Ukraine inaweza kushindwa vita 2024. Hivi ndivyo inavyoweza kutokea.

g

Na Frank Gardner ,

Mwandishi wa BBC wa masuala ya usalama

Aliyekuwa kamanda wa vikosi vya muungano wa Uingereza ameonya kuwa Ukraine inaweza kushindwa katika vita na Urusi.

Jeberaki Richard Barrins ameiambia BBC kuwa kuna “hatari kubwa” ya Ukraine kushindwa vita vinavyoendelea nchini humo, mwaka huu.

Sababu kubwa anasema ni “kwasababu Ukraine inaweza kujihisi kuwa haiwezi kushinda.”

“Na watakapofikia kwenye hatua hiyo, kwanini watu watataka kuendelea kupigana na kufa, ili kutetea nchi ambayo haiwezi kutetewa?”

Ukraine bado haijafika kwenye hatua hiyo.

Lakini vikosi vyake vinaishiwa silaha, wanajeshi na silaha za anga. Vikosi vyake vingi vililishindwa kuondoa vikosi vya Urusi kutoka kutoka kwenye eneo ambalo walikuwa wanadhibiti na sasa Moscow inajiandaa kwa mashambulizi mengine ya majira ya kiangazi.

Kwa hivyo hatua hiyo itakuwa vipi na malengo yake ya kimkakati ni yapi?

“Sura ya vikosi vya Urusi vitakavyokuja ipo wazi”, alisema Gen Barrons.

Tunaiona Urusi ikipigana katika mstari wa mbele, ikitumia njia zenye mkakati mkubwa katika ufyatuaji risasi, silaha kundi la watu wa ziada wenye uelewa wa matumizi ya silaha mpya.

h

Chanzo cha picha, getty Images

Maelezo ya picha, Ukraine sasa ina uhaba mkubwa wa risasi, kwa sehemu kwa sababu ya mizozo ya kisiasa katika mataifa ya Magharibi

Hizi ni pamoja na bomu linalojulikana kama FAB glide ambalo lilitumika wakati wa Sovieti lenye mabawa na teknolojia ya GPS inayoilekeza na lenye vilipuzi vikubwa likiwa na uzito wa kilogramu 1500 na linaathiri vibaya vikosi vya Ukraine.

Wakati fulani katika majira ya kiangazi mwaka huu," anasema Jenerali Barrons, "tunatarajia kuona mashambulizi makubwa ya Urusi, Wakiwa na nia ya kufanya zaidi kuliko kupiga hatua na kupata faida ndogo, ili kujaribu kuvishambulia vikosi vya Ukraine.

“Na kama hilo likitokea basi tutaingia kwenye hatari ya majeshi ya Urusi kupenya na kuingia katika maeneo ya Ukraine ambayo wanajeshi wa Ukraine watashindwa kuwazuia."

Lakini ni katika maeneo gani?

Mwaka jani Urusi ilijua ni maeneo gani ambayo Ukraine wangeshambulia kuanzia upande wa kusini mwa Zaporizhzhia hadi kuelekea kwenye bahari ya Azov. Ilipanga vizuri na kufanikiwa kuharibu mipango ya Ukraine.

Na sasa Urusi imekusanya wanajeshi wake na kuifanya Kyiv kubahatisha ni wapi itashambulia.

g

Mojawapo ya changamoto ambazo Ukraine inayo," anasema Dk Jack Watling, mtafiti mwandamizi mwenzake katika vita vya ardhini katika taasisi ya fikra ya Whitehall ya Taasisi ya Huduma za Kifalme ya Umoja wa Kifalme (Rusi), "ni kwamba Urusi inaweza kuchagua mahali wanapoweka majeshi yao.

“Ni mstari mrefu wa mbele ya mapigano na Ukraine lazima iweze kujilinda.”

Kitu ambacho, hawawezi.

Wanajeshi wa Ukraine watashindwa," anasema Dk Watling. "Swali ni je: ni kwa kiasi gani na ni maeneo gani ya watu yataathirika?"

Inawezekana kabisa kuwa majenerali wa Urusi bado hawajaamua ni mwelekeo gani waweke juhudi zao zaidi. Lakini inawezekana kabisa wakalenga zaidi katika maeneo makubwa matatu.

Kharkiv

“Ni hakika kabisa kuwa Kharkiv ipo hatarini” anasema Dkt Watling.

Kama mji wa pili wa Ukraine, ambao upo karibu na mpaka wa Urusi, Kharkiv ni lengo linalovutia sana kwa Moscow.

Hivi sasa unashambuliwa kila siku na makombora ya Urusi, huku Ukraine ikishindwa kuweka ulinzi wa kutosha wa anga ili kuzuia mchanganyiko hatari wa ndege zisizo na rubani, meli na makombora yanayolenga upande wake.

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Urusi huipiga Kharkiv kila siku kwa kutumia ndege zisizo na rubani, makombora na mizinga

"Nadhani mashambulizi ya mwaka huu yataibuka kutoka Donbas ikiwa kama lengo lao la kwanza," anaongeza Jenerali Barrons, "na jicho lao litakuwa Kharkiv ambao upo umbali wa kilomita 29 kutoka mpaka wa Urusi, ni tuzo kubwa sana. "

Je, Ukraine bado inaweza kusimama imara endapo Kharkiv itaanguka? Wachambuzi wanasema ndiyo, lakini litakuwa ni pigo kubwa kwa ari yake na uchumi wake.

The Donbas

Eneo la mashariki mwa Ukraine linalojulikana kwa pamoja kama Donbas limekuwa kwenye vita tangu 2014, wakati watu wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Moscow walijitangaza kuwa "jamhuri ya watu".

Mnamo mwaka wa 2022, Urusi iliteka wilaya mbili za Donbas, au majimbo, ya Donetsk na Luhansk, kinyume na sheria. Hapa ndipo mapigano mengi juu ya ardhi yamekuwa yakifanyika katika kipindi cha miezi 18 iliyopita.

Ukraine, kwa kutatanisha, imetumia juhudi nyingi, katika nguvukazi na rasilimali, ili kujaribu kushikilia kwanza mji wa Bakhmut, na kisha Avdiivka.

Imepoteza yote miwili, pamoja na baadhi ya vikosi vyake bora kwa mapigano, kwenye jaribio hilo.

Kyiv imepinga kwamba upinzani wake umesababisha hasara kubwa kwa Warusi.

Hiyo ni kweli, huku uwanja wa vita katika maeneo haya ukiitwa "eneo la machinjio ya nyama".

Lakini Moscow ina askari wengi zaidi wa kutupa kwenye vita - na Ukraine haina.

Kamanda wa Majeshi ya Marekani barani Ulaya, Jenerali Christopher Cavoli, ameonya kuwa iwapo Marekani haitapeleka silaha nyingi na risasi zaidi nchini Ukraine basi vikosi vyake vitazidiwa nguvu.

Ni jambo kubwa. Mbinu za jeshi la Urusi zinaweza kuwa duni kuliko za Ukraine, lakini lina ubora wa juu katika idadi, haswa silaha, kwamba ikiwa haitafanya chochote mwaka huu, chaguo lake la msingi litakuwa kurudisha vikosi vya Ukraine katika mwelekeo wa magharibi na kuchukua kijiji baada ya kijiji.

Zaporizhzhia

Mji huu, pia, ni tuzo linaloivutia Moscow.

Mji wa kusini mwa Ukraine wenye zaidi ya watu 700,000 upo karibu na mstari wa mbele wa Urusi.

Pia ni jambo hatari kwa Urusi ikizingatiwa kuwa ni mji mkuu wa eneo lenye jina moja ambalo Urusi umeuteka kinyume cha sheria, na bado mji huo unaishi kwa uhuru mikononi mwa Ukraine.

Lakini ulinzi wa kutisha ambao Urusi ilijenga kusini mwa Zaporizhzhia mwaka jana, kwa matarajio sahihi ya shambulio la Ukraine, sasa ungeweza kutatiza kusonga mbele kwa Urusi kutoka huko.

Kinachojulikana kama Mstari wa Surovikin, unaojumuisha aina tatu za ulinzi, umezungukwa na uwanja mkubwa zaidi wa migodi duniani. Urusi inaweza kusambaratisha eneo hili kwa sehemu kadhaa lakini maandalizi yake huenda yangegunduliwa.

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ukraine sasa ni moja ya maeneo yanayochimbwa zaidi duniani

Lengo la kimkakati la Urusi mwaka huu linaweza lisiwe hata la kumiliki eneo fulani. Linaweza tu kuwa kuvunja nguvu ya kuendelea kupigana ya Ukraine na kuwashawishi wafuasi wake wa Magharibi kuwa vita hivi wameshashindwa.

Dkt. Jack Watling anaamini kuwa leonga la Urusi ni “kutengeneza hali ya kukosa matumaini.”

“Mashambulizi haya ya Urusi hakika hayotomaliza mzozo huo, bila kujali hali itakuwaje kwa pande zote mbili," anasema.

Jenerali Barrons pia ana mashaka kuwa, licha ya hali mbaya ambayo inaikumba Ukraine kwasasa, Urusi itaendesha moja kwa moja kushambulia wakitumia silaha zilizoendelea zaidi.

“Nadhani kitu ambacho kinaweza kutokea kuwa Urusi itakuwa imefaidika, lakini haitokuwa imeweza kupata mafanikio makubwa.

“Haitokuwa na vikosi vikubwa ama vyenye nguvu ambavyo vitaweza kukabiliana na mto (Dnipro)…lakini vita hivi vitakuwa vimependelea upande wa Urusi.”

Kitu kimoja ambacho ni cha uhakika ni kuwa: Rais wa Urusi, Vladimir Putin hana nia yoyote ya kukata tamaa kwenye suala la kushambulia Ukraine.

Yeye ni kama mchezaji wa kamari, anafanya lolote lile ili kupata ushindi. Anategemea nchi za Magharibi zitashindwa kuipatia Ukraine msaada wa kutosha ili wawezi kujilinda.

Licha ya kuwepo kwa mikutano yote ya NATO, makongamano yote, na hotuba zote za kusisimua, bado kuna nafasi ya kuwa yupo sahihi.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Elizabeth kazibure na kuhaririwa na Dinah Gahamanyi