Jinsi majaji wa Kenya walivyosimama kidete dhidi ya Rais William Ruto

Kufuatia wiki kadhaa za mabishano makali ya wiki kadhaa kati ya Rais William Ruto na majaji wa Kenya, mahakama mbili tofauti zimetoa uamuzi dhidi ya serikali, zote mbili kuhusu masuala muhimu yaliopo katika moyo wa rais.

Kwanza, siku ya Ijumaa mahakama iliamuru serikali kuacha kuchukua malipo ya ushuru mpya wa nyumba na saa moja au zaidi baadaye, mahakama nyingine tofauti ilisema rais hawezi kutuma maafisa 1,000 wa polisi nchini Haiti, kama Bw Ruto alivyoihaidi UN.

Wachambuzi wanaona kama hii ni ishara kuwa majaji wa Kenya kuwa wapo huru licha ya kile wanachokiona kuwa ni majaribio ya rais ya kuwatisha.

Hivi majuzi Bw Ruto ameanzisha msururu wa mashambulizi dhidi ya idara ya mahakama akiwashutumu majaji ambao hawakutajwa kwa ufisadi huku akikashifu walioenda mahakamani kusimamisha miradi ya serikali.

Alikuwa akijibu mlolongo wa awali wa maamuzi dhidi ya utawala wake, mmoja wao ulibatilishwa wiki iliyopita.

Kabla ya uamuzi wa Ijumaa, wakili ambaye alikuwa katika timu iliyounda katiba ya sasa aliiambia BBC kuwa Wakenya, kwa kuzingatia ukosoaji unaoendelea wa mahakama, "watakuwa na hamu ya kuona kama sasa, tutaona maamuzi ambayo yanaunga mkono upande wa kwa serikali".

Bobby Mkangi alisema kauli dhidi ya majaji hao "imeundwa ili kufikia hatua ambapo mahakama itaegemea uzito wa mtendaji".

Lakini hili linaonekana kuwa bado halijatokea.

Rais wa Chama cha Wanasheria nchini Kenya Eric Theuri aliiambia BBC kuwa baada ya uamuzi huo kuhusu ushuru wa nyumba kwamba ingawa ukosoaji huo ulikuwa "kwa njia ya kutisha mahakama", matokeo ya kesi hiyo "hayakuwa ya kushangaza" kwani serikali ilikuwa imewasilisha " kesi dhaifu sana".

“Tulitarajia na tulikuwa na matumaini kwamba mahakama ingeweza kuangalia sheria na kutoa uamuzi kwa misingi ya sheria na si kitu kingine chochote,” alisema.

Katika wiki za hivi majuzi, mashambulizi ya rais dhidi ya majaji yalizua taharuki kutoka kwa raia wa Kenya, wakiwemo wanasiasa na mashirika ya kiraia.

Bw Mkangi alisema "mashambulizi yanayotolewa na rais yamesababisha "shinikizo" dhidi ya majaji, akiongeza kwamba bado hatua hiyo itazingatiwa na kutoa maamuzi yanayoegemea upande wa serikali.

Alisema "mahakama kweli ilihisi shinikizo na ilihisi kuamriwa na shinikizo hilo" la kuomba mkutano ambao haujawahi kufanywa unaohusishwa na kesi za moja kwa moja za mahakamani kati ya jaji mkuu na rais.

Lakini alitilia shaka "falsafa ya uongozi" ya Jaji Mkuu Martha Koome, ambaye aliomba mkutano huo, akiongeza kuwa hilo litazua shaka.

Mkutano huo wa Jumatatu umezuwa mjadala mkali wa kitaifa, huku kukiwa na dhana kwamba mahakama ilikuwa inashindwa dhidi ya rais.

Jaji Mkuu Koome mwenyewe alikuwa ameonya kwamba "vitisho na matamko" dhidi ya mahakama yalikuwa "makubwa sana".

Alisema ni "shambulio dhidi ya katiba, utawala wa sheria na utulivu wa taifa na inaweza kusababisha machafuko katika nchi mama".

Lakini ombi lake la kukutana na rais na mahudhurio yake ya baadaye lilizua maswali.

