Ugunduzi wa Pliosaur: Mnyama mkubwa wa baharini aibuka kutoka kwenye miamba ya Dorset

TH

Chanzo cha picha, BBC/TONY JOLLIFFE

Na Jonathan Amos na Alison Francis

BBC News, Sayansi

Fuvu la mnyama mkubwa sana wa baharini limetolewa kutoka kwenye miamba ya Pwani ya Jurassic ya Dorset.

Ni mabaki ya pliosaur, kiumbe wa baharini ambaye alitisha bahari karibu miaka milioni 150 iliyopita.

Mabaki hayo ya urefu wa 2m ni mojawapo ya vielelezo kamili zaidi vya aina yake kuwahi kugunduliwa na inatoa maarifa mapya kuhusu mwindaji huyu wa kale.

Fuvu hilo litaangaziwa katika kipindi maalum cha David Attenborough kwenye BBC One Siku ya Mwaka Mpya.

th

Chanzo cha picha, BBC STUDIOS

"Oh wow!"

Kuna mishangao huku karatasi inayofunika mabaki ya mnyama huyo ikivutwa nyuma na fuvu la kichwa kufichuliwa kwa mara ya kwanza.

Mara moja ni dhahiri kwamba pliosaur hii ni kubwa na imehifadhiwa kwa njia nzuri

Hakuna kielelezo popote pengine kinacholingana nacho, anaamini mtaalamu wa elimu ya historia Steve Etches.

"Ni mojawapo ya mabaki ya mnyama wa kale kuhifadhiwa kwa njia bora zaidi ambayo nimewahi kufanyia kazi. Kinachoifanya kuwa ya kipekee ni kamili," aliambia BBC News.

"Taya ya chini na fuvu la juu vimeunganishwa pamoja, kama ingekuwa hai. Ulimwenguni kote, hakuna vielelezo vyovyote vilivyopatikana kwa kiwango hicho cha undani. Na ikiwa ndivyo, sehemu nyingi hazipo, ingawa hii, imepotoshwa kidogo - ina kila mfupa uliopo.

th

Chanzo cha picha, BBC STUDIOS

Maelezo ya picha, Steve Etches anaonyesha Sir David Attenborough pua - kipande cha kwanza kupatikana

Fuvu la kichwa ni refu kuliko wanadamu wengi, ambayo hukupa hisia ya jinsi kiumbe huyo anapaswa kuwa kwa ujumla.

Huwezi kujizuia kuzingatia meno yake 130, haswa yale ya mbele.

Ni marefu na wenye makali kama wembe ,yangeweza kuua kwa kuuma mara moja. Lakini ukiangalia karibu kidogo - ikiwa unathubutu - na nyuma ya kila jino ni alama ya matuta mazuri. Haya yalimsaidia mnyama huyo kutoboa nyama na kisha kung’oa meno yake kama kisu upesi, tayari kwa shambulio la haraka la pili.

TH

Chanzo cha picha, BBC/TONY JOLLIFFE

Pliosaur ilikuwa mashine kuu ya kuua na yenye urefu wa 10-12m, ikiwa na miguu minne yenye nguvu kama nzige ili kujiendesha kwa mwendo wa kasi, ilikuwa ni mwindaji wa juu kabisa baharini.

"Mnyama huyo alikuwa mkubwa sana hivi kwamba nadhani angeweza kuwinda ipasavyo kitu chochote ambacho kilikuwa cha bahati mbaya kuwa katika nafasi yake," anasema Dk Andre Rowe kutoka Chuo Kikuu cha Bristol.

"Sina shaka kwamba hii ilikuwa kama T. rex chini ya maji ."

Milo yake ilijumuisha wanyama watambaao wengine kama vile binamu yake mwenye shingo ndefu, plesiosaur, na pomboo-kama ichthyosaur - na ushahidi wa mabaki yake unaonyesha kwamba alikula pliosaurs wengine wanaopita.

Jinsi fuvu hili la mabaki yake lilivyopatikana ni la ajabu.

Ilianza kwa kupata nafasi wakati wa matembezi kando ya ufuo karibu na Ghuba ya Kimmeridge kwenye Pwani maarufu ya Urithi wa Dunia wa Jurassic kusini mwa Uingereza.

