Kwanini dhana kwamba saratani inaua inaweza kudhuru afya yako

Na Christine Ro,

Mwandishi wa Makala

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuwa na saratani sio kwamba sasa umehukumiwa kifo, lakini ni imekuwa kawaida watu wengi huamini hivyo.

Leonora Argate alipopata uvimbe kwenye titi lake, jambo la kwanza alilohisi lilikuwa hofu. Aliwaza, "Saratani haionekani kuwa na tiba, sivyo?"

Argate, mwenye umri wa miaka 64 ambaye anaishi nyumbani kwake na watu wengine tisa na mmiliki wa sari-sari (duka dogo la bidhaa za rejareja ) huko Taguig, Ufilipino, alisita kutembelea kituo cha afya ili kuthibitisha kile alichoshuku.

Ilichukua karibu mwezi mmoja kabla ya kukubali kwenda kuchunguzwa. Na baada ya kugunduliwa ana saratani ya matiti, hakufika hospitalini kwa ajili ya kupata ushauri wa upasuaji. "Kwa kweli sikutaka kupata matibabu kwa sababu niliogopa," anaeleza. Binamu yake alikuwa amefariki kutokana na saratani licha ya kufanyiwa upasuaji.

Jirani wa Argate pia alikuwa amepatwa na saratani na akampeleka kwa daktari.

Wasaidizi wa wagonjwa (Patient navigators) ni wahudumu wa afya au kijamii ambao huwaongoza wagonjwa kupitia hatua mbalimbali za kukabiliana na hali ya kiafya, ambayo inaweza kujumuisha kuwaunganisha na usaidizi wa kifedha na usafiri.

Jiji anakoishi Argate, Taguig, lina mpango wa usaidizi wa wagonjwa kwa watu walio na saratani ya matiti, kwa ushirikiano kati ya maafisa wa afya na Wakfu wa iCanServe.

Saratani ya Argate ilipitia hatua kadhaa. Lakini kufuatia upasuaji, tiba ya mionzi na dawa, sasa yuko katika hali ya kutoweka au kuisha kwa seli za saratani.

Mabadiliko haya ya kimwili yameambatana na mabadiliko ya mtazamo wake kuhusu saratani. Hapo awali alihisi kutokuwa na tumaini juu ya ugonjwa huo - kama watu wengi wanavyohisi, kote ulimwenguni.

Wanasaikolojia, wahudumu wa afya na wengine wamekuwa wakichunguza jambo hili, linalojulikana kama kifo cha saratani, ili kuelewa ni kwa nini hali hii ni endelevu na kuwasaidia watu kuchukua hatua mapema.

Matumaini ni kwamba siku moja utafiti huu unaweza kuokoa maisha.

Kwanini imani kwamba saratani inaua ni ngumu

Imani kwamba saratani inaua imekuwa ngumu kuifafanua. Inafikiriwa kwa ujumla kama imani kwamba matokeo hayawezi kubadilishwa.

Kwa Oscar Esparza-Del Villar, profesa wa saikolojia katika Chuo cha Universidad Autónoma de Ciudad Juárez huko Mexico, anasema kile ambacho watu wengine hukiita kuwa kifo kinaweza kutengwa na mambo yanayohusiana kama vile kutokuwa na msaada na imani katika udhibiti wa kimungu .

Watafiti waligundua kuwa hatari na mambo haya yanayohusiana, ni kutokuwa na uwezo ambao huathiri mtu kiafya zaidi.

Imani kuwa saratani inaua inaweza kuwa na misemo tofauti sana katika tamaduni tofauti, lakini inaonekana ulimwenguni kote katika viwango tofauti. Esparza-Del Villar alishirikiana na utafiti wa nchi sita wa kuhusu imani kwamba saratani inaua.

"Tulishangazwa na idadi kubwa ya watu wa Ujerumani walikuwa katika kundi lililokuwa na kiwango cha juu cha watu wenye imani kuwa saratani inaua," Esparza-Del Villar anaelezea - zaidi ya Ghana, Kenya, Mexico, Nigeria au Uswizi. Hii ilikuwa kinyume na baadhi ya mitazamo kwamba saratani inaua ilikuwa ya kawaida zaidi katika nchi za kipato cha chini na cha kati.