Bw Theuri, rais wa LSK, aliiambia BBC kuwa matokeo ya mkutano huo yalionekana kana kwamba mahakama ilienda “kuombaomba”kwa rais... na hatimaye kuonyesha hali ya kudhoofisha uhuru wa mahakama."

Ekuru Aukot, kiongozi wa chama cha upinzani cha Third Way Alliance, aliiambia kituo cha runinga moja ya eneo hilo kwamba jaji mkuu amejiruhusu "kuingia kwenye mazungumzo na mtu anayewatisha".

BBC iliwasiliana na ofisi ya msemaji wa serikali na ofisi ya rais ili kupata maoni yao kuhusu tuhuma za kuhujumu idara ya mahakama.

Baada ya mkutano huo, kauli za jaji mkuu na rais zilisisitiza kwamba wamejitolea kusimamia sheria na uhuru wa mahakama.

Jaji mkuu alisema wamekubaliana kuwa hatua mahususi zitawasilishwa ili kuharakisha kesi za ufisadi.

Pia iliamuliwa kuwa wabunge na serikali wangeunga mkono ongezeko la fedha kwa idara ya mahakama, ikiwa ni pamoja na kuajiri majaji zaidi.

Licha ya mkutano huo, ukosoaji wa majaji uliendelea.

Siku ya Alhamisi, Chama cha Mahakimu na Majaji wa Kenya (KMJA) kilisema "kimeona kwa wasi wasi mkubwa kuendelea kwa mashambulizi dhidi ya mahakama, majaji binafsi na mahakimu na tabaka la kisiasa hata baada ya mkutano wa pande tatu".

Ilisema mahakama sasa zitazingatia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaoshambulia mahakama, majaji binafsi na mahakimu.

Mapema wiki hii, Mahakama ya Juu ilichukua hatua isiyo ya kawaida ya kumzuia kwa muda usiojulikana wakili mashuhuri anayeiunga mkono Ahmednasir Abdullahi kufika mbele yake, baada ya kumshutumu kwa "kuendesha kampeni inayolenga kuibua kashfa, kukejeli na kuidhalilisha mahakama hii".

Bw Abdullahi alisema ilikuwa ni "beji ya heshima" kwa X, na baadaye akasema kwamba angewasilisha ombi la kupinga marufuku hiyo katika Mahakama ya Afrika Mashariki katika nchi jirani ya Tanzania badala ya "kupoteza muda katika mahakama ya wafisadi ya Koome".

Mgawanyiko kati ya mahakama na tabaka la kisiasa unatarajiwa tu kuongezeka, huku kila upande ukisimama kidete.

Licha ya maamuzi hayo, Bw Ruto ameapa kuendelea na miradi ya serikali, jambo ambalo huenda likasababisha makabiliano zaidi na idara ya mahakama.

Kuna hofu kuwa jambo hilo huenda likaweka mazingira ya Wakenya wengine kutotii maamuzi ya mahakama, na kusababisha “taharuki” kama jaji mkuu alivyoonya.

KMJA ilibainisha Alhamisi kuwa katika mji wa magharibi wa Eldoret, "kiongozi mmoja wa kisiasa aliyechaguliwa alijipanga na kuongoza genge kuharibu mali ambayo bado inafikishwa mahakamani".

Mahakama ilipoamua Ijumaa, Bw Ruto alisema ana uungwaji mkono wa kutosha wa umma kuendelea na miradi ya ujenzi wa nyumba, ambayo alisema inaibua ajira nyingi kwa vijana wa Kenya.

"Mapenzi ya watu ni mapenzi ya Mungu," alisema, akiongea kwa Kiswahili na umati wa watu katika mji mmoja katikati mwa Kenya, na kuongeza kuwa mpango huo utaendelea licha ya kurudi nyuma kwa muda.

Rais alisema serikali itakata rufaa dhidi ya uamuzi huo na bunge litafanyia kazi sheria mpya ya hazina ya nyumba ambayo itaruhusu mpango huo kuendelea.

Mtu anaweza kufikiria itikio la Bw Ruto ikiwa hilo lingepingwa mahakamani.