Ubongo wa binadamu umekuwa ukisinyaa na hakuna anayejua ni kwanini

Na Jasmin Fox-Skelly

h

Chanzo cha picha, Getty Images/BBC

Ubongo wa wanadamu wa enzi ya sasa ni ndogo kwa karibu 13% kuliko ule wa binadamu wa enzi ya Homo sapiens (binadamu) walioishi miaka 100,000 iliyopita. Kwa nini bado inawashangaza watafiti.

Kijadi "ubongo wetu mkubwa" hufikiriwa kuwa ndio hutenganisha spishi zetu na wanyama wengine. Uwezo wetu wa mawazo na uvumbuzi ulituwezesha kuunda sanaa ya kwanza, kuvumbua magurudumu, na hata kutua kwenye Mwezi.

Kwa hakika, ubongo wetu ni mkubwa sana ukilinganishwa na wanyama wengine wa wenye ukubwa sawa na wetu. Ubongo wa mwanadamu umeongezeka karibu mara nne kwa ukubwa katika miaka milioni sita tangu spishi zetu ziliposhiriki babu mmoja na sokwe. Hata hivyo, tafiti zinaonyesha ukubwa wa ubongo umebadilika katika Homo sapiens . Katika spishi zetu, ukubwa wa wastani wa ubongo umepungua katika kipindi cha miaka 100,000 iliyopita.

Kwa mfano katika utafiti wa hivi mkaribuni mwaka 2023 , Ian Tattersall, mtaalamu wa utambuzi masalia ya binadamu walioishi miaka ya kale na michoro yao (paleoanthropologist) aliyestaafu katika Jumba la Makumbusho la Marekani la Historia ya Asili katika Jiji la New York, alifuatilia historia ya ubongo wa hominins wa kale katika nyakati mbali mbali. Alianza na aina ya kale inayojulikana, na kuishia na wanadamu wa kizazi cha kisasa.

Aligundua kwamba ukupanuka haraka kwa ubongo kulitokea katika aina tofauti za hominins, na kwa nyakati tofauti katika Asia, Ulaya na Afrika. Spishi ambazo ubongo wake ulikua baada ya muda ni pamoja na Australopithecus afarensis , Homo erectus, Homo heidelbergensis , na Homo neanderthalensis .

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ukubwa wa ubongo ulibadilika kadiri spishi mpya za wanadamu, kama vile Homo neanderthalensis zilipoibuka

Hata hivyo, mwelekeo wa kupanuka kwa ubongo baada ya muda uligeuka juu ya kichwa chake na kuwasili kwa wanadamu wa kisasa. Mafuvu ya vichwa vya wanaume na wanawake leo kwa wastani ni madogo kwa 12.7% kuliko yale ya Homo sapiens ambao waliishi nyakati zilizopita za enzi ya barafu.

"Tuna mafuvu yenye umbo la kipekee, kwa hivyo binadamu wa mapema ni rahisi sana kuwatambua - na wale wa kwanza kabisa wana akili kubwa mno," anasema Tattersall.

Utafutaji wa Tattersall unaiga ule wa wengine. Kwa mfano katika mwaka 1934, Gerhardt Von Bonin, mwanasayansi mzaliwa wa Ujerumani aliyeshirikiana na Chuo Kikuu cha Chicago huko Illinois, aliandika kwamba "kuna dalili dhahiri ya kupungua [katika ubongo wa binadamu] angalau katika Ulaya ndani ya miaka 10,000 au 20,000 iliyopita."

Kwa hivyo tunawezaje kuelezea kusinyaa huku kwa kushangaza kwa ubongo? Tattersall anasema kwamba kupungua kwa ukubwa wa ubongo kulianza karibu miaka 100,000 iliyopita, ambayo inalingana na kipindi cha muda ambacho wanadamu walihama kutoka kwa mtindo angavu zaidi wa kufikiria hadi kile anachoita "mawasiliano ya ishara" - au kufikiria zaidi ili kuelewa vizuri mazingira yako.

''Kadiri ubongo ulivyokuwa mdogo zaidi na kuwa wa mpangilio mzuri ndivyo ulivyoweza kufanya hesabu ngumu zaidi, akili kubwa za gharama kubwa za 9kimfumo hazihitajiki''.

"Huu ulikuwa wakati ambapo wanadamu walianza kutengeneza vitu vya sanaa vya mfano na nakshi zenye picha za maana ," anasema Tattersall.

Tattersall anaamini kwamba kichocheo kilichosababisha mabadiliko haya katika mtindo wa kufikiri ni uvumbuzi wa lugha moja kwa moja. Hii ilisababisha njia za neva za ubongo kupangwa upya kwa njia bora zaidi ya kimfumo.

Kwa maneno mengine, kwa vile ubongo mdogo na uliopangwa vizuri uliweza kufanya hesabu ngumu zaidi, ubongo mkubwa wa gharama kubwa za kimfumo za maumbile yake zilikua sio lazima.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwisho wa enzi ya barafu ya mwisho ulisababisha joto la juu; binadamu walikuwa na ubongo mndogo ikiwa ni njia ya kupoza mwili

"Siku hizi tukipata joto tunaweza kuvaa fulana, kuruka kwenye bwawa, au kuwasha kiyoyozi, lakini miaka 15,000 iliyopita chaguzi hizi hazikuwa zikipatikana kwetu," anasema Stibel.

"Ubongo ndio msingi mkubwa zaidi ya nishati ya viungo vyote, kwani una uzito wa karibu 2% ya uzani wa mwili wetu lakini hutumia zaidi ya 20% ya nishati yetu ya mwilini . Kwa hivyo, ikiwa ubongo ni mtumiaji mkubwa wa nishati na joto, basi unapaswa kuzoea hali ya hewa pia. Nadharia yetu ni kwamba ubongo mdogo hukupunuza joto vizuri, na unakuwa na kiwango cha kidogo cha joto kinachopungua pia.

Ugunduzi huo unaonyesha kuwa sayari ya leo inayoongezeka joto haraka inaweza kusababisha ubongo wetu kusinyaa zaidi.

Kuongezeka kwa ustaarabu tata

Labda nadharia mashuhuri zaidi iliyotolewa kuelezea ubongo wetu unavyopungua ni kwamba ilianza wakati babu zetu walipoacha kuwa wawindaji, kuweka mizizi, na kuanza kujenga jamii zilizoishi maisha magumu.

Mnamo 2021, Jeremy DeSilva, mtaalamu wa historia ya binadamu wa kale katika Chuo cha Dartmouth nchini Marekani, alichanganua visukuku vya fuvu kuanzia Miocene hominid Rudapithecus (miaka milioni 9.85 iliyopita) hadi wanadamu wa kisasa (miaka 300,000 hadi 100 iliyopita).

Alihesabu kwamba ubongo wetu uilianza kupungua miaka 3,000 tu iliyopita , karibu wakati huo huo ustaarabu tata ulianza kuibuka (ingawa tangu wakati huo amerekebisha makadirio yake , akisema kuwa kupungua kwa ukubwa wa ubongo kulitokea kati ya miaka 20,000 na 5,000 iliyopita).

Upungufu wa virutubishi unaweza kuashiria maambukizi kwenye shehemu ya ubongo

DeSilva anasema kwamba kuzaliwa kwa jamii zenye maisha tata na himaya kulimaanisha kwamba ujuzi na kazi unaweza kuenea.

Watu hawakuhitaji tena kujua kila kitu, na kama watu binafsi hawakuhitaji tena kufikiria sana ili kuishi, ukubwa wa ubongo wao ulipungua.

Lakini , nadharia hii pia inapingwa.

"Sio jamii zote za wawindaji zilizokuwa na maisha magumu kwa njia sawa na, tuseme, Wamisri walifanya kazi ngumu kwa miaka 3,000 iliyopita, lakini ukubwa wa ubongo umepungua katika jamii hizi pia," anasema Eva Jablonka, profesa aliyestaafu katika Taasisi ya Historia ya Cohn, inayohusika na Falsafa ya Sayansi na Mawazo katika Chuo Kikuu cha Tel Aviv nchini Israel.

Jablonka anahoji kwamba ikiwa hata kama ubongo ulisinyaa wakati changamano za kijamii zilipoibuka, haifuati kwamba ubongo mdogo ulikuwa jibu la mabadiliko.

"Ikiwa miaka 3,000 iliyopita jamii kubwa zaidi tata ziliibuka, hii inaweza kuwiana na tofauti kubwa zaidi katika tabaka za kijamii. Kama matokeo yake watu wengi wangekuwa maskini, basi tunajua kwamba umaskini na utapiamlo na mambo kama hayo vingedumaza ukuaji na maendeleo ya ubongo."

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuwasili kwa jamii changamano zaidi - na uvumbuzi wa lugha zilizoandikwa kama vile Sumeri - pia kunaweza kusababisha akili kupungua kwa ukubwa

Marta Lahr, kutoka Kituo cha Leverhulme cha Chuo Kikuu cha Cambridge cha Mafunzo ya Mageuzi ya Binadamu, pia amesema kwamba upungufu wa virutubishi unaweza kuelezea kongosho zetu. Mnamo 2013, alichambua mifupa na mafuvu kutoka kote Ulaya, Afrika na Asia. Aligundua kuwa Homo sapiens wenye ubongo mkubwa zaidi waliishi miaka 20,000 hadi 30,000 iliyopita, na kwamba akili za binadamu zilianza kupungua miaka 10,000 iliyopita.

Hii ni ndani ya muda ambao babu zetu wanadhaniwa waliacha kuwa wawindaji-wawindaji na kufanya kazi ya kilimo . Anasema kuwa kutegemea kilimo kunaweza kuwa kumesababisha upungufu wa vitamini na madini, na kusababisha ukuaji kudumaa.

Wakati huo huo baadhi ya wanasayansi wamesema kuwa mafuvu ya vichwa vya binadamu yamekuwa madogo kwa sababu ya kujitawala, kwa kuzingatia ukweli kwamba wanyama wanaofugwa kama mbwa na paka (ambao wanafugwa kwa urafiki wao) wana ubongo ambao ni mdogo kwa 10-15% kuliko mababu zao wa porini.

Ikiwa katika mazingira rafiki zaidi, wanadamu katika kijamii walifanikiwa katika mageuzi, basi akili inaweza kuwa imepungua kwa muda. Lakini si wote waoamini hivyo.

"Sikubaliani na nadharia hii ," anasema Jablonka.

Wakati kupungua kwa ukubwa wa ubongo kulianza ni swali ambalo haliko wazi kabisa kwa sababu rekodi sio nzuri - Ian Tattersall

"Kujitawala mwenyewe, ikiwa kulitokea, lazima kuwe kulitokea miaka 800,000 iliyopita, na hakuna ushahidi wowote kwamba ubongo wa binadamu ulipungua wakati huo."

Kwa hiyo hilo linatuacha wapi? Kwa bahati mbaya, ili kuelewa ni kwa nini ubongo ulipungua, utahitaji kubainisha hasa wakati kupungua kulianza. Lakini rekodi ya visukuku hufanya hili kuwa jambo lisilowezekana kabisa. Visukuku vya zamani ni vigumu kupata, kwa hivyo rekodi imepotoshwa sana kuelekea vielelezo vipya zaidi. Kwa baadhi ya spishi zilizohifadhiwa vibaya, kwa sasa tunategemea chache au hata fuvu moja.

"Tunachojua ni kwamba huko nyuma akili za binadamu zilikuwa na ukubwa sawa na ubongo wa Neanderthal, ambao ni mkubwa zaidi kuliko ukubwa wa wastani wa ubongo wa binadamu leo," anasema Tattersall.

"Wastani wa ubongo wote wa Homo sapiens (binadamu wa sasa) ambao wana zaidi ya miaka 20,000, pia ni wa juu. Lakini kupungua kwa ukubwa kulipoanza ni swali ambalo haliko wazi kabisa kwa sababu rekodi sio nzuri. Tunachojua ni kwamba wakati huo ubongo ulikuwa mkubwa, na sasa ni mdogo kwa 13% ."

Je, tunazidi kuwa werevu?

Unaweza pia kusoma:

Ikiwa ubongo unapungua, hii inamaanisha nini kwa akili ya mwanadamu?.Kulingana na nadharia unayoamini, ubongo mdogo unaweza kutufanya kuwa nadhifu, wapumbavu, au usiwe na athari yoyote kwenye akili.

Ni kweli kwamba ukubwa wa ubongo sio kila kitu. Ubongo wa wanaume ni karibu 11% kubwa kuliko ubongo wa wanawake kutokana na ukubwa wa miili yao.

Hata hivyo utafiti umeonyesha kuwa wanawake na wanaume wana uwezo sawa wa utambuzi. Kuna baadhi ya ushahidi unaopingwa kwamba spishi ndogo za ubongo, kama vile Homo floresiensis na Homo naledi, ziliweza kuwa na tabia mchanganyiko na kupendekeza kuwa jinsi ubongo unavyounganishwa ndicho kibainishi kikuu cha akili. Lakini kwa ujumla, kuwa na ubongo mkubwa kulingana na ukubwa wa mwili wako kunahusiana na akili.

"Ukweli kwamba ukubwa wa ubongo wetu unapungua kwa kiasi kikubwa hivi sasa inatoa hitimisho la kimantiki kwamba uwezo wetu wa akili zaidi unapungua, au angalau haukui," anasema Stibel.

"Hata hivyo, tulichofanya katika kipindi cha miaka 10,000 iliyopita ni zana na teknolojia zinazotuwezesha kupakia utambuzi kwenye vitu vya kale. Tuna uwezo wa kuhifadhi taarifa kwenye kompyuta, na kutumia mashine kukihesabu vitu. Kwa hivyo ubongo wetu unaweza kuwa na uwezo mdogo wa kiakili , lakini hiyo haimaanishi kuwa sisi kama spishi kwa pamoja tunazidi kuwa werevu."

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi