Nenda kwa yaliyomo

Lena Headey

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lena Headey Mwaka 2019

Lena Kathren Headey (amezaliwa Hamilton, Oktoba 3, 1973[1]) ni mwigizaji wa Uingereza. Alianza kuwa maarufu kimataifa baada ya kuigiza kama Cersei Lannister katika tamthilia ya Game of Thrones ambapo alichaguliwa mara 5 kuwania tuzo za Primetime Emmy Award na Golden Globe Award . Na pia alikua maarufu baada ya kuigiza kama Malkia Gorgo kwenye filamu ya 300 (2006).

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Lena Kathren Headey ni mtoto wakike na wazazi wake wote Sue na John Headey wakiwa ni Waingereza. Baba yake alikuwa afisa wa polisi kutoka Yorkshire, alifanya kazi Hamilton wakati Lena anazaliwa katika kituo cha Polisi cha Bermud. Anamdogo wake wakiume anayeitwa Tim[2]. Lena ana asili ya Kiingereza na Ireland. Alipokua na umri wa miaka mitano familia yake ilirudi Uingereza na kuishi Somerset. Alisoma masomo ya ballet akiwa mdogo[3]. Headey alipata uzoefu wake katika kuigiza alipokua mwanafunzi wa Chuo cha Shelley, akiwa na umri wa miaka 17. Akiwa anaigiza katika ukumbi wa Chuo ulioitwa Royal National Theatre, alichaguliwa kuigiza katika tamthilia ya Waterland 1992[4].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.tvguide.com/celebrities/lena-headey/bio/161706
  2. "She's Beautiful When She's Angry". Men's Health (kwa American English). 2010-10-05. Iliwekwa mnamo 2024-04-30.
  3. Lena Heady on Letterman, iliwekwa mnamo 2024-04-30
  4. YorkshireLive (2008-01-16). "Lena gets ready to terminate TV ratings". Yorkshire Live (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-30.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lena Headey kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.