Hii inaonyesha kwamba tathmini za kisaikolojia za imani kuwa saratani inaua zinapaswa kubadilishwa katika tamaduni tofauti. Esparza-Del Villar na wenzake waliunda kipimo cha kwanza cha kupima imani kuhusiana na kifo cha saratani ambacho kitatengenezwa kwa wakati mmoja katika lugha za Kihispania na Kiingereza .

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya aina za saratani zinatibika sana zinapopatikana mapema

Labda cha kushangaza, imani ya kufa inaweza kuwa na faida fulani. Katika utafiti na wahamiaji karibu na mpaka wa Mexico na Marekani , "wale walio na hatari kubwa ya kufa waliripoti viwango vya chini vya msongo wa mawazo na wasiwasi," Esparza-Del Villar anaelezea. "Ilikuwa kama sababu ya kinga kwao." Hakika, fimani ya kufa inaweza kutoa hisia ya katika kipindi kigumu.

Lakini, kuna uhusiano kati ya kifo na tabia zinazoweza kudhuru, haswa kuhusiana na saratani. Imani ya kifo imehusishwa na viwango vya chini vya uchunguzi wa saratani ya utumbo mpana nchini Ireland .

Nchini Ghana, baadhi ya watu wanasema kwamba hatima haiwezi kubadilishwa wanapokataa matibabu ya saratani ya matiti .

Nchini Marekani, watoto hutumia mafuta kidogo ya kuzuia jua wakati wazazi wao wana hatari na wana historia ya familia ya saratani ya ngozi- melanoma.

Nchini Ufilipino, “mielekeo ya kiafya ni ya kawaida,” anaripoti Janine Pajimna, mtaalamu wa mafunzo katika Kituo cha Matibabu cha St. Luke katika Jiji la Quezon, Ufilipino.

Yeye na wenzake hivi majuzi walitaja hatari ya saratani kama mchangiaji wa viwango vya chini sana vya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi nchini Ufilipino, ingawa inagunduliwa kwa kutumia kipimo cha bei ya chini kabisa.

Kuna msemao wa Kifilipino usemao - kung oras mo na, oras mo na , ambao Pajimna anautafsiri kama "wakati ni wakati wako, wakati wako umekwisha." Anahisi kwamba hisia hizo zinaweza kuwa na madhara.

"Taarifa hii ina makosa sana kwa njia ambayo baadhi ya wagonjwa wa Ufilipino hawatatafuta ushauri au kufuata matibabu ya kuokoa maisha ambayo yanaweza kurefushwa na/au kuboresha ubora wa maisha yao," Pajimna anasema. "Ni sawa na kukubali tu hatima zao bila kufanya chochote kwa sababu hiyo ndiyo imani yao," anasema.

Ugonjwa wa saratani ni wa kawaida sana

Ugonjwa wa saratani una pande mbili , anasema Laura Marlow, mtafiti mkuu katika Kitengo cha Sayansi ya Tabia ya Saratani katika Chuo cha King's College London nchini Uingereza. Moja ni kuepukika: wazo kwamba nguvu za nje husababisha saratani na haiwezi kuzuiwa .

Nyingine ni kutopona: imani kwamba ikiwa mtu ana saratani atakufa kutokana nayo .

Linapokuja suala la kutoweza kuepukika, usemi mmoja wa imani mbaya ambao Samuel Smith, profesa wa tabia ya saratani katika Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza anasema unatoa taswira kwamba ni ugonjwa hatari .

Kutoweza kuepukika ni sehemu moja ya hatari ya saratani, lakini "kipengele cha kutoweza kupona ni kile tunachotaka kushinda," Marlow anasema, kwa sababu katika hali nyingi huo sio ukweli tena.

Kinyume na hili, Smith asema, "ujumbe kuhusu saratani umekuwa thabiti kwa kiasi kuhusiana na viambishi vya mazingira kwa miaka mingi: usivute sigara, punguza unywaji wako wa pombe (hakuna iliyo bora zaidi), kudumisha uzito mzuri, kudumisha lishe bora, na kufanya mazoezi ya mwili."

Bado, kwa watu wengi, "neno saratani linamaanisha kifo," Malgorzata Polnik anasema. Polnik alikuwa muuguzi wa saratani kabla ya kuwa mtaalamu wa magonjwa ya akili huko Devon, Uingereza, ambako anaendelea kuwahudumia wateja wengi wenye saratani.

Katika uzoefu wake, wagonjwa wengi huacha kwenda kupata ushauri wa kimatibabu mara tu wanaposikia neno saratani.

Inaweza kuwa vigumu kusikia kitu kingine chochote - kama vile ukweli kwamba baadhi ya aina za saratani kimsingi ni magonjwa sugu, ambayo yanaweza kudhibitiwa vyema ikiwa yatapatikana mapema vya kutosha. "Ninaona kwamba kwa mgonjwa anayesikia neno hili lenye nguvu, husababisha mchakato mzima wa kutafakari na labda hawi tayari mara moja kuzungumzia juu ya matibabu yote," Polnik anaelezea.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watoto wa wazazi walio na imani kwamba saratani inaua huwa hawatumii cream ya jua mara kwa mara

Kwa kweli kuna vizuizi vingi vya kiutendaji na vya kimuundo vya kupata utambuzi au matibabu ya saratani. Lakini kulingana na mtu, majibu ya utambuzi na hofu ya tisho hili la kiafya inaweza kuwa muhimu vile vile, Smith anasema. Hii ni pamoja na wasiwasi wa saratani, hofu na imani ya kifo kuhusu saratani.

"Sote tunashikilia imani hizi kwa kiasi fulani," anasema Smith.

Mnamo 2015 aliandika kuhusu utafiti wa Marekani ambao uligundua kuwa 66% ya washiriki walidhani kwamba kila kitu husababisha saratani, na 58% yao walihusisha moja kwa moja saratani na kifo. Hii ni licha ya viwango vya maisha ya saratani kuongezeka kwa wakati , hasa katika nchi tajiri kama Marekani.

Marlow anaamini kwamba "vitu kama vile kifo ni hatari katika hatua ya awali ya saratani ," ambapo watu huepuka kufikiria juu ya mambo kama uchunguzi wa saratani. "Sio lazima wavumilie mambo mengine yote ambayo tunapaswa kuweka ili kusaidia watu kuweza kushiriki katika tabia hizi." Lakini vipengele vyote hivyo vinahitaji kushughulikiwa ili kuboresha matokeo ya afya.

Zaidi ya imani ya kifo

Polnik anapofanya kazi na wagonjwa wanaoamini kwamba saratani yao itawaua, yeye huzingatia kuuliza maswali badala ya kutoa taarifa. Kwa mfano, anauliza jinsi mawazo iwapo Mawazo hayo yanavyofaa, na kama yana msingi wa kweli. "Mapema au baadaye, huwa tunafikia hitimisho kwamba imani haina msingi," Polnik anasema. Kisha anaweza kuuliza ikiwa imani kama hizo zinawasaidia wagonjwa wake kutatua mizozo yao, au ikiwa inawazidishia wasiwasi walionao.

Aina hii ya mbinu ya hatua kwa hatua husaidia kupunguza mzigo wa mawazo unaowalemea kuhusiana na ugonjwa.

Imani zina nguvu lakini hazieleweki vizuri kila wakati. Kwa mfano, imani ya kidini sio sababu kuu inayofanya watu waaminifu wanaweza kuepuka hatua fulani za afya, kama inavyofikiriwa nyakati nyingine.

Kwa hakika, katika baadhi ya matukio mahudhurio ya huduma za kidini huhusishwa na uchunguzi zaidi dhidi ya saratani .

Pajimna anasema kuwa usawa ni muhimu. Ingawa baadhi ya watu wanaona kwamba imani ina manufaa kwa afya yao ya akili, baadhi ya watu huichukulia kwa kupita kiasi na huona ushahidi wa kisayansi kuwa ni batili, anasema. "Mtazamo huu unatumika kama kikwazo kwa tabia muhimu za kutafuta afya, kama vile kufanyiwa uchunguzi wa saratani wa mara kwa mara na kupokea chanjo za kuokoa maisha," anasema Pajimna.

