Vita vya Ukraine: Kwanini Ukraine inaweza kushindwa na Urusi 2024?

d

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

  • Author, Frank Gardner
  • Nafasi, BBC

Kamanda wa zamani wa Uingereza ameonya kwamba Ukraine inaweza kushindwa na Urusi mwaka 2024.

Jenerali Sir Richard Barrons aliiambia BBC kuwa kuna "hatari kubwa" Ukraine inaweza kupoteza vita mwaka huu.

Sababu ni kwamba "ikiwa Ukraine itafikia hatua na kufikiri kuwa haiwezi kushinda vita. Kwa nini watu watataka kupigana na kufa, ili tu kutetea wasiyowezekana?

Pia unaweza kusoma

Ukraine yashindwa kusonga mbele

X

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Kwa miaka miwili, Ukraine imekuwa ikijilinda dhidi ya uvamizi mkubwa wa Urusi.

Vikosi vya Ukraine vinakosa silaha, wanajeshi na ulinzi wa anga. Mwaka jana, mashambulizi mengi yalishindwa kuwaondoa Warusi kutoka kwenye ardhi waliyokuwa wameikamata, na Moscow sasa inajiandaa kwa mashambulizi ya majira ya joto.

"Tunaiona Urusi ikishinda mstari wa mbele kwa kutumia silaha na makombora, pamoja na wanajeshi wa ziada wanaofunzwa matumizi ya silaha mpya,’’ anasema Barrons.

"Wakati wa kiangazi," anasema Jenerali Barrons, "tutarajie kuona uvamizi mkubwa wa Urusi, kwa nia ya kusonga mbele polepole kujaribu kuvunja safu za wanajeshi wa mstari wa mbele wa Ukraine.

"Iwapo hilo litatokea, kuna hatari ya vikosi vya Urusi kuingia katika maeneo ya Ukraine ambapo vikosi vya Ukraine haviwezi kuwazuia.

Mwaka jana, Urusi ilijua haswa ni wapi Ukraine ingeshambulia; kutoka upande wa Zaporizhzhia kusini, kuelekea Bahari ya Azov. Walipanga ulinzi imara na wakafaulu kuizuia Ukraine kusonga mbele.

Leo mambo yapo kinyume chake; Urusi inapeleka wanajeshi wake mbele na kuiacha Kyiv ikiwa haina uhakika juu ya shambulio lake lijalo.

Mchambuzi wa masuala ya kiusalama Jack Watling, kutoka taasisi ya Royal United Services (Rusi), anasema moja ya changamoto zinazoikabili Ukraine ni kwamba Urusi wanaweza kuchagua mahali pa kuwaweka majeshi wao.

"Kwa sababu ni mstari wa mbele wa vita ambao ni mrefu sana na Ukraine lazima waweze kuutetea kwa ukamilifu. Jambo ambalo hadi sasa bado hawajafanikiwa.’’

"Jeshi la Ukraine litapoteza nafasi," anasema Dakt. Watling. "Swali ni kwa kiwango gani na maeneno gani ya watu yataathirika.

Inawezekana kabisa kwamba makamanda wakuu wa Urusi bado hawajaamua juu ya mwelekeo wao. Hata hivyo, inawezekana kukawa na machaguo matatu katika maeneo matatu makubwa.

Kharkov

C

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Ukraine sasa ina uhaba mkubwa wa silaha

"Kwa hakika Kharkiv iko hatarini," anasema Dk. Watling. Mji wa pili wa Ukraine, ulio karibu na mpaka wa Urusi. Kharkiv ni mji unaoivutia Moscow.

Hivi sasa iko chini ya mashambulizi ya kila siku ya makombora ya Urusi, huku Ukraine ikishindwa kuweka ulinzi wa kutosha wa anga kuzuia makombora na ndege zisizo na rubani, zinazolenga upande wake.

"Nadhani lengo la kwanza la Urusi la mwaka huu litakuwa ni kuondoka Donbas," anasema Jenerali Barrons, "na kwenda Kharkiv, mji ambao uko umbali wa kilomita 29 kutoka mpaka wa Urusi."

Je, Ukraine bado inaweza kupigana ikiwa Kharkiv itaanguka mikononi mwa Urusi? Ndiyo, wachambuzi wanasema, lakini itakuwa pigo kubwa kwa ari na uchumi wake.

Donbas

CX

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Urusi huipiga Kharkiv kila siku kwa kutumia ndege zisizo na rubani, makombora na milipuko ya mabomu

Hili ni eneo la mashariki mwa Ukraine linalojulikana kwa pamoja kama Donbas, limekuwa kwenye vita tangu mwaka 2014, wakati watu wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Moscow walipojitangazia uhuru.

Mwaka 2022, Urusi iliteka maeneo mawili ya Donbas, yaani majimbo mawili ya Donetsk na Luhansk. Hapa ndipo mapigano mengi ya ardhini yamefanyika katika kipindi cha miezi 18 iliyopita.

Ukraine ilifanya juhudi kubwa, katika masuala ya wanajeshi na rasilimali, katika kujaribu kutetea mji wa Bakhmut na kisha Avdiivka.

Lakini ilipoteza miji yote miwili, pamoja na baadhi ya askari wake bora katika vita, katika jaribio la kulinda miji hiyo.

Kyiv ilisema kwamba upinzani wake umesababisha hasara kubwa kwa Urusi. Mapigano katika maeneo haya, yalisababisha umwagaji damu mkubwa sana.

Lakini Moscow ina wanajeshi wengi zaidi wa kupeleka vitani, jambo ambalo ni tofauti kwa Ukraine.

Kamanda wa majeshi ya Marekani barani Ulaya, Jenerali Christopher Cavoli, alionya kwamba ikiwa Marekani haitatuma silaha nyingi zaidi kwa Ukraine, vikosi vyake vitazidiwa kwenye uwanja wa vita kwa uwiano wa kumi kwa mmoja.

Mbinu, amri na vifaa vya jeshi la Urusi vinaweza kuwa duni kuliko vile vya Ukraine, lakini Urusi ina wanajeshi wa kupigana.

Ikiwa Ukraine haitafanya chochote mwaka huu, chaguo la msingi la Urusi litakuwa ni kuendelea kusukuma vikosi vya Ukraine kuelekea magharibi, kuchukua kijiji baada ya kijiji.

Zaporozhye

S

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Ukraine ya leo ni moja ya nchi yenye mabomu mengi ya ardhini.

Mji huu wa kusini mwa Ukraine, ambao una wakazi zaidi ya 700,000 (kabla ya vita), uko karibu na mstari wa mbele wa Urusi.

Pia ni mwiba kwa Urusi, ikizingatiwa kuwa ni mji mkuu wa Donbas, na mji huo bado unaishi kwa uhuru mikononi mwa Ukraine.

Lakini ulinzi wa kutisha ambao Urusi uliuweka kusini mwa Zaporizhzhia mwaka jana, kwa kutarajia shambulio la Ukraine, unaweza kutatiza harakati za Urusi kusonga mbele.

Kinachojulikana kama Mstari wa Surovikin, ni tabaka tatu za ulinzi wa Urusi, ni uwanja mkubwa zaidi duniani wa mabomu ya chini ya ardhi. Urusi inaweza kusambaratisha ulinzi huo, lakini maandalizi yake yanaweza kugunduliwa.

Lengo la kimkakati la Urusi mwaka huu linaweza lisiwe hata kuchukua eneo. Inaweza kuwa ni kuporomosha ari ya wanajeshi wa Ukraine na kuwashawishi waungaji mkono wake wa Magharibi kwamba Ukraine imepoteza katika vita.

Jack Watling anaamini lengo la Urusi ni "kujaribu kuikatisha tamaa Ukraine."

Jenerali Barrons pia ana shaka kwamba, licha ya hali mbaya ambayo Ukraine inajikuta hivi sasa, Urusi itajiimarisha kwa mbinu madhubuti.

"Nadhani Urusi itasonga mbele, lakini itashindwa kupenya. Haitakuwa na nguvu za kutosha au kushambulia hadi mto Dnipro, lakini vita vitakuwa na faida kwa Urusi."

Jambo moja ni hakika: Rais wa Urusi Vladimir Putin hana nia ya kuacha kuishambulia Ukraine. Anazitegemea nchi za Magharibi kutoipatia Ukraine silaha za kutosha za kujilinda.