijana wa Osnabrücker SC na Post SV Osnabrück, kabla ya kuhamia VfL.

Takwimu za usimamizi[hariri | hariri chanzo]

(Hali ya 6 Julai 2020)

Taarifa ya usimamizi
Timu Nchi Kuanzia Hadi Matokeo Marejeo
Mechi alipohusika Ushindi Sare Kushindwa Goli upande wake Goli dhidi yake Tofauti Asilimia ya kushinda
Osnabrück Ujerumani 5 Oktoba 2017 6 Julai 2020 105 39 33 33 152 135 +17 37.14 [8]
Hamburger SV Ujerumani 6 Julai 2020 (Julai 2020) 0 0 0 0 0 0 0 - [9]
Jumla &0000000000000105.000000105 &0000000000000039.00000039 &0000000000000033.00000033 &0000000000000033.00000033 &0000000000000152.000000152 &0000000000000135.000000135 +17 &0000000000000037.14000037.14

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Emedia : DANIEL THIOUNE, D'ORIGINE SÉNÉGALAISE, PREMIER ENTRAÎNEUR NOIR EN ALLEMAGNE". emedia.sn. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-04-17. Iliwekwa mnamo 2020-07-15.
  2. "„Schule ohne Rassismus – Schule mit Courage" am Graf-Stauffenberg-Gymnasium". vfl.de. VfL Osnabrück. 6 Juni 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-14. Iliwekwa mnamo 14 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Harding, Jonathan (29 Januari 2019). "Daniel Thioune: Der Trainer, der neue Wege geht". dw.com. Iliwekwa mnamo 14 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Riepe, Louisa (3 Septemba 2019). "Spieltag #5 mit Trainer Daniel Thioune - Die Intensität stimmt". noz.de. Iliwekwa mnamo 14 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Alberti, Stefan (26 Novemba 2018). "VfL-Coach Daniel Thioune liefert souveränen TV-Auftritt ab". noz.de. Iliwekwa mnamo 14 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "DANNY THIOUNE NEUER CO-TRAINER UND PRAKTIKANT". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Julai 2011. Iliwekwa mnamo 27 Mei 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Daniel Thioune – 2014/2015". Fussballdaten.
  8. "Vfl Osnabrück: Matches". Soccerway. Perform Group. Iliwekwa mnamo 6 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Hamburger SV: Matches". Soccerway. Perform Group. Iliwekwa mnamo 6 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]