Kwa nini 'kusitishwa kwa huduma za serikali' hutokea Marekani pekee

TH

Chanzo cha picha, EPA-EPE/Rex/Shutterstock

Serikali ya Marekani imefunga kazi mara kumi katika kipindi cha miaka 40 na zaidi. Wakati huo huo, katika nchi nyingine, serikali zinaendelea kufanya kazi, hata katikati ya vita na migogoro ya kikatiba. Kwa hivyo kwa nini jambo hili la kipekee la Marekani linaendelea kutokea?

Kwa sehemu kubwa ya dunia, kufungwa kwa huduma za serikali ni habari mbaya sana - matokeo ya mapinduzi, uvamizi au maafa. Kwamba viongozi wa mojawapo ya mataifa yenye nguvu zaidi Duniani walichochea kwa hiari mzozo ambao unasimamisha huduma za umma na kupunguza ukuaji wa uchumi ni jambo la kushangaza kwa wengi.

Katika makubaliano ya dakika za mwisho siku ya Jumamosi, bunge la Congress iliweza kuzuia kufungwa kwa huduma za serikali kwa kupitisha muswada wa matumizi ya fedha ambao utaifanya serikali kuendelea kwa siku 45 zingine. Lakini hiyo inamaanisha kuwa wanasiasa watalazimika kurudi kwenye meza ya mazungumzo, na nchi inaweza kukabiliwa na hatua ya kufungwa tena kwa serikali mara ufadhili utakapomalizika.

Kwa hivyo kwa nini hii inaendelea kutokea?

Mfumo wa serikali ya shirikisho la Amerika unaruhusu matawi tofauti ya serikali kudhibitiwa na vyama tofauti. Ulikuwa ni muundo uliobuniwa na waasisi wa taifa ili kuhimiza maelewano na mashauri, lakini hivi majuzi umekuwa na athari tofauti.

Hiyo ni kwa sababu mwaka 1980, Mwanasheria Mkuu wa Serikali chini ya utawala wa Rais Jimmy Carter alitoa tafsiri finyu ya Sheria ya Kupambana na Upungufu ya 1884. Sheria ya matumizi ya Karne ya 19 ilipiga marufuku serikali kuingia mikataba bila kibali cha bunge; kwa karibu karne moja, ikiwa kulikuwa na pengo katika bajeti, serikali ilikuwa imeruhusu matumizi ya lazima kuendelea. Lakini baada ya 1980, serikali ilichukua mtazamo mkali zaidi: endapo hakuna bajeti, basi hakuna matumizi.

Ufafanuzi huo umeiweka Marekani kando na demokrasia nyingine zisizo za wabunge, kama vile Brazili, ambapo tawi lenye mamlaka kubwa lina uwezo wa kuendelea na huduma za serikali hata pakiwepo na msukosuko wa bajeti.

Kusitishwa kwa huduma za serikali mara ya kwanza Marekani kulitokea muda mfupi baada ya mwaka wa 1981, wakati Rais Ronald Reagan alipopinga mswada wa ufadhili, na kudumu kwa siku chache. Tangu wakati huo, kumekuwa na angalau hatua kama hizo kumi ambazo zilisababisha kusimamishwa kwa huduma, na kudumu kutoka nusu-siku hadi zaidi ya mwezi. Ya mwisho, kutoka 21 Desemba 2018 hadi 25 Januari 2019, ilikuwa ndefu zaidi kwenye rekodi.

TH

Chanzo cha picha, AFP

Ndivyo ilivyotokea nchini Canada mwaka wa 2011, wakati vyama vya upinzani vilipokataa bajeti iliyopendekezwa na Waziri Mkuu wa wakati huo Stephen Harper's wa chama cha Conservative ambacho kilikuwa na wabunge wachache. Baraza la Commons kisha lilipitisha hoja ya kutokuwa na imani, na kusababisha uchaguzi. Wakati huo huo, huduma za serikali zilisitishwa.

Hata nchini Ubelgiji, ambayo haikuwa na serikali iliyochaguliwa madarakani kwa siku 589 kati ya 2010-2011, treni ziliendelea kufanya kazi.

Hivi majuzi, Ireland iliweza kufanikisha shughuli zote za huduma za umma kutoka 2016-2020 chini ya serikali ya wachache yenye mfumo wa imani na usambazaji, wakati ambapo vyama visivyo na mamlaka vinakubali kuunga mkono bili za matumizi na kura za imani.

Lakini aina hii ya ushirikiano imezidi kuwa nadra nchini Marekani, ambapo vyama vya siasa vinavyopigana vinaonekana kuwa tayari sana kutumia utendaji wa kila siku wa serikali kama njia ya kujadiliana ili kupata madai kutoka upande mwingine. Kusitishwa kwa hivi punde zaidi, kwa mfano, ni matokeo ya wachache wa wanachama wa Republican wenye msimamo mkali wa Congress wanaodai kupunguzwa kwa matumizi makubwa ambayo wafuasi wa chama chao na Democrats hawataunga mkono.

Makubaliano yalifikiwa siku ya Jumamosi, lakini kwa tahadhari kubwa: hakuna ufadhili wa ziada kwa vita vya Ukraine.

Huku muda ukiyoyoma kwenye ufadhili wa siku 45 wa kuacha pengo, inabakia kuonekana ni aina gani ya makubaliano mapya yataafikiwa - ikiwa maafikiano yatapatikana kati ya vyama hivyo.