'Nilijihisi kama chambo katika mzozo wa Iran na nchi za magharibi'

Kamran Ghaderi (kulia), na Massud Mossaheb (kushoto) wakisalimiana nana Waziri wa mambo ya nje wa Austria Alexander Schallenberg, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Vienna mnamo Juni 3

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kamran Ghaderi (kulia), na Massud Mossaheb (kushoto) waliachiwa huru mapema mwezi Juni baada ya mazungumzo na serikali ya Austria
  • Author, Parham Ghobadi
  • Nafasi, BBC Persian

Kamran Ghaderi, Mustria mzaliwa wa Iran ambaye alizuiliwa kwa miaka sana na nusu katika jela hatari la Evin nchini Iran, alizungumza na BBC kuhusu masaibu yake siku ya kubadilishana wafungwa ambayo ilishuhudia Wairan watano wa Marekani wakiachiwa huru na Tehran.

"Hujihisi kama mwanadamu. Wanachukua ubinadamu kutoka kwako," Ghaderi, 60, aliongeza.

Ghaderi, Muaustria mwezake mzaliwa wa Iran Massud Mossaheb, 77, na vlogger wa Usafiri wa Denmark Thomas Kjems, 28, waliachiliwa wiki moja baada ya Ubelgiji na Iran kutekeleza mabadilishano ya wafungwa. Mabadilishano ya awali yalihusisha mfanyakazi wa misaada wa Ubelgiji Olivier Vandecasteele na mwanadiplomasia wa Iran Assadollah Assadi.

Awali Ghaderi alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa tuhuma za "kushirikiana na taifa lenye uadui", "nchi yenye uadui" ikiwa ni Ujerumani, kwa mujibu wa mamlaka ya Iran.

Assadi alikuwa amefungwa jela miaka 20 na mahakama nchini Ubelgiji, ambayo ilimpata na hatia ya kupanga shambulio la bomu kwenye mkutano wa hadhara wa kundi la upinzani la Iran lililokuwa uhamishoni nchini Ufaransa. Iran ilisisitiza kukamatwa kwake, kufunguliwa mashtaka na kuhukumiwa kulikiuka sheria za kimataifa.

'Utekaji nyara ni biashara yenye faida kwa Iran'

Massud Mossaheb alidai kuwa Iran ina maslahi ya kiuchumi nyuma ya kukamatwa kwa raia wa kigeni na Wairan wenye uraia pacha.

Maoni yake yaligusia habari kwamba ubadilishaji wa wafungwa wa Washington-Tehran, uliopatanishwa na Qatar, uliipa taifa la Mashariki ya Kati fursa ya kupata $6bn (£4.8bn) ya fedha za Iran zilizokuwa zikishikiliwa Korea Kusini.

Thoams Kjems
Maelezo ya picha, Mwandishi wa habari wa Denmark Thomas Kjems alikamatwa Septemba 2022 alipokuwa akisafiri nchini Iran

"Utekaji nyara ni biashara yenye faida kwa Iran," Mossaheb aliiambia BBC

"Wao [mamlaka ya Iran] huweka bei kwenye kichwa cha kila mtu," alisema.

"Iran inazinyang'anya fedha kutoka nchi za Magharibi na wataendelea kufanya hivyo isipokuwa mamlaka makubwa yatawazuia."

'Mwamuzi wa kifo'

Alikamatwa mwaka wa 2018 wakati wa safari ya kikazi nchini Iran, Mossaheb pia alishtakiwa kwa "kushirikiana na nchi yenye uadui". Awali alipokea kifungo cha miaka kumi iliyotolewa na jaji wa Iran Abolghassem Salavati, ambaye mashirika ya kutetea haki za binadamu yamemwita "Jaji wa Kifo". Adhabu hiyo baadaye ilipunguzwa hadi miaka minane.

Hapo awali Salavati amekuwa akilengwa na Umoja wa Ulaya na Marekani, ambazo zilimshutumu kwa "kukosa haki katika kesi za maonyesho".

Mossaheb alizuiliwa kwa miaka minne na nusu katika jela la Evin.

Kamra Ghaderi alisema kuwa, katika juhudi za kutaka kuachiliwa huru, alianza kuwasiliana na wabunge na maafisa wa Iran. Kisha akadai kuwa alitembelewa na maafisa wa ujasusi wa Iran.

"Waliniambia kuwa Austria ilijua kuhusu madai ya kuachiliwa kwangu, lakini matakwa ya serikali yangepaswa kutekelezwa ili niachiliwe."

"Waliniambia kwamba 'tunaweza kufunga miaka 10 zaidi'."

Ghaderi alisema amefurahi kuachiliwa na kuwa na familia yake. Lakini kama Mossaheb, alikuwa na wasiwasi kwamba uhuru wake ungeweza kuhimiza utawala wa Iran kuwafunga raia wa kigeni zaidi au wenye uraia pacha.