Urusi: Kwanini maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi wanakamatwa?

wesd

Chanzo cha picha, REUTERS

Maelezo ya picha, Generali Vadym Shamarin

Mkuu wa Kurugenzi Kuu ya Jeshi na Naibu Mkuu wa majenerali, Jenerali Vadym Shamarin, amekamatwa. Hii ni mara ya nne kukamatwa afisa wa ngazi ya juu wa Urusi ndani ya mwezi mmoja.

Shamarin anashukiwa kupokea hongo, mashirika ya Urusi yakinukuu mahakama ya kijeshi, ambayo iliamua jenerali huyo awekwe kizuizini.

Wa kwanza kukamatwa alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi Timur Ivanov, ambaye alisimamia ujenzi wa kambi za jeshi. Alikamatwa Aprili 24.

Katikati ya Mei, ilifahamika kuwa mkuu wa Idara ya Wafanyakazi ya Wizara ya Ulinzi, Yuriy Kuznetsov alikuwa kizuizini.

Mwezi Mei 17, kamanda wa zamani wa Kikosi cha 58 katika Wilaya ya Kijeshi ya Kusini, Ivan Popov, alikamatwa.

Wote wanatuhumiwa kwa ufisadi au ubadhirifu.

Pia unaweza kusoma

Vita dhidi ya Ufisadi

"Bila shaka, mapambano dhidi ya rushwa yanaendelea katika idara zote," alisema msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmytro Peskov baada ya kukamatwa kwa Shamarin.

Bbaada ya kuapishwa Vladimir Putin mwezi Mei, Serhiy Shoigu aliacha wadhifa wa waziri wa ulinzi na kuwa katibu wa Baraza la Usalama.

Mtaalamu wa uchumi Andrei Belousov bila kutarajiwa ndiye amekuwa Waziri mpya wa Ulinzi.

Kremlin ilielezea kwamba wizara hiyo inapaswa kuwa ya uvumbuzi na mipango bora. Hii ndio sababu, Putin alimchagua Belousov.

Wachambuzi wa mambo wanaamini uteuzi huo ni juhudi za kudhibiti ongezeko kubwa la gharama zinazohusiana na kufadhili vita na kupambana na ufisadi ndani ya Wizara ya Ulinzi.

Sakata la Mawasiliano ya Jeshi

Mwaka 2020, mtangulizi wa Vadym Shamarin, Jenerali Khalil Arslanov, alikamatwa kwa ubadhirifu.

Miaka sita kabla ya kukamatwa kwake, aliahidi jeshi litahamia haraka kwenye mfumo wa mawasiliano wa kidijitali.

Uchunguzi wa kesi ya Arslanov bado unaendelea, baadhi ya waliokuwa chini yake tayari wako gerezani, na ubora wa mawasiliano ya jeshi unakosolewa na baadhi.

Novemba 2022, mwanablogu Andriy Morozov, jina la utani Murz, alikosoa Wizara ya Ulinzi kwamba inanunua mifumo ya mawasiliano ya gharama kubwa ambayo haikidhi sifa zilizotangazwa na haifai kutumika katika ngazi ya kitaifa.

Kulingana na yeye, hii ndiyo sababu jeshi la Urusi liliamua kununua mfumo wa mawasiliano ya redio kutoka China mwezi Februari 2024. Morozov alijiua.

Mabadiliko katika Wizara ya Ulinzi

dfxc

Chanzo cha picha, GAVRIIL GRIGOROV/RUSSIAN PRESIDENCY

Maelezo ya picha, Andriy Belousov wakati wa mkutano na Vladimir Putin huko Kremlin Julai 2023

Waziri mpya alianza kujenga timu yake, akiwaondoa washirika wa zamani wa Sergei Shoigu. Lakini watu walitarajia mabadiliko ya namna hiyo katika Wizara ya Ulinzi ya Urusi.

Serhiy Shoigu amefanya kazi kwa zaidi ya miaka thelathini - kwanza kama mkuu wa Wizara ya Hali ya Dharura, kisha gavana wa Moscow na kwa miaka 12 iliyopita, kama waziri wa ulinzi.

Wakati huu Belousov akiongoza Wizara ya Ulinzi, watu wengi wanaamini ukaguzi mkubwa utafanywa katika wizara hiyo.

Vita vikiingia mwaka wa tatu, imeamuliwa kwamba sera za Wizara ya Ulinzi juu ya mawasiliano pia zitabadilika chini ya kiongozi mpya.

Askari walioko mstari wa mbele bado hawajapata ushindi kamili. Wakati huo huo, Andriy Belousov anapanga timu yake katika Wizara ya Ulinzi ya Urusi, akiwaondoa washirika wa zamani wa Sergei Shoigu.