Je vita vya Urusi nchini Ukraine vinakwenda kama Urusi inavyotaka?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Katikati ya mwezi Mei, Urusi iliishambulia Ukraine kutoka kaskazini-mashariki, ambako majeshi yake yalivamia eneo la Kharkiv na hata kuyateka baadhi ya maeneo ambayo Urusi iliyakalia mwanzoni mwa vita lakini baadaye iliyaachilia.

Baadhi ya wataalamu wanaelezea hali hiyo kama vita "wakati ulimwengu umelala."

Ilipiganwa karibu na mji wa Vovchansk, ulioko kilomita tano kutoka mpaka wa Urusi na Ukraine.

Mtazamo wa kile kinachoweza kutokea katika siku zijazo ni wa kutisha kwa Ukraine: Kuna ishara kwamba Urusi inasonga mbele hadi kufikia mahali ambapo inaweza kuukamata mji wa Khirkiv, mji mkubwa wa Ukraine wenye idadi ya watu milioni 1.4.

Ukraine inajihami kwa silaha, na msaada wa kijeshi kutoka nchi za Magharibi unachukua muda mrefu kuifikia baada ya miezi kadhaa uamuzi wa kupelekwa kwake Ukraine.

Ishara hiyo inaonyesha kuwa Urusi imegundua makosa ambayo imeyafanya katika siku za nyuma, kwa hivyo hatua inayofuata itakayochukua kuhusiana na vita inaweza kuwa uvamizi katika majira ya kipupwe.

Mchambuzi wa masuala ya kijeshi katika kituo cha Uingereza Royal United Services Center, Jack Watling amesema kuwa lengo la uvamizi huo halitakoma kaskazini mashariki mwa Ukraine, litapanuliwa hadi eneo la "Donbas" mashariki mwa Ukraine, ambalo tayari lina sehemu ya eneo hilo. Limekuwa chini ya udhibiti wa Urusi tangu mwaka 2014.

Unaweza pia kusoma:

Je, Urusi imefanikiwa katika uvamizi wake wa hivi karibuni?

Ni karibu miezi miwili tangu vikosi vya Urusi vilipopenyeza zaidi na zaidi katika maeneo ambayo wanapigana, lakini walishindwa kuchukua udhibiti kamili wa miji ya Vovchansk na Chasiv Yar. Maeneo yote yamekumbwa na mapigano makali katika kipindi cha wiki sita zilizopita.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuidhibiti miji hiyo kutaipa Urusi fursa kubwa ya kukata usambazaji wa silaha na chakula kwa jeshi la Ukraine na vikosi vya Urusi vitapata fursa ya kuendelea kuyakalia maeneo zaidi.

Sababu kuu ya kutoendelea kuingilia kati ni, kwa upande mmoja, kushindwa kwa Urusi kupeleka vikosi vya kijeshi katika maeneo sahihi na kwa wakati sahihi ili kuhakikisha nia yake ya vita.

Kwa upande mwingine, msaada mpya wa vifaa vya kijeshi kutoka Magharibi umeanza kuingia Ukraine, kitu ambacho kimeongeza ujasiri wake wa kuilinda ardhi yake.

Hata hivyo, wakati huo huo mashambulizi ya Urusi yalicheleweshwa na vikosi vya Ukraine vikapata fursa ya kupigana, hiyo haimaanishi kuwa Urusi haikufanikiwa katika vita. Mambo mawili yanaathiri jinsi mambo yanavyokwenda.

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Sababu ya kwanza: Makombora ya Cruise

Moja ya sababu ni matumizi ya mabomu ya makombora ya cruise ambayo ni moja ya njia ambayo Urusi imekuwa ikiitumia katika hadi sasa.

Maafisa wa Ukraine wanasema anga ya Urusi imekuwa ikidondosha makombora 100 kwa siku katika wiki za hivi karibuni.

Mabomu ya kulipua ni ya kawaida na mengi ya hayo yalianza kutumika katika enzi ya Muungano wa usovieti na yalitumika katika Vita vikuu vya Pili vya Dunia.

Lakini pia wamekuwa wakitumia makombora ya kisasa ya GPS kufuatilia programu – yanayowezesha kulenga shabaha. Ndege za kivita za Urusi zimekuwa zikidondosha makombora mara kwa mara wakati zikiruka katika anga la Urusi.

Ni vigumu sana kwa mabomu na droni kuyakabili makombora ya cruise.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky alifafanua suala hili katika mahojiano ya hivi karibuni na gazeti la Marekani.

Ili kuzuia ndege za kivita za Urusi kuacha mabomu hayo ya angani, Ukraine iliomba mataifa ya magharibi ruhusa ya kutumia vifaa vya kigeni kushambulia ardhi ya Urusi kwa kushambulia ndege zake za kivita.

Mchambuzi Mykola Bieleskov, alisema kuwa shambulio dhidi ya kambi ya jeshi la anga la Urusi ni njia pekee ya kukomesha "nguvu ya mabomu ya angani."

Sababu ya pili: Mashambulizi ya Urusi

Mafanikio ya Ukraine katika vita na kuendelea kwa mashambulizi ya Urusi kwenye vituo vya nishati vya Ukraine yameilazimu Marekani kubadili fikra zake kuhusu matumizi ya silaha ambazo zitaisaidia Ukraine katika kupambana na Urusi.

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Awali ya yote, Ukraine ilipata ruhusa ya kuzindua silaha zilizotolewa na Marekani kwenye kambi za kijeshi za Urusi karibu na mkoa wa Khirkiv.

Mwishoni mwa mwezi Juni, mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Jake Sullivan alisema kuwa makubaliano na Ukraine kuhusu matumizi ya silaha zilizotolewa na Marekani dhidi ya Urusi yaliongezwa "hadi popote vikosi vya Urusi vinapotokea katika mpaka wa Urusi na Ukraine."

Ruhusa hii haikupatikana moja kwa moja kwa sababu watu wengi nchini Marekani na maeneo mengine ya Ulaya Magharibi wanasita kukabiliana na Urusi. Kremlin imesema katika siku za nyuma kwamba kuruhusu Ukraine kutumia silaha za Marekani dhidi ya Urusi inaonyesha "ushirikiano wa Marekani katika vita".

Unaweza pia kusoma:

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vitaendelea kwa muda gani?

Licha ya ukweli kwamba vita ambayo Urusi inafanya haijaipatia maendeleo yoyote makubwa katika suala la uvamizi hadi sasa, hali ya sasa haijaeleweka.

Jeshi la Urusi ni kubwa zaidi kuliko lile la Ukraine. Jenerali mwandamizi katika jeshi la Ukraine alisema katika baadhi ya maeneo jeshi la Urusi ni mara 10 ya lile ya Ukraine. Hata hivyo, Urusi bado inapoteza wanajeshi wake.

Uchunguzi uliofanywa na idhaa ya BBC ya Urusi kuhusu idadi ya hasara ya kijeshi iliyopata inaonyesha majeruhi zaidi katika wiki chache zilizopita, ukiakisi kile kilichotokea katika mashambulizi ya hivi karibuni.

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Mambo mengi hayaendi kama yalivyopangwa tangu kuanza kwa vita mnamo Februari 2022, lakini hamu ya Urusi kupinga msaada wowote wa Magharibi kwa Ukraine inazidi kuwa imara.

Rais wa zamani wa Urusi na waziri mkuu wa zamani Dmitry Medvedev amesema baada ya bunge la Marekani kuidhinisha mfuko mpya wa msaada kwa Ukraine: "Tutashinda, licha ya msaada wa dola bilioni 61. Nguvu na uaminifu kwa upande wetu."

Akizungumzia kuhusu muda gani vita vitachukua, Francis Dearnley, mhariri wa gazeti la Telegraph, gazeti kubwa zaidi nchini Uingereza, ambaye mtangazaji wake alielezea kwamba "Magharibi na Marekani zinajibu badala ya kupigana - Zalensky mshirika bora wa Amerika – ambayo iliidhinisha matumizi ya silaha kuendelea na vita lakini sio kwa ushindi."

"Vita hivi, ambavyo ni vibaya zaidi barani Ulaya tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia, vimedumu kwa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa."

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi