Mhimili wa dunia umeinama sentimita 80 kuelekea mashariki: Nini kimesababisha?

ffdfdfd

Chanzo cha picha, Science Photo Library

Maelezo ya picha, Kuhama kwa maji hubadilisha uzito wa dunia

Mhimili wa dunia umeinama sentimita 80 kuelekea mashariki kutokana na uchimbaji wa maji ya ardhini na kuyahamishia sehemu nyingine. Mabadiliko haya yalitokea kati ya 1993-2010.

Kulingana na utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la Geophysical Research Letters, sababu ya hii ni uchimbaji wa maji ya chini ya ardhi na mwendo mkubwa wa maji ndani ya bahari. Wanasema kwamba mwenendo huu huhamisha kiwango kikubwa cha maji kama bahari, na kusababisha kuinamisha kwa mhimili wa dunia.

Mhimili ni mstari wima ambao unatoka kaskazini hadi kusini kupitia katikati ya dunia unapojizungusha yenyewe. Hii inaitwa Axis kwa Kiingereza. Kiwango cha bahari pia huathiriwa na kuhamishwa kwa chemichemi.

"Maji ya ardhini yaliyochimbwa hufukiza angani au kuingia kwenye mito. Kisha yanakutana na bahari kwa namna ya mvua. Kwa njia hii maji hufika baharini kutoka ardhini,'' anasema profesa wa sayansi ya ardhi katika chuo kikuu cha kitaifa cha Seoul huko Korea Kusini, Ki-Weon Seo.

Iligunduliwa mnamo 2016 kuwa maji yana uwezo wa kubadilisha mzunguko wa Dunia. Utafiti wa 2021 ulioangazia jinsi barafu inayoyeyuka na maji kuingia baharini huathiri mwelekeo wa mhimili wa dunia.

Athari ya shughuli za binadamu

ioiujkjjh

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maji ya chini ya ardhi huathiri kupanda kwa kiwango cha bahari

Wanasayansi wametaja katika utafiti mpya mabadiliko waliyoyaona kuhusiana na mhimili wa dunia wa mzunguko na mienendo ya maji.

Hapo awali, wanasayansi walidhani kwamba sababu ya kuhama kwa maji ilikuwa kuyeyuka kwa barafu. Lakini, baadaye mabadiliko ya usambaaji wa maji ya chini ya ardhi yaliyongezwa kama chanzo chengine.

Uchunguzi wa awali ulikadiria kuwa wanadamu walitoa gigatoni 2,150 za maji ya chini ya ardhi kati ya 1993-2010. Kiasi cha gigatonni 2,150 za maji ni sawa na kupanda kwa usawa wa bahari kwa zaidi ya milimita 6.

Utafiti huu mpya ni muhimu, alisema Surendra Adhikari, mwanasayansi wa utafiti kwa NASA. Surendra Adhikari ni mmoja wa waandishi wa utafiti wa 2016 'Athari ya usambaaji mpya wa Maji”.

Seo alifafanua kuwa usambaaji mpya wa maji hauathiri misimu.

"Mhimili wa mzunguko wa dunia kwa kawaida hubadilika kwa mita chache tu kwa mwaka. Hii ina maana kwamba mabadiliko ya mita moja katika mzunguko wa mhimili katika miaka kumi au miwili haitaathiri hali ya hewa.

Jambo muhimu kwa wanasayansi kuzingatia hapa ni kuthibitisha kwamba uchimbaji wa maji ya ardhini huathiri mhimili wa mzunguko wa dunia.

weewwewewe

Chanzo cha picha, Getty Images

Wasiwasi

"Kama mkaazi wa sayari ya dunia na baba, nina wasiwasi mkubwa kujua kwamba uchimbaji wa maji chini ya ardhi ni sababu nyingine ya kupanda kwa kina cha bahari. Ukame unaweza kuwa mbaya zaidi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Uchimbaji wa maji chini ya ardhi na ukame unaweza kuongezeka.

Wanasayansi wana wasiwasi juu ya uhusiano kati ya mienendo ya maji na kupanda kwa viwango vya bahari.

"Ni wasiwasi mkubwa. Kwa sababu wengi wetu tunaishi katika miji ya pwani.

Kizazi changu kitaishi vizuri. Lakini, watoto wangu wanaweza kuwa matatani kutokana na kupanda kwa kina cha bahari katika siku zijazo,” Seo alisema.