Je, unaweza kujua ni saa ngapi ukiwa mwezini?

dcxz

Chanzo cha picha, Getty Image

Maelezo ya picha, Siku moja ya mwezini ina masaa 708.7

Hakuna anayeweza kusema ni saa ngapi akiwa mwezini kwa sasa. Wakati ambapo nchi nyingi zinapanga kukanyaga mwezi na kufanya kazi huko katika siku zijazo, kuna mjadala ikiwa ni bora kuweka wakati rasmi kwenye mwezi pia.

Shirika la Anga za Juu la Ulaya linasema kuweka wakati rasmi uliokubaliwa katika mwezi kutakuwa na manufaa kwa mashirika mbalimbali ya utafiti wa anga duniani kote.

Shirika linasema ni muhimu kutengeneza ramani ya nyakati katika mwezi na kutambua maeneo ya mwezi ili iwe rahisi kutoka eneo moja hadi jingine.

Shirika la Anga la Ulaya linafanya kazi na NASA kushughulikia jambo hili. Kwa sasa, Saa ya Ulimwenguni (UTC) inatumika kwa misheni zote kwa sababu mwezi hauna masaa yake.

Shirika la Anga za Juu la Ulaya linasema kuwa UTC haiwezi kutegemewa kwa misheni za kwenda mwezini. Muda sahihi kwenye mwezi ni muhimu kwa vyombo vya anga vya juu kufanya kazi kwa ufanisi.

Kwa nini hakuna saa katika mwezi?

dscxz

Chanzo cha picha, Getty Image

Maelezo ya picha, Siku moja kwenye mwezi ni sawa na siku 29 duniani

Maafisa wa anga za juu wa Ulaya wanasema shirika la anga za juu linafaa kuwajibika kuweka muda wa mwezi. Saa kwenye eneo la mwezi la Chandamama hukimbia kwa kasi zaidi kuliko duniani, kwa hivyo kuweka wakati sawa na wa dunia kutaleta shida kidogo.

Ikilinganishwa na saa 24 za duniani ambayo ni siku moja. Siku moja ya mwezini ina masaa 708.7. Hii ni kwa sababu nguvu ya mvutano (gravity) katika mwezi ni ndogo.

Hii inaweza kuwa sababu kwa nini wanaanga kwenye mwezi huweka miadi yao mbele ya wakati wa duniani. Kufuata saa za kwenye mwezi kunaweza isiwe sahihi kwa duniani.

Saa Zone ni nini?

DCX

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Je, saa za mwezini na duniani zinapaswa kuwa sawa?

Maeneo ya dunia yamegawanywa katika kanda za wakati kulingana na mistari ya kufikirika inayoitwa meridians. Mistari hiyo inatoka ncha ya kusini hadi ncha ya kaskazini.

Greenwich Standard Time au GMT ni muda uliobainishwa kulingana na mstari wa greenwich unaopita karibu na London, Uingereza.

Siku moja ya duniani imegawanywa katika masaa 24. Nchi zilizo mashariki mwa mstari wa greenwich ziko mbele ya Uingereza. Nchi za Magharibi ziko nyuma ya Uingereza. .

Siku moja kwenye mwezi ni sawa na siku 29 duniani. Lakini pia kuna maswali mengi kuhusu saa kwenye mwezi. Je, saa za mwezini na duniani zinapaswa kuwa sawa? Au ziwe tofauti?

NASA iko kwenye ratiba ya kuzindua safari yake ya kwanza ya mwezini baada ya miaka 50, 2025. Katika misheni ya Artemi, nchi hiyo itatuma mwanamke mwezini kwa mara ya kwanza.