Haiti kuunda serikali ya mpito

Haiti kuunda serikali ya mpito

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Haiti kuunda serikali ya mpito

Wanasiasa nchini Haiti wametia sahihi makubaliano ya dakika za mwishi ya kubuni serikali ya mpito siku moja kabla ya rais Michel Martelly kuondoka madarakani bila ya kuwepo mrithi aliyechaguliwa.

Makubaliano hayo yaliyotiwa sahihi na marais wa bunge zote mbili yanaizuia nchi kutokana na kutumbukia katika hali ya kutokuwa na kiongozi.

Shughuli ya kumchagua mrithi wa bwana Martelly ilihairishwa mwezi uliopita kutokana na hofu ya kutokea ghasia na kuwepo kwa udanganyifu.

Shughuli ya kumchagua mrithi wa bwana Martelly ilihairishwa mwezi uliopita kutokana na hofu ya kutokea ghasia na kuwepo kwa udanganyifu.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Shughuli ya kumchagua mrithi wa bwana Martelly ilihairishwa mwezi uliopita kutokana na hofu ya kutokea ghasia na kuwepo kwa udanganyifu.

Chini ya makubaliano hayo bunge litamchagua rais wa kipindi cha mpwito ambaye atahudumu mwa muda wa miezi minne.

Uchaguzi wa nchi hiyo sasa umepangiwa kufanyika tarehe 24 mwezi Aprili.