Mpox ni nini na hueneaje?

Milipuko nchini DR Congo imeathiri watoto pamoja na watu wazima

Chanzo cha picha, Reuters

Aina mpya ya virusi vya mpox inaenea kwa haraka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na wataalamu wanasema ni aina hatari zaidi waliyoishuhudia.

Mpox, ambayo zamani iliitwa monkey pox, imeenea katika sehemu za magharibi na kati mwa Afrika na kesi zimekuwa zikiongezeka katika bara hilo kwa miongo kadhaa.

Mnamo 2022, janga la ulimwengu la mpox liliathiri Ulaya, Australia, Marekani na nchi nyingine nyingi.

Unaweza kusoma

Ugonjwa wa Mpox husababishwa na virusi vya monkeypox, familia moja ya virusi na ndui, ingawa si kali sana.

Virusi hivi awali vilisambazwa kutoka kwa wanyama hadi kwa wanadamu, na hupatikana zaidi katika nchi zilizo karibu na misitu ya mvua ya kitropiki.

Katika maeneo hayo , kuna maelfu ya wagonjwa na mamia ya vifo kutokana na ugonjwa huo kila mwaka, na watoto chini ya umri wa miaka 15 wameathirika zaidi.

Kuna aina mbili kuu za virusi zinazojulikana kuwepo. Hali mbaya zaidi ilisababisha mlipuko wa kimataifa mnamo 2022 ambao ulienea kwa karibu nchi 100 ambazo hazikuwahi kukumbwa na virusi hivyo.

Shida ya pili, hatari zaidi ni ya kawaida katika Afrika ya kati ni sababu ya aina mpya iliyogunduliwa hivi karibuni nchini DR Congo.

Aina hizi mbili hubeba hatari tofauti za ugonjwa na vifo.

Dalili za ugonjwa wa Mpox

Mpox,  huenezwa kwa kuwasiliana kwa karibu na watu walioambukizwa

Chanzo cha picha, Getty Images

Dalili za awali ni pamoja na homa, maumivu ya kichwa, uvimbe, maumivu ya mgongo na misuli kuuma.

Mara baada ya homa , upele unaweza kutokea, mara nyingi huanza kwenye uso kisha kuenea kwenye sehemu nyingine za mwili, mara nyingi viganja vya mikono na nyayo za miguu.

Upele, ambao unaweza kuwasha au kuumiza sana, hubadilika na kupitia hatua tofauti kabla hatimaye kutengeneza kipele, ambacho hutumbuka baadaye. Vidonda vinaweza kusababisha makovu.

Maambukizi kawaida huisha yenyewe na hudumu kati ya siku 14 na 21.

Kesi mbaya zinaweza kutokea kwa kushuhudia vidonda vikishambulia mwili mzima, na haswa mdomo, macho na sehemu za siri.

Je, hueneaje?

Mpox huenea kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine kwa kuwa karibu na mtu aliyeambukizwa, ikiwa ni pamoja na kupitia ngono, kugusana ngozi na kuzungumza au kupumua karibu na mtu mwingine.

Virusi vinaweza kuingia mwilini kupitia ngozi iliyo na michubuko, njia ya upumuaji au kupitia macho, pua au mdomo.

Inaweza pia kuenea kwa kugusa vitu ambavyo vilishikwa au kutumiwa na mwenye virusi, kama vile matandiko, nguo na taulo.

Kugusana kwa karibu na wanyama walioambukizwa, kama vile nyani, panya na Kuchakuro (squirrels), ni njia nyingine.

Wakati wa mlipuko wa kimataifa mnamo 2022, virusi vilienea zaidi kupitia mawasiliano ya ngono.

Mlipuko wa sasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unasukumwa na mawasiliano ya ngono, lakini pia umepatikana katika jamii nyingine.

Ni nani aliye hatarini zaidi?

Kuna chanjo ambazo hukinga dhidi ya sumu kali

Chanzo cha picha, Getty Images

Kesi nyingi mara nyingi hupatikana kwa watu wanaofanya ngono na wanaume wanaofanya ngono na wanaume. Watu walio na wapenzi kadhaa au wapenzi wapya wanaweza kuwa katika hatari zaidi.

Lakini mtu yeyote ambaye ana mawasiliano ya karibu na mtu aliye na dalili anaweza kupata virusi, pamoja na wafanyakazi wa afya na wanafamilia.

Ushauri ni kuepuka kugusana kwa karibu na mtu yeyote mwenye mpox na osha mikono yako kwa sabuni na maji ikiwa virusi viko katika jamii yako.

Wale ambao wana mpox wanapaswa kujitenga na wengine hadi vidonda vyao vyote vipotee.

Mpira wa kiume unapaswa kutumika kama tahadhari wakati wa kufanya ngono kwa wiki 12 baada ya kupona, Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema.

Je, inaweza kutibiwaje?

Tiba iliyoundwa kutibu ndui inaweza pia kuwa muhimu katika kutibu mpox, lakini kuna utafiti mdogo kuhusu jinsi inavyofaa.

Milipuko ya mpox inaweza kudhibitiwa kwa kuzuia maambukizi, njia bora ya kufanya hivyo ni kwa chanjo.

Kuna chanjo tatu ambazo zipo lakini ni watu walio hatarini tu au ambao wamewasiliana kwa karibu na mtu aliyeambukizwa kwa kawaida wanaweza kuipata.

WHO kwa sasa haipendekezi kuchanja watu wote.

Majaribio zaidi ya chanjo dhidi ya aina mpya za mpox yanahitajika ili kuelewa ni kiasi gani cha ulinzi kinachotoa.

Unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Lizzy Masinga