Monkeypox: Ugonjwa huu unaweza kuwa janga?

w

Chanzo cha picha, Science Photo Library

Maelezo ya picha, Virusi vinasababisha homa kali na vipele

Kuna maswali kadhaa yasiyo na majibu ya wazi na ya haraka kuhusu milipuko wa ugonjwa wa Monkeypox ambao tunaona ukienea katika zaidi ya nchi kumi na mbili.

Isipokuwa kwa wachache, virusi hivi kwa ujumla vimedhibitiwa katika maeneo ya Afrika Magharibi na Kati, lakini sasa tuko katika hali mpya ambayo inashangaza na inatia wasiwasi.

Hapo awali, idadi ndogo ya visa viliibuka katika sehemu kadhaa duniani, na ambazo zinaweza kuhusishwa na watu ambao walikuwa wamesafiri kwenda nchi zilizoathiriwa na kurudi na maambukizi.

Sasa haijulikani watu wanaupata ugonjwa huo kutoka kwa nani.

Ingawa wagonjwa wanakuwa na mabadiliko, jumuiya ya wanasayansi imeanza kufanya kazi ili kufafanua haraka kile kinachotokea.

1. Je ugonjwa wa monkeypox unaweza kuwa janga?

"Haiwezekani kabisa," Profesa Brian Ferguson, kutoka Idara ya Patholojia katika Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza, anaiambia BBC Mundo.

Na kwa nini inachukuliwa kuwa haiwezekani kuwa janga?

Sababu ya kwanza ni kwamba ni vigumu sana kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine, tofauti na virusi vya kupumua kama vile Sars-Cov2.

Uambukizaji wa Monkeypox hutokea wakati mtu anapogusana na virusi kupitia mnyama, binadamu au vifaa vyenye maambukizi.

M

Chanzo cha picha, Getty Images

Sababu ya pili ni kwamba dalili za wazi za monkeypox, hasa kuonekana kwa kutokea kwa vipele vikubwa kwenye ngozi, husaidia kutambua kisa kwa haraka zaidi na kudhibiti milipuko kwa urahisi.

Na mwisho, ni ugonjwa ambao ingawa wengi hawajausikia hadi sasa, umejulikana tangu 1958 na unachunguzwa zaidi.

2: Kwa nini tunaona milipuko kwa wakati mmoja katika nchi nyingi?

Kupata jibu swali la swali hili ndio dharura kuu kwa wanasayansi, njia ya kuzuia visa zaidi kutokea na kudhibiti milipuko wake.

Kwa sasa, monkeypox inaonekana kuenea hasa kupitia vitendo vya ngono, ambavyo hata hivyo haimaanishi kuwa ni ugonjwa wa zinaa.

Pox

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni mapema sana kufanya hitimisho kuhusu ugonjwa huu na unavyotokea, lakini hivi sasa hakuna ushahidi kwamba tunashughulika na ugonjwa usiojulikana.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa visa vya sasa vya ugonjwa huu vinahusiana sana na aina za virusi zilizoonekana mnamo mwaka 2018 na 2019.

3. Kwa nini tunaona visa vingi zaidi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja?

Je, tabia za ngono hurahisisha kuenea kwa ugonjwa huu? Je, ni bahati mbaya tu? Je, jamii inafahamu zaidi afya ya ngono na kuwa na uchunguzi wa kimatibabu unaowezesha utambuzi?

Kuna maswali kadhaa ambayo yanaweza kuulizwa wakati wa kuona kwamba wengi wa walioathiriwa ni wapenzi wa jinsia moja na wapenzi wa jinsia mbili, lakini wanasayansi wanaonya kwamba "hakuna kitu cha kibaolojia katika virusi ambacho kinasema kuwa jamii hii inahusika zaidi kuliko wengine," anasema Ferguson, ambaye anahimiza kutolinyanyapaa kundi hili bila misingi.

w

Chanzo cha picha, Science Photo Library

4. Je, tutaona kesi nyingi zaidi katika wiki zijazo?

Ni vigumu kutabiri kwa kiasi fulani kwa sababu ukubwa wa maambukizi na sababu zinazotufanya tuone mlipuko mkubwa zaidi wa ugonjwa huu nje ya Afrika bado hazijaeleweka kikamilifu.

Hata hivyo, wataalam wanasisitiza kwamba mara maambukizi ama visa vinapobainika na tahadhari za afya kutolewa, inapaswa kuwa "rahisi kudhibiti milipuko."

"Muingiliano na wanyama pori unaongezeka kutokana na ukataji wa miti, ukuaji wa miji usiodhibitiwa, utalii na mabadiliko ya tabia nchi...kuna sababu nyingi ambazo pamoja na kinga ya kundi kuwa ndogo, husababisha milipuko ya magonjwa kujitokeza mara kwa mara, ndicho kinachotokea," anamalizia Raúl Rivas González, Profesa kutoka chuo Kikuu cha Salamanca Hispania.