'Tunawaangalia wezi wakiwachukua watoto wetu'

Maelezo ya video, Mgogoro wa utekaji nyara Nigeria: ‘Tunawaangalia wezi wakiwachukua watoto wetu’
'Tunawaangalia wezi wakiwachukua watoto wetu'

Nigeria imekumbwa na matukio matatu ya utekaji nyara katika wiki moja iliyopita, huku utekaji nyara mkubwa zaidi ikifanyika Alhamisi iliyopita, ambapo zaidi ya watoto 280 walichukuliwa shuleni na watu wenye silaha Kuriga, katikaJimbo la Kaduna.

Mwandishi wa BBC Chris Ewokor amesafiri hadi Kaduna na kukusanya ushuhuda mkali kutoka kwa mama aliyekuwa akisubiri kwa hamu habari za mwanawe aliyetekwa nyara na mmoja wa wavulana waliofanikiwa kutoroka.