Nyoka aliyezaa watoto 14 bila kupewa mimba na mwenza

Ronaldo hajawa na nyoka wa kiume kwa miaka tisa

Nyoka ambaye amekuwa akidhaniwa kuwa dume kwa miaka mingi amezaa watoto 14 bila ya kujamiiana.

Ronaldo, mwenye umri wa miaka 13, anaishi katika Chuo cha City of Portsmouth.

Pete Quinlan, mtaalamu wa wanyama katika chuo hicho, alidhani ni nyoka wa kiume hadi Ronaldo alipozaa watoto.

Si hivyo tu, aliongeza kuwa katika miaka tisa iliyopita, Ronaldo hajawahi kujamiiana na nyoka wa kiume.

Kuzaliwa kwa watoto bila mwenzi wa kiume kunaitwa 'parthenogenesis'. Hii hutokea mara tatu tu kwa nyoka mmoja.

Unaweza kusoma
Quinlan hapo awali alifikiria Ronaldo kama nyoka wa kiume

"Nilimwokoa Ronaldo miaka tisa iliyopita," Quinlan alisema.

Alisema wakati anajiunga na idara ya uhifadhi wa wanyama chuoni hapo chini ya miaka miwili iliyopita, alileta pia nyoka aliowakusanya hapa.

Quinlan alisema alikuwa mahali pengine wakati watoto wa Ronaldo walizaliwa. "Mwanafunzi aliwatahadharisha wafanyakazi baada ya kuona watoto wa nyoka wakizurura kwenye tanki."

"Mara moja nilikimbia kwenda kuangalia nini kinatokea huko," alisema.

Ronaldo alizaa watoto 14

Inawezekana katika baadhi ya viumbe kuzaa watoto bila mpenzi wa kiume.

Aina nyingi za wanyama wasio na uti wa mgongo kama vile wadudu huzaa watoto bila kujamiiana.

Kwa kujipanga wenyewe, wanazalisha watoto wanaofanana na wao wenyewe.

Mnamo Februari, stingray huko Marekani alipata mimba bila mwenzi.

Hata hivyo, hii ni nadra kwa wanyama wenye uti wa mgongo kama vile nyoka.

Unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Liz Masinga