Mzozo wa Ukraine: Hii ni mifano ya mbinu ya"bendera feki" vitani

.

Chanzo cha picha, Reuters

Wakati wasiwasi ukiongezeka bada ya Urusi kuivamia Ukraine, Uingereza na Marekani huenda wakatumia mashambulizi ya "bendera feki" na kutumia mbinu hiyo kama kisingizio cha kuvamia jirani yao.

Waasi wanaoungwa mkono na Urusi walilituhumu jeshi la Ukraine kwa kuanzisha mfululizo wa mashambulizi na kuwataka raia wake kuondoka.

Mbinu hii ya "bendera feki" ikoje hasa?

Neno "bendera feki ama bendera ya uongo" linamaanisha hatua yoyote ya kisiasa au kijeshi inayofanywa kwa lengo la kumtupia lawama mpinzani. Mataifa mengi kwa muda mrefu yamekuwa yakikimbilia kutumia mbinu hii kwa kuanzisha mashambulizi ya kweli au ya kufikirika kwa majeshi au sehemu zao na kuushutumu upande mwingine kufanya hivyo na hivyo kutumia hiko kama kisingizio cha kuanzisha vita.

Kwa ufupi ni kutumia bendera ya mpinzani wako, ama nchi nyingine kwenda kumvamia mpinzani wako, ili kuficha utambulisho wako na kukwepa lawama za kuanzisha mzozo ama vita.

Neno hilo lilitumika kwa mara ya kwanza katika karne ya 16 kuelezea jinsi maharamia walivyopandisha bendera ya nchi ya kirafiki kuzihadaa meli za wafanyabiashara, ili waweze kuzikaribia, kuzishambulia kwa kushtukiza, na kupora vyombo vya kibiashara.

Hii ni baadhi ya mifano maarufu zaidi ya matumizi ya mbinu au ujanja huo katika historia.

Ujerumani ilipoivamia Poland mwaka 1939

Usiku mmoja kabla ya Ujerumani kuivamia Poland, askari saba wa kikosi maalum cha Ujerumani walijifanya kuwa wanajeshi wa Poland na kuvamia kituo cha redio huko Glyftz

Chanzo cha picha, NURPHOTO VIA GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Usiku mmoja kabla ya Ujerumani kuivamia Poland, askari saba wa kikosi maalum cha Ujerumani walijifanya kuwa wanajeshi wa Poland na kuvamia kituo cha redio huko Glyftz

Usiku mmoja kabla ya Ujerumani kuivamia Poland, askari saba wa kikosi maalum cha Ujerumani walijifanya kuwa wanajeshi wa Poland na kuvamia kituo cha redio huko Glyftz mpakani mwa nchi hizo. walituma ujumbe mfupi wakisema kwamba kituo hicho sasa kilikuwa mikononi mwa Poland.

Wanajeshi hao pia wamuacha mtu mmoja aliyevalia kama mwanajeshi wa Poland ili ionekane kana kwamba ameuawa kwa kushambuliwa.

Vita ya Urusi na Finland mwaka 1939

Wanahistoria wamehitimisha kwa kusema kwamba kushambuliwa kwa kijiji hicho haukufanywa na jeshi la Finland, lakini ulipangwa vikosi vya usalama vya Soviet

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wanahistoria wamehitimisha kwa kusema kwamba kushambuliwa kwa kijiji hicho haukufanywa na jeshi la Finland, lakini ulipangwa vikosi vya usalama vya Soviet

Katika kipindi cha mwaka huo huo, Kijiji kimoja cha Urusi cha Mainella kilishambuliwa kwa makombora ya Artillery. Kijiji hicho kilikuwa karibu na mpaka wa Finland, na muungano wa Soviet ulitumia shambulio linalodaiwa kuvunja makubaliano ya kati yake na Finland kabla ya kuanzisha vita vya majira ya baridi.

Wanahistoria wamehitimisha kwa kusema kwamba kushambuliwa kwa kijiji hicho haukufanywa na jeshi la Finland, lakini ulipangwa vikosi vya usalama vya Soviet.

Tukio la Tonkin la mwaka 1964

.

Chanzo cha picha, UNIVERSAL IMAGES GROUP VIA GETTY IMAGES

Agosti 2, 1964, vilitokea vita vya majini vikihusisha boti za Marekani na Vietnam ya Kaskazini katika pwani ya Vietnam (Gulf ya Tonkin).

Meli za pande zote mbili ziliharibiwa, huku Vietnam ya Kaskazini ilipoteza watu wanne na wengine sita walijeruhiwa.

Usalama wa taifa Marekani lilidai kuwa siku mbili baadaye vita vingine kama hivyo vilitokea.

Lakini sasa inaonekana kuwepo kwa uwezekano kuwa shambulio la pili, ambalo Marekani inaishutumu Vietnam ya Kaskazini kutekeleza, kwamba halijawahi kutokea.

Nyaraka zilizothibitishwa mwaka 2005 zinaonyesha kuwa jeshi la wanamaji la Vietnam Kaskazini halikuwa likishambulia meli ya Marekani lakini lilikuwa likijaribu kuokoa boti mbili zilizoharibiwa katika vita vya kwanza.

"Watu wafupi wa kijani, Crimea mwaka 2014

Crimea

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Siku chache kabla ya Urusi kuliteka eneo la Crimea, watu waliovalia kama jeshi la Urusi wakiwa na silaha walianza kuonekana mitaani bila beji za Urusi katika sare zao za jeshi.

Siku chache kabla ya Urusi kuliteka eneo la Crimea, watu waliovalia kama jeshi la Urusi wakiwa na silaha walianza kuonekana mitaani bila beji za Urusi katika sare zao za jeshi.

Urusi ilisisitiza kuwa hawa walikuwa wanachama wa "makundi ya kujilinda" ambayo yalitaka kurudisha himaya kwa Urusi kutoka mikononi mwa Ukraine.

Ilidaiwa kuwa watu hao walikuwa wamenunua nguo zao na silaha madukani.

Waandishi wa habari wa Urusi walikuwa wakiwaita "watu wenye roho nzuri," wakati wenyeji wa Crimea waliwaelezea kama "watu wadogo wa kijani," akimaanisha rangi ya sare zao isiyojulikana asili yake.

Kashmir mwaka 2000

.

Chanzo cha picha, NURPHOTO VIA GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, India na Pakistan kwa muda mrefu zimekuwa zikishutumiana kwa mashambulizi ya uongo katika mpaka wa eneo linalozozaniwa la Kashmir ili kuchochea mzozo wa kijeshi.

India na Pakistan kwa muda mrefu zimekuwa zikishutumiana kwa mashambulizi ya uongo katika mpaka wa eneo linalozozaniwa la Kashmir ili kuchochea mzozo wa kijeshi.

Mwaka 2020, wizara ya mambo ya nje ya Pakistan ilivishutumu vikosi vya India kwa kuishambulia kwa risasi gari lililokuwa limebeba waangalizi waliokuwa upande wa mpaka wa Pakistan wakiamini Umoja wa Mataifa utaaamini kwamba mashambulizi hayo yamefanywa na vikosi vya Pakistan.

India inajaribu kuchochea mzozo kati ya Pakistan na Jumuiya ya kimataifa, wizara hiyo imesema, ikimwelezea waziri mkuu wa Pakistan Imran khan kama "asiyejali".

India ilikanusha madai hayo na kuilaumu Pakistan kwa kushindwa kudumisha usalama kwenye mpaka wake.