Aina za mazishi zisizoharibu mazingira

hgjkl

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Mazishi ya asili yanazidi kuwa maarufu. Inahusisha kuzika mwili bila vizuizi vya kuzuia mwili kuoza, vifungashio vya plastiki au masanduku ya chuma
  • Author, Becca Warner
  • Nafasi, BBC

Sio wengi wetu wanaopenda kuzungumzia kifo. Lakini ukweli usiofurahisha ni kwamba; mara tu tunapoondoka, miili yetu inahitaji mahali pa kwenda - na njia za kuchoma moto au kuzika miili huja na gharama ya kutisha kwa mazingira.

Watu wengi nchini Uingereza (ambapo mimi ninatoka) huchomwa wanapokufa. Uchomaji wa kawaida nchini Uingereza unatumia gesi, na inakadiriwa kuzalisha takribani kilogramu 126 za CO2 - sawa na kuendesha gari kutoka Brighton hadi Edinburgh. Nchini Marekani, uzalishaji ni wa juu zaidi, kilogramu 208 za CO2.

Pengine si jambo linalozalisha kaboni nyingi - lakini kadiri watu wengi wanapochagua kuchomwa wanapokufa, hewa chafu huongezeka haraka.

Kuzika mwili sio njia bora vilevile. Kaburi likijengwa kwa zege, mwili ukiwa kwenye jeneza la mbao au chuma. Maji yenye sumu kama vile formaldehyde, hutumiwa mara nyingi, ambayo huingia kwenye udongo pamoja na chuma ambayo hudhuru mifumo ya ikolojia na kuchafua maji.

Jeneza la Uyoga

weqrfq

Chanzo cha picha, Getty Image

Vipi kuhusu vitu visivyo vya asili vinavyoingia ndani ya mwili wa binadamu - dawa, plastiki na vyuma kutoka kwenye majeneza. Bob Hendrikx amekuja na suluhisho kwa kutengeneza jeneza la uyoga.

"Moja ya matatizo tunayokabiliana nayo ni uharibifu wa udongo - ubora wa udongo unazidi kuwa duni na duni, hasa katika maeneo ya mazishi, kwa sababu kuna uchafuzi mwingi wa mazingira. Mwili wa binadamu [pia] unazidi kuchafua," anasema Hendrikx.

Uyoga una uwezo wa kuongeza afya ya udongo na kunyonya maji maji ya chuma ambayo yangeweza kuvuja kwenye maji ya ardhini. Baadhi ya spishi za uyoga zinaweza kuharibu plastiki.

Ninamuuliza Rima Trofimovaite, mwandishi wa ripoti ya Planet Mark; ni faida gani zinazopatikana katika jeneza la uyoga, "tunajua kwamba mazishi ya asili ndiyo yasiyotoa moshi, lakini si kila mtu anapenda kufungwa katika sanda ya pamba. Lakini watu wanaweza kupendelea jeneza la uyoga kwa sababu lina umbo."

Maiti kuwa mbolea

fqwe

Chanzo cha picha, Getty Image

Mwanafunzi wa usanifu Katrina Spade alichunguza nini kingeweza kufanywa ili kufanya mazishi katika miji yasiwe na ubadhirifu. Suluhisho lake ni kuiweka maiti kwenye mbolea kwenye sanduku lenye udongo wa rutuba ambao familia inaweza kuuweka kwenye bustani yao.

Spade alizindua kituo cha kwanza cha kutengeneza mbolea ya binadamu duniani, huko Seattle mwaka 2020. Washington lilikuwa jimbo la kwanza la Marekani kuhalalisha mbolea ya binadamu mwaka huo huo, na zoezi hilo sasa ni halali katika majimbo saba ya Marekani.

Hadi sasa ameshughulikia karibu miili 300. Mchakato huo hufanyika kwa muda wa wiki tano hadi saba. Mwili hulazwa - huzungungukwa na mbao, alfalfa na majani. Mifupa na meno - ambayo hayaozi - huondolewa, huvunjwa, na kuongezwa kwenye mbolea.

‘’Lakini mbolea haitengenezwi ikiwa mtu amekufa kwa Ebola, ugonjwa wa ubongo unaoambukiza, au kifua kikuu, kwani vimelea vya magonjwa hayo haviharibiki kwa kutengeneza mbolea,’’ anasema Spade.

Kuyeyusha maiti

Lipo chaguo jingine; njia ya uyeyushaji maiti, ilikuwa chaguo la Askofu Mkuu Desmond Tutu, ambaye alisaidia kukomesha ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Ni njia bora zaidi kuliko uchomaji maiti, huzalisha kilogramu 20 tu za CO2. Inapunguza kiasi kikubwa cha hewa chafu ikilinganishwa na uchomaji moto.

Takriban lita 1,500 (galoni 330) za maji huchanganywa na asidi, na kupashwa moto hadi nyuzi joto 150C (302°F) kwa masaa manne. Zaidi ya watu 20,000 wameyeyushwa katika kipindi cha miaka 12 iliyopita, haswa nchini Merikani.

Ninapozingatia chaguzi mbalimbali ambazo nimejifunza – kuyeyushwa, kufanywa mbolea, kuzikwa na jeneza la uyoga. Ninaafiki mazishi ya asili ya kufungwa sanda ya pamba pekee. Nimefurahi kwamba Trofimovaite amefikia hitimisho sawa. "Mazishi ya asili ndiyo yanayovutia zaidi."