Wanadamu ni mara mia moja 'hatari ' zaidi kuliko papa

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Binadamu ni hatari zaidi kwa wanyama wanaotuzunguka kuliko papa mkubwa mweupe

Wanadamu wanajulikana sana kama wanyama wanaowinda wanyama wengine lakini kwa mara ya kwanza wanasayansi wameweka takwimu.

Tunawinda karibu theluthi ya wanyama wote wa porini kwa chakula, dawa au kufuga kama wanyama wa nyumbani, na kuwaweka karibu nusu yao katika hatari ya kutoweka, wanasema.

Hiyo hutufanya kuwa hatari mara mia zaidi kuliko wanyama wanaowinda wanyama wengine kama vile papa mkubwa mweupe.

Na wanaonya juu ya athari kubwa kwa mfumo mzima wa ikolojia.

"Ukubwa wa kile tulichopata kinatushangaza," alisema Dk Rob Cooke wa Kituo cha Ikolojia na Hydrology cha Uingereza huko Wallingford, Oxfordshire.

"Binadamu wana matumizi mengi ya wanyama lakini tunahitaji kuelekea kwenye uhusiano endelevu wa asili ya binadamu kote ulimwenguni."

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Biashara ya usafirishaji haramu wa wanyama unaweka ndege wa porini katika hatari ya kutoweka

Watafiti walichambua data kuhusu karibu mamalia mwitu 50,000 tofauti, ndege, wanyama wanaotambaa, amfibia na samaki ambao wanadamu huvuna kwa chakula, dawa au nguo, au kukusanya kutoka porini kwa biashara ya wanyama.

Waligundua tunatumia au kufanya biashara ya spishi 14,663 - karibu theluthi moja ya wanyama wote wenye uti wa mgongo - na wanaongoza 39% ya hizi katika kuelekea kutoweka.

Na athari zetu ni kubwa mara 300 zaidi ya zile za wanyama wanaokula wenzao kama vile papa nweupe, simba au simbamarara.

Ubinadamu sasa una ushawishi mkubwa kwa wanyama wengine kwenye sayari kuliko wakati wowote ule katika historia.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uvuvi wa kupita kiasi unatishia spishi nyingi za baharini

Tunaingia kwenye ‘Anthropocene’, kipindi ambacho shughuli za binadamu zimekuwa na ushawishi mkubwa juu ya hali ya hewa na mazingira.

Wanyama wafugwao sasa wanachangia spishi nyingi za wanyama kwenye nchi kavu, na kutoa mwelekeo katika ulimwengu wa asili.

Watafiti wanaonya kuwa kuendelea kuwinda wanyama pori kupita kiasi kutakuwa na "matokeo makubwa kwa bioanuwai na utendaji kazi wa mfumo ikolojia".