Yafahamu majiji mazuri zaidi ya kuishi duniani kwa mwaka 2023

City

Chanzo cha picha, Getty Images

Baada ya kupungua kwa janga la Corona, ubora wa maisha unaongezeka tena katika miji mingi duniani. Kwa kweli, uwezo wa kuishi kwa ujumla umefikia kiwango cha juu zaidi katika miaka 15, kwa mujibu wa Kielelezo cha kila mwaka cha annual Global Liveability Index, ambacho kinafuatilia na kupanga kwa ubora miji ama majiji 173 wakifuata vigezo kadhaa vikiwemo vya uthabiti, huduma za afya, utamaduni na mazingira, elimu na miundombinu.

Ongezeko hilo linakuja kwa kiasi kikubwa kutokana na mafanikio ya huduma za afya na elimu kote Asia, Mashariki ya Kati na Afrika - licha ya viwango vya utulivu kupungua kwa ujumla kutokana na machafuko ya kiraia huku kukiwa na ongezeko la wasiwasi wa gharama za maisha duniani kote na kuendelea kwa migogoro katika miji kama Kiev.

Kuondolewa kwa vizuizi vya janga la Corona duniani pia kumeboresha viwango vya kitamaduni na mazingira kwani matukio na vivutio vingi vimerudi kwa kishindo.

Ingawa Global Liveability Index inaweza kuweka data kuhusu kile kinachofanya mahali paweze kutajwa kuwa bora kwa kuishi, ila ni watu ambao wanaoishi siku baada ya siku katika miji hiyo, ambao wanaweza kuzungumza vyema zaidi kuhusu kuishi katika miji hiyo kukoje.

Tulizungumza na wakazi katika miji michache kati ya miji ama majiji 10 bora yaliyoorodheshwa ili kujua sababu zao zilizowafanya miji wanyoishi waiite nyumbani.

City

Chanzo cha picha, Getty Images

Vienna, Austria

Mji mkuu wa Austria, Vienna sio mgeni kwenye kushika namba moja katika orodha ya kila mwaka ya majiji bora ya kuishi kwa mujibu wa Annual Global Liveability Index. Ukikosa nafasi hiyo kwa muda mfupi mwaka 2021 wakati janga la Corona lilipoathiri makumbusho na migahawa yake yenye kuvutia. Ikiwa na vigezo vya ubora vilivyokamilika kama uthabiti, huduma za afya, elimu na miundombinu, Vienna ni zaidi ya unachokisikia na kukiona, kulingana na wakaazi wake.

"Kimsingi una mzunguko uliokamilika wa maisha katika sehemu hii moja," alieleza Manuela Filippou, meneja wa mgahawa wa Michelin na baa ya divai ya asili, Konstantin Filippou (vyote anaendesha na mume wake ambaye ni mpishi asiyejulikana).

Kwa historia yake iliyohifadhiwa, mfumo wa usafiri wa umma wa uhakika, huduma za utunzaji wa watoto za bei nafuu na urahisi wa kuifikia migahawa, majumba ya sinema na hata viwanda vya divai ndani ya mipaka ya jiji, Vienna inaweza kukuwa mahali pa kukaa milele, alisema.

"Wakati mwingine, tunapofanya kazi kupita kiasi na kutoweza kwenda popote kwa muda mrefu, hatuwezi kugundua hilo kwa sababu tunaweza kupata kila kitu hapa," Filippou aliongeza.

Kwa mkazi Richard Voss, meneja mauzo na masoko katika hoteli ya Das Tigra, maisha ya jiji yanaimarishwa tu na historia tajiri ya kitamaduni na shughuli zinazopatikana hapa.

"Vienna ina aina mbalimbali za majengo ya kihistoria ya kuvutia, ikiwa ni pamoja na Schönbrunn Palace, Hofburg na Vienna City Hall," alisema. "Jiji hili pia linajulikana kwa utamaduni wake wa muziki, na watunzi maarufu kama vile Mozart, Beethoven na Strauss wameishi na kufanya kazi hapa." Anasema wakazi wanaweza kupata kwa urahisi mila hizo za kitamaduni kupitia makumbusho mengi ya jiji, sinema na nyumba za opera.

Anapendekeza pia kuchunguza historia ya upishi ya Vienna, kuchukua sampuli za vyakula vya kitamaduni kama vile wiener schnitzel na sachertorte, na kutembelea masoko mbalimbali, kama vile Naschmarkt, ili kufurahia vyakula vibichi na utaalam wa ndani.

Vienna

Chanzo cha picha, Getty Images

Melbourne, Australia

Miji ya Melbourne na Sydney, Australia ilitetea tena nafasi zao kwenye viwango vya ubira (ya tatu na ya nne mtawalia) katika 10 bora ya mjiji mazuri ya kuishi dunia, baada ya kushuka kwenye orodha hiyo wakati wa janga la Corona ambalo lilisababisha mfumo wa afya Australia kufungwa kwa muda mrefu. Melbourne haswa ilikuwa na alama za juu zaidi kwenye eneo la utamaduni na mazingira nchini humo- sifa ambazo huzungwa vyema na wakaazi.

"Melbourne ina eneo la ajabu la chakula, sanaa za kitamaduni, matukio na vivutio, na vile vile michezo na matukio yote makubwa ya kimataifa kama vile Australian Formula 1 Grand Prix na Australian Open," alisema Jane Morrell, mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Career Solutions. Anasema pia katika jiji hilo ni rahisi kusafiri, kwa usafiri bora unaokufikisha mpaka kwenye vitongoji. Pia ni mwendo mfupi tu kufika kwenye fukwe maarufu duniani na maeneo ya mvinyo.