Zaidi ya dini, sababu ambayo inaelezewa kwa kiasi kikubwa kifo cha saratani ni elimu . Bila shaka, elimu na elimu ya afya inaweza kuhusishwa na mambo mengine kama vile jinsia, kipato, na kabila , lakini baadhi ya utafiti unapendekeza kuwa mambo haya pekee hayatoshi kuelewa kwa ni nini imani ya kifo cha saratani imeenea sana katika vikundi fulani.

Mahala ambapo huduma ya afya haipatikani hatari ya saratani haishangazi, anasema Smith. Katika mazingira haya, saratani inaweza kusababisha viwango vya juu vya vifo kwa sababu mara nyingi hugunduliwa katika hatua ya baadaye au matibabu machache hupatikana.

Bila elimu, itakuwa rahisi kuwa na maoni yasiyofaa, lakini kwa kweli watu wanaweza kuboresha nafasi zao za kuishi kwa tabia rahisi kama vile kwenda kuchunguzwa.

"Ni muhimu kujaribu kushughulikia hilo na kujaribu kuhakikisha kuwa watu hao katika jamii wanaelewa kuwa sio jambo lisiloepukika," anasema Smith. Na hapo ndipo hadithi chanya zinahitajika hasa.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mitazamo sahihi kuelekea saratani inaweza kuzuia tabia nzuri kama vile kupata uchunguzi

Smith anatoa maoni kwamba imani kuhusu kifo cha saratani inapaswa kushughulikiwa sio tu kwa kiwango cha mtu binafsi, lakini pia katika kiwango cha jamii, ili kuhimiza uelewa wa umma wa saratani. "Kukutana na watu wanakoishi badala ya kuwatarajia waje kwako inaweza kuwa njia mojawapo ya kushughulikia hili," anasema Smith.

Kwa mfano, taasisi inayohusika na saratani ya utumbo nchini Uingereza,Bowel Cancer UK huandaa maonyesho ya barabarani nje ya maeneo kama vile maduka makubwa, ambapo watu wanaweza kutembelea na kujifunza zaidi kuhusu saratani ya utumbo.

Marlow anasema kuwa na uwezo wa kuzungumza na wataalamu wa afya kwa njia ya mazungumzo zaidi katika matukio kama vile maonyesho ya barabarani ni muhimu hasa "wakati watu wana ujuzi mdogo wa kiafya na wanaona vigumu kupata maana kwa kutumia mawasiliano ya maandishi".

Kwa ujumla, kwa sababu viwango vya elimu ni jambo muhimu zaidi katika hatari ya saratani, kupunguza tofauti za kielimu kunaweza kusaidia kushughulikia usawa mwingine unaoathiri afya.

Mbinu nyingine ni kukabiliana na ukosefu huo wa usawa katika upatikanaji wa huduma za afya wa ana kwa ana. Ingawa kurekebisha mifumo yote ya elimu na afya ni lengo kuu, pia kuna njia ndogo za kushughulikia tofauti katika viwango vya elimu, kama vile kutumia picha na lugha inayoweza kufikiwa katika nyenzo za elimu kuhusu saratani.

Inaweza pia kusaidia kwa wagonjwa kushiriki hadithi zao wenyewe, kama Argate anavyofanya. Aliweza kudhibiti hofu yake kwa msaada wa familia yake pamoja na wahudumu wa mgonjwa, ambao walikuwa wakipiga simu na kumtembelea nyumbani.

Haya yote yalisaidia kuunganisha hali halisi ya kihisia, kifedha na kimatendo ya kuishi na saratani. Huko Ufilipino, wagonjwa walio na wahudumu wa kushughulikia wagonjwa wana uwezekano mdogo wa kuacha matibabu ya saratani .

Sasa, Argate anasema, ikiwa mtu mwingine aliye na saratani atamwambia kwamba hataki kwenda kwa daktari, "Nitamwambia asiogope kutafuta matibabu kwa sababu kuna mtu anatusaidia."

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi