Kwa nini serikali ya Ujerumani imeamua kutoa mafunzo kwa maimamu 100 kila mwaka?

w

Chanzo cha picha, Getty Images

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani imetangaza kuwa itawasimamisha kazi taratibu maimamu walinaohubiri dini kutoka Uturuki waliokuwa wakifanya kazi katika misikiti ya nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Masuala ya Kidini ya Kiislamu ya Uturuki ambayo ilisema, "Tunafahamu hitaji la mabadiliko haya."

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani imesema kuwa, makubaliano hayo ya kuwapatia mafunzo maimamu yaliafikiwa baina ya Wizara ya masuala ya Dini na Wakfu na Jumuiya ya Masuala ya Dini ya Kiislamu nchini Uturuki baada ya mazungumzo ya muda mrefu.

Makubaliano hayo yanabainisha kuwa maimamu 100 watapatiwa mafunzo nchini Ujerumani kila mwaka, na maimamu hawa waliofunzwa katika mpango wa mafunzo ya pamoja wanakusudiwa kuchukua nafasi ya maimamu wanaotumwa Ujerumani kutoka Uturuki.

Pia, taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani imeeleza kuwa utaanzishwa ushirikiano kati ya Chuo cha Kiislamu cha Ujerumani kilichoanzishwa mwaka 2019 na Chuo Kikuu cha Osnabrück nchini Uturuki.

Maimamu hao watachukua nafasi ya wale wanaotoka Uturuki hatua kwa hatua baada ya kumaliza mafunzo yao.

DİTİB, yenye makao yake makuu mjini Cologne, Ujerumani, ni moja ya mashirika makubwa ya Kiislamu nchini Ujerumani na inasimamia takriban misikiti 900, huku maimamu zaidi ya 1,000 wakifanya kazi katika misikiti hii.

Kulingana na takwimu za Ujerumani, Waislamu milioni 5.5 wanaishi Ujerumani, idadi ambayo ni sawa na asilimia 6.6 ya jumla ya Wajerumani.

Maelezo ya video, Imam jasiri aliyeendelea na salah wakati wa tetemeko la ardhi

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani: "Tunahitaji mamlaka za kidini zinazotetea maadili yetu"

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Nancy Feaser, alisema kuwa mafunzo ya maimamu nchini Ujerumani, ambayo yatawawezesha kuchukua nafasi ya wale walioletwa kutoka Uturuki, ni "muhimu kwa ushirikiano" wa jumuiya za Kiislamu nchini Ujerumani.

Waziri Feaser alisema, "Tunahitaji viongozi wa kidini wanaozungumza lugha yetu, wanaoijua nchi yetu na kutetea maadili yetu."

Feaser pia anasema kwamba wanataka maimamu "wachangie katika mazungumzo ya dini mbalimbali na kushiriki katika majadiliano kuhusu masuala yanayohusiana na imani za jamii."

Jumuiya ya Waislamu DİTİB, ilisema kuwa mabadiliko haya ni muhimu

g

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Imam

Mpango huu tayari umewekwa pamoja na Erdoğan na kiongozi wa Ujerumani

Suala la maimamu waliotumwa waliopelekwa Ujerumani kutoka Uturuki limekuwa likizua mvutano kati ya Berlin na Ankara, kutokana na propaganda za kisiasa na shutuma za ujasusi kati ya nchi hizo mbili.

Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Waislamu ya DİTİB ilisema kwamba ni muhimu kuzingatiwa kwa matakwa ya pande zote.

Taarifa hiyo pia ilisema kwamba DİTİB "inafahamu hitaji la mabadiliko, ambalo limekuwa lengo la mijadala mikali ya kijamii kuhusu sera ya ujuzi wa lugha na ushirikiano wa kijamii wa maimamu katika muongo mmoja uliopita."

Shirika hilo pia lilisisitiza kuwa ni muhimu kuwa na ufadhili wa mara kwa mara kila mwaka ili kuwafunza maimamu 100 watakaofanya kazi misikitini.

Shirika hilo pia lilipendekeza kwamba maimamu wafungwe na masharti kama vile kuwa na shahada ya kwanza kutoka kwa Jumuiya katika masuala ya Kiislamu kama vile teolojia.

Taarifa zaidi kuhusu jinsi ushirikiano huo utakavyotekelezwa zitatangazwa na pande zote mbili mapema mwaka ujao, shirika hilo lilisema.

Mpango huu tayari umewekwa pamoja na Erdoğan na kiongozi wa Ujerumani

w

Chanzo cha picha, reuters

Maelezo ya picha, Viongozi wa Uturuki na Ujerumani

Mafunzo hayo kwa maimamu wa Ujerumani tayari yamekubaliwa na marais wa nchi mbili baada ya kiongozi Uturuki nchini Ujeremani na Recep Tayyip Erdoğan kuizuru Berlin mwezi Novemba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ujerumani kwa vyombo vya habari, kiongozi wa Ujerumani Olaf Scholz na rais Recep Tayyip Erdoğan walikubaliana kuharakisha mafunzo ya maimamu nchini Ujerumani na kusitisha taratibu mpango wa kuwapeleka huko maimamu kutoka Uturuki.

Katika hotuba yake kwa bunge la Ujerimani (Bundestag) mwaka 2018, Kansela wa zamani wa Ujerumani, Angela Merkel, alisisitiza haja ya mafunzo ya imamu nchini Ujerumani, na kusema, "Hii inatufanya kuwa nchi huru, na ni muhimu kwa ajili ya siku zijazo."

Maelezo ya video, Paka akimrukia Imam wakati wa Sala nchini Algeria