Rafiki ya Steve Etches na mpenda mabakoi ya viumbe wa kale mwenzake Phil Jacobs alikutana na ncha ya pua ya pliosaur iliyolala kwenye ardhi. Ikiwa nzito sana kubeba, alikwenda kumchukua Steve na wenzi hao wakatengeneza machela ili kupeleka kipande hicho cha mabaki mahali salama.

TH

Chanzo cha picha, STUDIO ZA BBC

Lakini sehemu nyingine ya mnyama huyo ilikuwa wapi? Uchunguzi wa ndege zisizo na rubani wa uso wa mwamba mrefu ulibainisha mahali panapowezekana. Shida ilikuwa njia pekee ya kuichimba ilikuwa kuruka kutoka juu.

Kuondoa mabaki hayo kutoka kwa mwamba daima ni kazi yenye uchungu na na mvuto wake, Lakini kufanya hivyo huku ukining'inia kwenye kamba kutoka kwenye mwamba unaoporomoka, mita 15 juu ya ufuo, kunahitaji utaratibu mwingine wa ujuzi.

Ujasiri, kujitolea, na miezi iliyotumiwa kusafisha fuvu, hakika imekuwa na thamani yake. Wanasayansi kutoka kote ulimwenguni watakuwa wakipiga kelele kutembelea mabaki ya Dorset ili kupata maarifa mapya kuhusu jinsi viumbe hawa wa ajabu walivyoishi na kutawala mfumo wao wa ikolojia.

Mtaalamu wa elimu ya viumbe Prof Emily Rayfield tayari amechunguza matundu makubwa ya duara yaliyo nyuma ya kichwa. Yanamwambia juu ya saizi ya misuli inayoendesha taya za pliosaur, na nguvu zilizojitokeza kama mdomo wake ulifunga na kuponda mawindo yake.

Katika sehemu ya juu ya mwisho , hii inatoka kwa karibu newtons 33,000. Kwa muktadha, taya zenye nguvu zaidi katika wanyama walio hai zinapatikana kwenye mamba wa maji ya chumvi, kwa toni 16,000.

"Ikiwa unaweza kuiga kuumwa kwa nguvu sana, unaweza kulemaza mawindo yako; kuna uwezekano mdogo wa kunusurika. Kuumwa kwa nguvu kunamaanisha kuwa unaweza pia kuchubua tishu na mfupa kwa ufanisi kabisa," mtafiti wa Bristol alielezea.

"Kuhusu mbinu za kula: mamba hufunga taya zao karibu na kitu na kisha kukunja, ili labda kupotosha kiungo kutoka kwa mawindo yao. Hii ni tabia ya wanyama ambao wamepanua vichwa nyuma, na tunaona hii katika pliosaur."

TH

Chanzo cha picha, BBC/TONY JOLLIFFE

Kielelezo hiki kipya kilichogunduliwa kina vipengele vinavyopendekeza kilikuwa na uwezo mkubwa wa kihisia na muhimu sana.

Pua yake ina mashimo madogo ambayo huenda yalikuwa mahali pa tezi ili kuisaidia kutambua mabadiliko katika msukumo ama presha ya maji yanayofanywa na wanyama waliolengwa naye kama mlo. Na juu ya kichwa chake kuna shimo ambalo lingekuwa na parietali, au jicho la tatu. Mijusi, vyura na baadhi ya samaki walio hai leo wana mojawapo ya haya. Haihisi mwangaza na huenda ilisaidia katika kuwatafuta wanyama wengine, hasa wakati pliosaur ilipokuwa ikitoka kwenye kina kirefu, chenye giza totoro.

Steve Etches ataweka fuvu hilo kwenye maonyesho mwaka ujao kwenye jumba lake la makumbusho huko Kimmeridge - the Etches Collection.

th

Chanzo cha picha, BBC/TONY JOLLIFFE

"Nina uhakika kwamba sehemu ya mnyama huyu iliyosalia iki hapo" anaambia BBC News.

"Na kwa kweli unapaswa kujitokeza sababu iko katika mazingira ya kumomonyoka kwa kasi sana. Sehemu hii ya mstari wa mwamba inaporomoka kwa futi moja kila mwaka . Na haitachukua muda mrefu kabla ya pliosaur wengine kupotea. Ni fursa ya mara moja katika maisha."

Ripoti ya ziada ya Rebecca Morelle na Tony Jolliffe

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah