Kuna tofauti gani kati ya chuki dhidi ya Wayahudi na chuki ya Uzayuni?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Huku mzozo kati ya Israel na Gaza ukiendelea, baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii wanajaribu kuelewa tofauti kati ya chuki dhidi ya Wayahudi na chuki ya Uzayuni.

Je, maneno haya yanamaanisha nini?

Kupinga Uyahudi maana yake ni chuki dhidi ya watu wa Kiyahudi, na chuki hii ya Uyahudi imekuwepo kwa karne nyingi.

Kuupinga Uzayuni kwa ujumla kunaweza kufafanuliwa kama upinzani dhidi ya uwepo wa Jimbo la Israeli.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mapigano kati ya Wapalestina na polisi wa Israeli mbele ya Dome of the Rock mnamo 2021

Kupinga Uyahudi ni nini?

Wayahudi wamekabiliwa na ubaguzi, uadui, na mateso kwa karne nyingi.

Wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, Wayahudi milioni sita waliuawa na Wanazi au washirika wao, katika kile kinachojulikana kama mauaji ya Holocaust.

Katika nyakati za kisasa, chuki dhidi ya Wayahudi inaweza kuchukua njia nyingi, ikiwa ni pamoja na nadharia za njama kuhusu udhibiti wa Wayahudi wa mfumo wa kimataifa wa kifedha na vyombo vya habari, mashambulizi dhidi ya masinagogi, maneno ya matusi au matamshi ya chuki, na picha za kuudhi na emoji kwenye mitandao ya kijamii.

Wakati mwingine watu wenye mitazamo tofauti kuhusu Israeli hawakubaliani kuhusu iwapo maoni au maoni fulani yanapingana na Wayahudi au la.

Mara nyingi, majadiliano yanajumuisha Israeli na neno "Uzayuni’’

w

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chama cha Nazi cha Ujerumani kiliua mamilioni ya Wayahudi na wengine, na mauaji ya Holocaust yalitokea wakati wa Vita ya pili vya dunia

Uzayuni ni nini?

Uzayuni ulianza kama vuguvugu la kisiasa barani Ulaya mwishoni mwa karne ya 19. Vuguvugu hilo lilitaka kuanzisha taifa la Kiyahudi katika ardhi inayojulikana kama Palestina - ambayo pia inajulikana kwa Wayahudi kama Ardhi ya zamani ya Israeli.

Mnamo 1947, Umoja wa Mataifa ulipendekeza kugawanywa kwa Palestina katika mataifa ya Kiyahudi na Kiarabu, na mnamo 1948 Jimbo la Israeli lilitangazwa rasmi kuanzishwa .

Hata hivyo, wakazi wengi wa Waarabu wanaoishi Palestina na maeneo jirani walipinga kuanzishwa kwa Taifa la Israel; Wanachukulia suala hili kama kuwanyima haki Waarabu.

Siku hizi, watu hao wanaohesabiwa kuwa ni sehemu ya vuguvugu la Kizayuni wanaamini katika umuhimu wa kulinda na kuendeleza Taifa la Israel kama taifa la Kiyahudi.

Kuna tofauti ndani ya vuguvugu la Wazayuni - kwa mfano, baadhi ya Wazayuni wanaamini kuwa Israel ina haki ya baadhi ya maeneo nje ya ardhi yake. Wazayuni wengine wanapinga imani hii.

Wayahudi wengi wanaunga mkono kanuni za msingi za Uzayuni zinazohusiana na ulazima wa dola ya Kiyahudi katika eneo ambalo sasa linajulikana kama Israeli. Kuna wachache wanaopinga Uzayuni kwa sababu za kidini au kisiasa.

Watu wasio Wayahudi pia wanaweza kuwa Wazayuni.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jimbo la Israeli lilianzishwa mnamo 1948

Kupinga Uzayuni ni nini?

Kupinga Uzayuni kwa ujumla kunaweza kufafanuliwa kama upinzani dhidi ya uwepo wa Jimbo la Israeli.

Wapo Wazayuni wanaokosoa sera za serikali ya Israel, kama vile kukalia kwa mabavu Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, ujenzi wa vitongoji vya walowezi na njia ya ukuta wa utengano (uliojengwa na Israel ndani na nje ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kusema ni njia ya usalama dhidi ya washambuliaji wa Kipalestina, ingawa wafuasi wa Palestina wanaona ukuta huu kama chombo cha kunyakua ardhi).

Katika baadhi ya matukio, watu wanapoikosoa sana Israeli, ni vigumu kujua kama ukosoaji huo unachochewa na chuki dhidi ya Wayahudi au la.

Hii imesababisha shutuma kwamba chuki dhidi ya Uzayuni - kukataliwa kwa dola ya Kiyahudi - ni aina ya kisasa ya chuki dhidi ya Uyahudi.

Muungano wa Kimataifa wa Kukumbuka mauaji ya Holocaust unasema baadhi ya tuhuma na shutuma dhidi ya Israel zinajumuisha chuki dhidi ya Wayahudi.

Wale wanaokataa wazo hili wanasema kwamba hoja hii inatumiwa kama chombo na wafuasi wa Israeli kunyamazisha ukosoaji dhidi ya Israeli, kwa kuonyesha ukosoaji kama huo kama ubaguzi wa rangi.

Wengine wanasema neno "Mzayuni" linaweza kutumika kama shambulio la siri kwa Wayahudi, wakati wengine wanasema serikali ya Israel na wafuasi wake kwa makusudi wanachanganya chuki dhidi ya Uzayuni na chuki dhidi ya Wayahudi ili kuepusha ukosoa

Maelezo ya video, Wayahudi wanaovalia kama Waislamu ili kuepukaa marufuku ya maombi