Vita vya Pili vya Dunia: Je, unajua jinsi Hitler alivyodanganywa na kompyuta ya kwanza ya kidijitali duniani?

f

Chanzo cha picha, CROWN COPYRIGHT

Maelezo ya picha, Colossus inachukuliwa kuwa kompyuta ya kwanza ya dijitali katika historia.

Picha hii ni ya kompyuta inayofanana na jengo kubwa la ghorofa iliopakiwa kwenye chumba kimoja kilichokuwa na kompyuta iliyowasaidia Washirika kushinda Vita kuu ya Pili ya Dunia.

Makao Makuu ya Mawasiliano ya Serikali ya Uingereza wiki hii yalifichua picha za kompyuta ya 'Colossus' iliyotumiwa kubainisha siri nyingi za kijasusi ambazo ziliwasaidia Washirika wa vita hivyo kuendeleza ushindi wao katika Vita ya Pili ya Dunia.

Kompyuta hii ambayo ilitengenezwa nchini Uingereza mwaka huu inatimiza miaka 80 tangu kuundwa kwake.

Picha hizi hutoa ushahidi wa jinsi kifaa hiki, ambacho kinachukuliwa na wataalamu wengi kuwa kompyuta ya kwanza ya kidijitali katika historia.

w

Chanzo cha picha, CROWN COPY

Maelezo ya picha, Jumla ya kompyuta 10 zilitengenezwa katika mradi wa Colossus.

Uwepo wake umekuwa wa shaka tangu Vita ya pili ya Dunia. Lakini ilikuwa ni mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambapo serikali ya Uingereza ilitoa maelezo yote ya kompyuta ya Colosso.

Kompyuta hii ilianza kufanya kazi mwanzoni mwa mwaka 1944.

Iliundwa ili kuchanganua na kufafanua habari iliyofichwa kwa nambari za siri zilizotumwa na mawakala wa Wanazi.

Uingereza iliidanganya Ujerumani kwa kutumia kompyuta ya kidijitali

w

Chanzo cha picha, CROWN COPY

Maelezo ya picha, Ilifichuliwa mapema miaka ya 2000 kwamba Mradi wa Colossus ulikuwepo.

Inakadiriwa mwishoni mwa vita kwamba kompyuta kama hizo 10 zilihusika katika utaftaji wa Wanazi wa nambari zilizofichwa.

Kompyuta hii yenye urefu wa karibu mita mbili ilinyenyuliwa na valvu 2,500. Inahitaji timu iliyo na ujuzi katika saketi ndani ya mashine mpya ili tumia.

Watu wengi waliobobea katika kuendesha kompyuta hii kubwa wanatoka katika Jeshi la wanamaji la wanawake.

Moja ya picha iliyotolewa wiki hii inaonyesha wanawake kutoka kikosi hicho wanaohudumu kwenye Coloso.

Makao makuu ya mawasiliano ya serikali ya Uingereza yalifichua mipango ya jinsi Colossus ilivyojengwa, barua inayorejelea "amri hatari za Wajerumani" zilizonaswa na kompyuta, na rekodi ya sauti iliyodaiwa kuonyesha kompyuta hiyo inavyofanya kazi.

g

Chanzo cha picha, CROWN COPY

Maelezo ya picha, Watu wengi walioendesha kompyuta ya Colossus walikuwa wanawake

Takwimu za Colosso zinaonyesha umuhimu wake. Watu 550 waliofanya kazi kwenye kompyuta waligundua karibu vipande milioni 6.3 vya habari za Wajerumani zilizotumwa kwa siri kwa kutumia nambari.

Moja ya mafanikio muhimu zaidi ya kompyuta hiyo ilikuwa kusaidia kumficha Hitler kwamba uvamizi wa kihistoria (D-Day) ungefanyika Normandy mnamo Juni 1944 kwa kudanganya kwamba D-Day ingefanyika katika jiji la Ufaransa la Calais.

Kulingana na wanahistoria tofauti, kompyuta hii ilipunguza kiwango cha vita na kuokoa maisha ya watu wengi.

Takwimu za Colosso zinaonyesha umuhimu wake. Watu 550 waliofanya kazi kwenye kompyuta waligundua karibu vipande milioni 6.3 vya habari za Wajerumani zilizotumwa kwa siri kwa kutumia nambari.

Moja ya mafanikio muhimu zaidi ya kompyuta hiyo ilikuwa kusaidia kumficha Hitler kwamba uvamizi wa kihistoria (D-Day) ungefanyika Normandy mnamo Juni 1944 kwa kudanganya kwamba D-Day ingefanyika katika jiji la Ufaransa la Calais.

Kulingana na wanahistoria tofauti, kompyuta hii ilipunguza kiwango cha vita na kuokoa maisha ya watu wengi.

h

Chanzo cha picha, CROWN COPY

Maelezo ya picha, Watu wengi walioendesha kompyuta ya Colossus walikuwa wanawake

Lakini zaidi ya ushawishi wake, wahandisi waliofanya kazi kwenye mradi wa Colossus walitia saini hati za siri ili kuvunja kanuni na kufichua habari. Kwa hivyo haikujulikana kwa miaka mingi kuwa kompyuta kama hiyo ilikuwepo.

Mpango huo ulizinduliwa rasmi na serikali ya Uingereza mwanzoni mwa karne ya 21.

Hatahivyo mpango huo ulitolewa rasmi na serikali ya Uingereza mwanzoni mwa karne mpya.

Baada ya vita, kompyuta 8 kati ya 10 zilizohusika katika operesheni hiyo ziliharibiwa.

Kwa kweli, Tommy Flowers, mhandisi aliyetengeneza kompyuta, aliamuru nyaraka zote kwenye Colossus zikabidhiwe.

Bill Marshall, mhandisi wa zamani wa makao makuu ya mawasiliano ambaye alifanya kazi huko Colossus katika miaka ya 1960 katika utunzaji wa siri alisema alisema hakujua jinsi kompyuta hiyo iliyochukua jukumu wakati wa vita.

Andrew Herbert, mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Makumbusho ya Kitaifa ya Kompyuta yenye makao yake katika Bletchley Park, alisema kutolewa kwa picha hizo ni fursa nyingine ya kusherehekea athari ya kudumu ya Colossus kwenye Vita vya Pili vya Dunia.

"Kwa mtazamo wa kiufundi, Colossus ilikuwa mtangulizi muhimu wa kompyuta ya kisasa ya kielektroniki," alisema.

Aliongeza kuwa, "Wengi wa wale walioitumia katika Bletchley Park walikuwa waanzilishi muhimu wa viongozi katika utengenezaji wa kompyuta ya Uingereza katika kipindi cha baada ya vita. Mara nyingi waliongoza ulimwengu kupitia kazi zao,” alisema.