Kwa mwanahabari Kimmie Conner, mwenye asili ya California, akilinganisha na mijiji mengine anasema: "Maeneo kama Sydney ni mazuri , yana muonekano wa kuvutia, ukanda wa pwani tulivu na majengo mashuhuri. Lakini Melbourne si jiji la alama, ni jiji la kitamaduni; na kugundua hilo kunahitaji kuingia ndani zaidi," alisema Conner, ambaye anaandikia jarida la Adventures & Sunsets na sasa amechagua kuishi katika jiji kuliko nyingine yoyote.

"Ili kugundua uzuri wa Melbourne, ni lazima upite kwenye vimgahawa vidogo ukiwa njiani upate kahawa bora maishani mwako. Inabidi ujaribu menyu za kuonja kwenye migahawa maalum karibu na jiji na ugundue maeneo bora yaliyojificha."

Melbourne

Chanzo cha picha, Getty Images

Vancouver, Canada

Miji mitatu ya Canada (ikiwa ni pamoja na Calgary na Toronto) imeingia katika 10 bora mwaka huu, lakini Vancouver iliorodheshwa ya juu zaidi (nafasi ya tano) kwa alama zake bora za tamaduni na mazingira - sifa ambazo wakaazi wanaonyesha zinawavutia kulipenda jiji lao.

"Vancouver ni rahisi kkwenda kwenye misitu, baharini na angani," alisema Tony Ho, mkazi na mmiliki wa biashara ndogo. "Mfumo wetu wa usafiri wa umma unakuruhusu kutoka kwenye Ghuba nzuri ya Kiingereza hadi maeneo ya milimani ya Grouse Mountain kwa siku moja na kwa kutumia basi, baiskeli, treni na mashua."

Pia anapenda vyakula mbalimbali vya jiji - kielelezo cha urembo wa kitamaduni wa Vancouver - ambapo unaweza kupata kila kitu kuanzia Injera ya Ethiopia hadi momos ya Tibentan. "Upana wa tamaduni za chakula kutoka jamii mbalimbali na wanavyoshiriki umekuwa ukikuwa kila wakati."

Kama mzazi, anasema anathamini pia kutembelea mbuga na fukwe nyingi - zote unaweza kuzifikia chini ya dakika 20 kutoka katikati mwa jiji. "Ni kitu ambacho nataka mtoto wangu apate kwa maisha yake yote," alisema Ho.

Vancouver

Chanzo cha picha, Getty Images

Osaka, Japan

Osaka imeorodheshwa katika 10 bora, na Japan nchi pekee ya Asia iliyoingia kwenye orodha hiyo. Osaka ilipata alama 100 bora katika matokeo yake kwenye maeneo ya uthabiti, afya na elimu. Gharama za maisha zinapoendelea kupunguza mapato mengi ya kaya duniani kote, uwezo wa kumudu maisha kwa Osaka imekuwa faida kubwa kwa wakazi.

"Gharama za kukodisha nyumba huko Osaka sio ghali ikilinganishwa na miji mikuu mingine nchini Japani na duniani," alisema mkazi Shirley Zhang, ambaye asili yake ni Vancouver. "Kodi yangu ni takriban £410 kila mwezi pamoja na bili za maji, mtandao na matengenezo. Ingawa nyumba ni ndogo, ila ni mpya na safi. Ikiwa ungekodisha mahali kama Vancouver, ingegharimu si chini ya £705."

Kula nje kwenye migahawa kwa bei nafuu pia ni jambo muhimu kwa wenyeji. "Tofauti na ninakotoka Uingereza, ambapo kula kwenye Migahaw akunaweza kukufilisi, Osaka ina migahawa yenye ubora wa juu na kwa bei nzuri za bajeti," alisema mkazi James Hills. "Unaweza kumudu kula chakula kizuri kilichopikwa na kitamu kwenye migahawa kila siku."

Osaka

Chanzo cha picha, Getty Images

Auckland, New Zealand

Ikiwa imefungana kwenye nafasi ya 10 na Osaka, Auckland ilipanda zaidi ya nafasi 25 kutoka nafasi ya 35 mwaka jana. Ilikuwa chini hivi kutokana na kuchelewa kufunguliwa tena kwa maeneo mengi kwa sababu ya Corona, ambapo vizuizi na maagizo havikuondolewa kikamilifu na vyote mpaka ilipofikia Septemba 2022.

Kando na kufanya vyema kwenye elimu, jiji hilo pia lilipata alama za juu zaidi kwenye utamaduni na mazingira kati ya miji 10 bora, vitu ambavyo wakaazi waliunga mkono katika uzoefu wao wa kuishi hapa.

"Ufukwe mzuri uliojitenga pengine upo ndani ya mwendo wa gari wa dakika 20 kutoka katika maeneo wanaoishi watu wengi Auckland, kama si karibu kabisa," alisema mkazi Megan Lawrence, ambaye anaandikia mtandao wa My Moments and Memories.

"Tuna uwanja mzuri wa michezo wa majini ulio karibu kabisa, wenye njia nyingi za kuufurahia. Vile vile, jiji hilo limezungukwa na vichaka vya asili vya kupendeza, ambapo ni rahisi kkwenda huko na kuhisi kama hauko mjini."