Kambi ya Wanazi ya Ravensbrück: Jinsi wanawake wa kawaida walivyobadilika na kuwa wanaotesa wengine

Ravensbrück women guards

Chanzo cha picha, Gedenkstätte Ravensbrück

Maelezo ya picha, Walinzi wa kike huko Ravensbrück (picha iliyopigwa takriban mwaka 1940)

"Wafanyakazi wa afya wa kike wenye umri kati ya miaka 20 hadi 40 wanatakikana kufanya kazi katika maeneo ya jeshi," lilisomeka tangazo la kazi kwenye gazeti la Ujerumani la mwaka 1944.

Kwa ambao wangechaguliwa, waliahidiwa mishahara mizuri, chakula bila malipo, malazi na mavazi.

Kile kisichotajwa ni kwamba mavazi yao yalikuwa sare ya kikosi cha SS wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia. .

Na kwamba "maeneo ya jeshi" ni kambi ya mateso ya Ravensbrück dhidi ya wanawake.`

Leo hii, kambi hiyo ya mbao hafifu na hatari ya wafungwa ni mambo ya zamani.

Kilichobaki ni shamba tupu lenye miamba, karibu kilomita 80 (maili 50) kaskazini mwa Berlin.

View of Ravensbrück in 1945

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muonekano wa Ravensbrück mwaka 1945

Lakini bado kuna nyumba nane thabiti zilizojengwa, majengo ya kupendeza yenye vifuniko vya mbao na ushoroba.

Pia kuna nyumba za Wanazi za Wajerumani za mwaka 1940.

Hapo ndipo walinzi wa kike waliishi, wengine na watoto wao.

Kutoka vibarazani wangeweza kuona msitu na ziwa zuri.

"Ilikuwa ni wakati mzuri sana maishani mwangu," alisema mlinzi mmoja wa zamani wa kike, miongo kadhaa baadaye.

Lakini kutoka kwenye vyumba vyao vya kulala pia wangeweza kuona vikundi vya wafungwa na mabomba ya kutoa moshi kwenye vyumba vya gesi.

Female guard Johanna Langefeld with her son and another guard's daughter

Chanzo cha picha, Gedenkstätte Ravensbrück

Maelezo ya picha, Guard Johanna Langefeld akiwa na kijana wake na binti wa mlinzi mwingine wa mwanamke

Wageni wengi wanaokuja kwenye eneo la ukumbusho wanaulizia juu ya wanawake hawa.

Hakuna maswali mengi sana utayasikia juu ya wanaume wanaliofanya kazi katika mashamba hayo," anasema Andrea Genest, mkurugenzi wa jumba la kumbukumbu huko Ravensbrück, wakati ananionesha mahali ambapo wanawake hao waliishi.

"Watu hawapendi kufikiria kwamba wanawake wanaweza kuwa wakatili mno."

Wanawake wengi vijana waliotoka katika familia masikini, waliacha shule mapema na walikuwa na nafasi chache katika taaluma zao.

Kazi katika kambi ya mateso ilimaanisha mshahara wa juu, malazi mazuri na uhuru wa kujitegemea kifedha.

"Ilikuwa ya kuvutia zaidi kuliko kufanya kazi kiwandani," anasema Dkt. Genest.

Wengi walikuwa wamefundishwa mapema katika vikundi vya vijana vya Wanazi na waliamini itikadi ya Hitler.

"Walihisi wanaunga mkono jamii kwa kufanya kitu dhidi ya maadui zake," alisema.

Ravensbrück crematorium

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kambi za mateso: mauaji yaliendelea hadi wakati wa ukombozi

Nyumba za kujivinjari na vilevile za mateso

Ndani ya nyumba moja, maonyesho mapya yanaonyesha picha za wanawake hao wakiwa katika wakati wao wa ziada.

Wengi walikuwa katika miaka yao ya ishirini, wazuri wakiwa na mitindo mbalimbali ya nywele.

Picha zinawaonyesha wakitabasamu wakati wakipata kikombe cha kahawa na keki nyumbani.

Au wakicheka, wakiwa wameshikana mikono wanapokwenda kutembea kwenye msitu wa karibu wakiwa wameandamana na mbwa.

Place marker for a female guard at Christmas table

Chanzo cha picha, Gedenkstätte Ravensbrück

Maelezo ya picha, Kadi ya Krismasi kwa walinzi wanawake wa kikosi cha SS

Matukio yanaonekana kuwa hayana hatia - mpaka utakapoona alama za sare za kikosi cha vita vya pili dunia - SS kwenye nguo za wanawake hao, na unakumbuka kwamba mbwa hao hao wa Alsatia walitumiwa kutesa watu katika kambi za mateso.

Wanawake 3,500 walifanya kazi kama walinzi katika kambi za mateso za Wanazi, na wote walianzia huko Ravensbrück.

Wengi wao baadaye walifanya kazi katika kambi za kifo kama vile Auschwitz-Birkenau au Bergen-Belsen.

Liberation of Ravensbrück, 30 March 1945

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ukombozi wa kambi ya Ravensbrück, Machi 30, 1945

"Walikuwa watu wabaya" Selma van de Perre wa miaka 98 ananiambia kwa simu kutoka nyumbani kwake London.

Alikuwa mpiganaji wa upinzani wa Kiyahudi wa Uholanzi ambaye alifungwa huko Ravensbrück kama mfungwa wa kisiasa.

"Walipenda sana kutesa watu pengine kwasababu iliwapa nguvu. Iliwapa nguvu nyingi juu ya wafungwa. Wafungwa wengine walitendewa unyama sana. Walipigwa."

2px presentational grey line

Mengi zaidi kuhusu vita vya Wanazi na Hitler:

2px presentational grey line

Selma alifanya kazi chini ya ardhi katika Uholanzi iliyokaliwa na Wanazi na kwa ujasiri alisaidia familia za Kiyahudi kutoroka.

Mnamo mwezi Septemba, alichapisha kitabu nchini Uingereza juu ya uzoefu wake, kwa jina 'My Name Is Selma', yaani jina langu ni Selma.

Mwaka huu kitatolewa katika nchi zingine ikiwa ni pamoja na Ujerumani.

Wazazi wa Selma na dada yake kijana waliuawa katika kambi hizo, na karibu kila mwaka anarudi katika kambi ya Ravensbrück kushiriki katika hafla za kuhakikisha uhalifu uliofanywa hapo hausahauliki.

Ravensbrück ilikuwa kambi kubwa zaidi ya wanawake chini ya Wanazi nchini Ujerumani.

Zaidi ya wanawake 120,000 kutoka kote Ulaya walifungwa huko.

Wengi walikuwa wapiganaji wa upinzani au wapinzani wa kisiasa.

"Wengine walionekana kuwa "wasiostahili" kwa jamii ya Wanazi: Wayahudi, wasagaji, wafanyabiashara ya ngono au wanawake wasio na makazi.

Takriban wanawake 30,000 walifariki dunia hapo.

Wengine waliwekewa gesi au kunyongwa, wengine walikufa njaa, walikufa kwa magonjwa au walifanyishwa kazi hadi kufa.

Walitendewa ukatili na walinzi wengi wa kike - walipigwa, kuteswa au kuuawa.

Wafungwa waliwapa majina ya utani, kama "Brygyda mwenye damu" au Anna bastola."

Chris van Houts
They were ordinary women doing diabolical things. I think it's possible with loads of people
Selma van de Perre
Ravensbrück survivor
1px transparent line

Baada ya vita, wakati wa majaribio ya uhalifu wa kivita wa Wanazi mnamo mwaka 1945, Irma Grese alipewa jina la "jinamizi mzuri" na waandishi wa habari.

Kijana wa kupendeza, alipatikana na hatia ya mauaji na akahukumiwa kifo kwa kunyongwa.

Mwanamke katili aliyevalia sare ya SS baadaye alikua mtu wa ibada ya ngono katika filamu na vichekesho.

Lakini kati ya maelfu ya wanawake ambao walifanya kazi kama walinzi wa SS, ni 77 tu waliofikishwa mahakamani.

Na ni wachache sana waliohukumiwa.

Himmler visiting Ravensbrück, Jan 1941

Chanzo cha picha, Gedenkstätte Ravensbrück

Maelezo ya picha, Mkuu wa kikosi cha SS Heinrich Himmler akitembelea kambi ya Ravensbrück (Januari mwaka 1941)

Walijionyesha kama wasaidizi wenye huruma - katika mfumo dume wa baada ya vita wa Ujerumani Magharibi.

Wengi hawajawahi kuzungumzia yaliyopita.

Walioa, walibadilisha majina yao na kufifia katika jamii.

Mwanamke mmoja, Herta Bothe, ambaye alifungwa kwa utekelezaji wa vitendo vya kinyama, baadaye alizungumza hadharani.

Alisamehewa na Waingereza, baada ya miaka kadhaa gerezani.

Katika mahojiano adimu, yaliyorekodiwa mnamo mwaka 1999 kabla tu hajafariki dunia, hakuwahi kutubu au kuomba msamaha.

"Je nilifanya makosa? Hapana. Makosa ni kwamba ilikuwa kambi ya mateso, lakini ilibidi niende huko, vinginevyo mimi mwenyewe ningewekwa ndani. Je hilo lilikuwa kosa langu?."

Hicho kilikuwa kisingizio ambacho mara nyingi kilitolewa na walinzi wa zamani. Lakini haikuwa kweli.

Rekodi zinaonyesha kwamba waajiriwa wengine wapya waliondoka Ravensbrück mara tu walipogundua kazi hiyo inahusu nini.

Waliruhusiwa kwenda na hawakushiriki yaliyotokea.

Nilimuuliza Selma ikiwa anafikiria walinzi walikuwa majinamizi.

"Nadhani walikuwa wanawake wa kawaida wanaofanya mambo ya kishetani. Nadhani inawezekana na watu wengi, hata huko England. Nadhani hiyo inaweza kutokea mahali popote. Inaweza kutokea hata hapa ikiwa inaruhusiwa."

Ni somo kwetu sote, anaamini hivyo.

Ravensbrück women guards

Chanzo cha picha, Gedenkstätte Ravensbrück

Maelezo ya picha, Licha ya uhalifu uliotendwa, ni wanawake wachache sana walinzi walioshtakiwa baada ya vita

Tangu wakati wa vita vya maafisa wa kike enzi ya vita vya pili vya dunia, walinzi wamekuwa wakihusishwa katika vitabu na fila

Maarufu zaidi imekuwa kitabu cha 'The Reader', riwaya ya Ujerumani ambayo baadaye ikawa filamu iliyoigizwa na Kate Winslet.

Wakati mwingine wanawake huonyeshwa kama waathiriwa wanaonyanyaswa.

Wakati mwingine ni kama majinamizi katili.

Ukweli ni wa kutisha zaidi.

Hawakuwa majinamizi wa ajabu, badala yake, wanawake wa kawaida ambao waliishia kufanya mambo mabaya.