Mamilioni ya watu wa umri wa makamo ni wanene kupita kiasi - utafiti

k

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Mafuta yanaweza kuzunguka kiuno kwa kadiri umri unavyosonga
  • Author, Philippa Roxby
  • Nafasi, BBC

Mamilioni ya watu wa umri wa makamo wanamini kuwa wao sio wanene, kulingana na utafiti kutoka Italia ambao uliangalia wingi wa mafuta ya mwili badala ya uzito kupitia vipimo vya kawaida vilivyozoeleka.

Kadiri umri unavyosonga, misuli hupungua na mafuta huongezeka karibu na viungo katika eneo la kiuno, mara nyingi bila uzito wa kawaida kuongezeka.

Njia ya kawaida ya kuchunguza uzito wa watu ni kwa kupima uzito wa mwili kwa kutumia kilogramu na kupima urefu kwa mita (BMI = kg/m2).

BMI ni ipimo cha kugawanya uzito wa mtu katika kilo kwa mraba wa urefu katika mita: Kg/m2 18.5-25 ni uzito wenye afya, k/m2 25-29 uzito mkubwa na kg/m2 30 na zaidi ni uzito uliopindukia.

Ni njia ya haraka na rahisi, inayoungwa mkono na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), na ni sahihi kabisa kwa watu wengi - lakini njia hiyo haitofautisha uzito wa mafuta, misuli na mifupa.

Utafiti wa watu wazima 4,800 wenye umri wa miaka 40-80, wa Chuo Kikuu cha Tor Vergata huko Roma, na kuwasilishwa katika Bunge la Ulaya juu ya uzito, uliangalia njia mbadala kwa kupima asilimia ya mafuta ya mwili.

Ni asilimia 38 tu ya wanaume na 41% ya wanawake walikuwa na uzito zaidi ya kg/m2 30 - lakini asilimia ya mafuta ya miili yao ilipopimwa, 71% na 64% walipatikana kuwa wanene.

“Tukiendelea kutumia kipimo cha WHO cha kupima unene tutawakosa watu wengi wa rika la kati na wazee ambao wako katika hatari ya kupata magonjwa yanayohusiana na mafuta ikiwemo kisukari aina ya pili, magonjwa ya moyo na saratani,” anasema mtafiti Prof. Antonino De Lorenzo.

"Kuanzisha kipmo kipya cha unene katika huduma za kimatibabu na miongozo kuhusu unene kutakuwa na manufaa kwa afya ya mamilioni ya watu," anasema Prof De Lorenzo.

Pia Unaweza Kusoma

Vifaa rahisi zaidi

Bado kuna uwezekano kwamba upimaji wa unene uliozoeleka hautaondoka kwa siku za hivi karibuni - kwani ni rahisi zaidi kuliko kupima watu mafuta ya mwili.

Watafiti wanakubali tafiti zaidi zinahitajika katika nchi nyingine ili kuthibitisha matokeo haya. Utafiti huu uliangalia tu watu wazima katika eneo moja la Italia na umeangalia tu asilimia ya mwili inayoundwa na mafuta.

Pia haikuuliza watu kuhusu milo yao au ikiwa wanafanya mazoezi – ili kuelewa kwa nini baadhi ya watu wako katika hatari zaidi kutokana na unene kuliko wengine.

"Tunahitaji vifaa rahisi vya kuchunguza unene kwa yeyote," anasema Prof Marwan El Ghoch, kutoka Chuo Kikuu cha Modena na Reggio Emilia.

Utafutaji wa chombo sahihi unaendelea.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla