Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 27.06.2024

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alexander Isak

Chelsea wameulizia kuhusu mshambulizi wa Newcastle Alexander Isak lakini watalazimika kulipa zaidi ya £115m kumsajili mshambuliaji huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 24. (Mail)

Newcastle wanasitasita kumuuza Isak na wangependa kumuuza Callum Wilson badala yake, huku timu za Uingereza, Ujerumani na Saudi Arabia zikimtaka mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 33. (TeamTalks).

Bayern Munich wanakaribia kumnunua kiungo wa kati wa Everton na Ubelgiji Amadou Onana, 22, baada ya kuchanganyikiwa katika juhudi zao za kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 28, kutoka Fulham. (Liverpool Echo).

Barcelona wanavutiwa na mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Julian Alvarez, 24. (Sport – In Spanish).

Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia, ambao unamiliki klabu nne za Saudi Pro League, unamsaka kiungo wa kati wa Arsenal na Ghana Thomas Partey, 31. (Caught Offside).

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Thomas Partey

Atalanta wametoa dau la pauni milioni 10 kwa ajili ya kumnunua beki wa Everton Ben Godfrey, huku klabu ambayo haijatajwa ikitoa pauni milioni 15 kumnunua beki huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26. (Athletic - Subscription).

Manchester United wanafikiria kuuza haki za majina kwa Old Trafford ili kusaidia kupata pesa. (Athletic – Subscription Required)

Everton wanakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Nigeria Wilfried Ndidi, 27, kwa uhamisho wa bila malipo mkataba wake wa Leicester utakapokamilika wiki ijayo. (Football Insider)

Mshambulizi wa Newcastle Yankuba Minteh amekataa kuhamia Lyon licha ya klabu hiyo ya Ufaransa kukubali ada ya £40m kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Gambia mwenye umri wa miaka 19. (Sun)

Brighton wanavutiwa na kiungo wa kati wa Inter Miami na Paraguay Diego Gomez, 21. (Talksport),

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jobe Bellingham

Crystal Palace wanashughulikia mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Sunderland Muingereza Jobe Bellingham, 18. (Fabrizio Romano),

Ipswich iko kwenye mazungumzo na Hull kuhusu mpango wa kumnunua beki wa Uingereza Jacob Greaves, 23. (Athletic – Subscription Rquired).

Manchester United inamlenga kipa wa Bayern Munich Mjerumani Maria Luisa Grohs, 23, kama mbadala wa Mary Earps, ambaye anatarajiwa kujiunga na Paris St-Germain. (Florian Plettenberg).

Klabu ya Saudia Al-Hilal inafikiria kumnunua winga wa Manchester United mwenye umri wa miaka 19, Alejandro Garnacho, ambaye kwa sasa yuko Copa America na Argentina. (Express).

Arsenal wanatazamiwa kumkosa mshambuliaji wa Stuttgart Serhou Guirassy huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea mwenye umri wa miaka 28 akitaka kuhamia Borussia Dortmund. (Metro).

Imetafsiriwa na Seif Abdalla