Jinsi nchi za Magharibi zinavyopoteza ushawishi barani Afrika

tt

Chanzo cha picha, AFP

  • Author, Na Andrew Harding
  • Nafasi, BBC News, Johannesburg

Eneo tajiri zaidi la Afrika linaanda kongamano kubwa wiki hii huku kukiwa na mchanganyiko wa fahari,afueni na dalidli za wasi wasi fulani.

Sandton - wilaya iliyopo nje kidogo ya jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini - ndio mahali ambapo mkutano wa hivi punde zaidi wa Brics utafanyika. Huu ni muungano wa mataifa yanayoimarika zaidi kiuchumi duniani unaojumuisha Brazil, Urusi, India, China, na Afrika Kusini zilizokuja pamoja kupinga ushawishi wa nchi za Magharibi katika masuala ya kimataifa. Makumi ya mataifa mengine yanapanga foleni kujiunga.

Afueni iliyopatikana Afrika Kusini kuhusiana na Brics inaweza kuelezewa na uamuzi wa hivi karibuni wa Rais wa Urusi Vladimir Putin kutohudhuria mkutano huo.

Laiti angesisitiza kuja, Afrika Kusini ingejipata mashakani kujaribu kufafanua msimamo wake katika utekelezaji wa wajibu wake wa kimataifa wa kumkamata kiongozi huyo wa Urusi kwa madai ya uhalifu wa kivita nchini Ukraine.

Baada ya kuepuka changamoto hiyo isiyo ya kawaida, maafisa wa Afrika Kusini sasa wanafurahia jukumu lao kama mwenyeji - kwa ufahari mkubwa imekuwa ikisambaza mwaliko kadha wa kadha kwa waandishi wa habari kuhusu mikutano ya kiamsha kinywa ya Brics, maonyesho ya biashara, midahalo ya mijini na kadhalika.

Kiwango hiki kisicho cha kawaida cha shauku rasmi kinasaidia, kwa baadhi ya watazamaji, kusisitiza jinsi nchi hii inavyoonekana kujitenga na nchi za Magharibi, sio tu kuelekea ulimwengu wenye uwezo mkubwa , lakini kwa uthabiti ndani ya China na, kwa kiwango kidogo mzunguko wa Urusi.

Rais Putin wa Urusi

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Rais Putin wa Urusi anatarajiwa kushiriki mkutano huo kupitia mtandaoni.

Katika kikao cha awali cha mawaziri wa mambo ya nje wa Brics mjini Cape Town hivi majuzi, mwandishi wa habari wa Urusi alininong'onezea katika mkutano wa waandishi wa habari na kusema: "Unaweza kusalia na paradiso yako ya haki za binadamu [ huko Magharibi]. Tunabuni ulimwengu mpya."

Brics huenda bado ni changa, lakini inavutia - katika sehemu fulani - hisia ya aina ya msisimko na nguvu ya kuvuruga hali ya kawaida.

Mfanyakazi mwenzangu aliyehudhuria warsha ya sera za mambo ya nje iliyoandaliwa na serikali ya Afrika Kusini aliniambia juu ya maafikiano makubwa huko kwamba China ndio tegemeo la siku zijazo, na Magharibi ilikuwa ikidorora.

Hapo ndipo hali ya wasiwasi ya Afrika Kusini inapoiwekwa kwenye mizani.

Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa - mfanyabiashara tajiri - anafahamu fika kwamba uchumi wa ndani, ulioathiriwa sana na Covid na kukabiliwa na viwango vya juu zaidi vya ukosefu wa ajira na usawa, unahitaji sana uwekezaji zaidi wa kigeni ikiwa anataka kuepusha kuongezeka mgogoro.

Urusi hakika sio jibu. Uhusiano wake wa kibiashara na Afrika Kusini ni kama haupo.

China inazidi kuwa mshirika muhimu lakini, hata hivyo, imegubikwa hapa na biashara ya muda mrefu, na uwekezaji kutoka, Umoja wa Ulaya (EU) na Marekani.

Kwa hivyo ni kwa nini Afrika Kusini itahatarishaje uhusiano huo muhimu wa Magharibi - ambao tayari una matatizo - wakati inakabiliwa na hali ya kutokuwa na uhakika wa kiuchumi?

Jibu, kwa kiasi, linaonekana kuwa ndani ya chama tawala nchini kinachozidi kupoteza ushawishi na kukosa mwelekeo.

Baada ya miongo mitatu madarakani, Chama cha African National Congress (ANC) kinajitahidi kujinasua na vita, ufisadi na machafuko ya kiutawala.

Ikikabiliwa na vita nchini Ukraine, kwa mfano, serikali ya Afrika Kusini imetoa majibu yaliyochafuka - kwanza kulaani uvamizi huo, kisha ikakataa waziwazi kulaani, kisha kuilaumu Nato, ikimsifu Bw Putin, ikijitolea kama mpatanishi wa amani, kuandaa mazoezi ya wanamaji wa Urusi, kukimbilia kujieleza kwa Washington, na kurudia mazungumzo ya Kremlin kiholela.

Halafu kuna kitendawili ambacho bado hakijateguliwa cha iwapo Afrika Kusini ilisambaza silaha kwa Urusi mwaka jana - kama inavyodaiwa na Marekani.

Kuna shaka kidogo kwamba Rais Ramaphosa hana wasiwasi sana kuhusu uvamizi wa Urusi na ana wasiwasi wa kujionyesha kama mtetezi mwenye busara na asiyeegemea upande wowote kwa ulimwengu huo wa nchi nyingi zaidi.

Lakini baadhi ya maafisa katika serikali yake na chama chake mara kwa mara hudhoofisha msimamo huo - mara nyingi wakitoa mfano wa kutaka kuungwa mkono na Moscow wakati wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na tuhuma za jumla zaidi za sera za kigeni za Marekani.

Ujumbe huo wa kubahatisha umeuudhi pande zote katika mzozo huo na kufanikiwa kuifanya Afrika Kusini kuonekana dhaifu na isiyo na maamuzi.

"Taifa la upinde wa mvua" la Nelson Mandela hakika linatatizika hivi sasa - huku wengine wakionya kwamba hivi karibuni linaweza kuwa "nchi iliyofeli".

Afrika Kusini inafurahia jukumu lake kama mwenyeji wa mkutano wa kilele wa Brics, ambao utakamilika Alhamisi

Chanzo cha picha, BRICS HANDOUT/GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Afrika Kusini inafurahia jukumu lake kama mwenyeji wa mkutano wa kilele wa Brics, ambao utakamilika Alhamisi

Lakini mkutano wa kilele wa Brics wa wiki hii, kwa kulinganisha, utaipa Kremlin jukwaa muhimu la kuonyesha diplomasia yake, ya kimkakati zaidi na yenye ufanisi.

Vichwa vya habari vya hivi majuzi kutoka bara hili huenda vilitawaliwa na mapinduzi ya Niger, na uwezekano wa mamluki wa kundi la Wagner kutoka Urusi kutumia vibaya machafuko hayo kwa manufaa yao, kama walivyofanya nchini Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Lakini cha muhimu zaidi ni mafanikio ambayo Moscow, kupitia kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov, na kupitia ujumbe wa vyombo vya habari, imeweza kujionyesha - baada ya miongo kadhaa bila uwepo katika bara - kama njia mbadala ya " ukoloni" na ushawishi wa nchi za Magharibi ndani ya Afrika.

Katika nchi zinazopambana na umaskini, athari za mabadiliko ya hali ya hewa, ongezeko la idadi ya vijana, na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira, kukatishwa tamaa na hali ilivyo, baadhi ya watu hawana budi kutafuta njia mbadala ya kujinasua.

Hii inazua swali - Je, mataifa ya Magharibi yamekuwa yakifanya nini ili kutoa changamoto kwa Urusi?

Bila shaka, ni hatari kutoa maoni ya jumla kuhusu bara hili, na ni makosa kuashiria kwamba serikali za Kiafrika zinatumika kama chambo cha kufufua Vita Baridi.

Lakini iko wapi toleo la Magharibi la Brics? Uingereza ina "waziri wa Afrika" - lakini ni kama hayupo kwa sababu hakuna mtu ambaye amewahi kujitolea kukaa kazini kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Kushughulishwa na miradi ya maendeleo, masharti magumu na mialiko ya kigeni iliyochaguliwa kwa viongozi wa Kiafrika wanaopendelewa, kumechochea madai kwamba Ufaransa, Uingereza na mataifa mengine ya zamani ya kikoloni bado yanalichukulia bara hili kama shida inayochosha kusimamiwa, badala ya mshirika wa kuungwa mkono.

Hii huenda si haki. Licha ya yote hayo, mataifa ya Magharibi, kwa miongo kadhaa, yametumia nishati na pesa taslimu kusaidia huduma za afya, biashara na serikali katika bara zima.

Lakini jukumu la majeshi ya Magharibi - wanajeshi wa Ufaransa na ndege zisizo na rubani za Kimarekani - katika maeneo kama vile Niger na Somalia, kumesababisha upinzani mkali.

Ambayo inaweza kusaidia kueleza kwa nini maono mbadala ya Brics yanapata umaarufu katika bara hili, na kwa nini muungano huo utatoa hoja yake, kwa sauti kubwa na kwa uhakika, katika kumbi za mikutano za Sandton wiki hii.

Ramani
Pia uanaweza kusoma: