Mbappe v Ronaldo? Mwongozo wa hatua ya mtoano Euro 2024

Picha ya mtu aliyevaa kama simba miongoni mwa mashabiki wa Uholanzi

Chanzo cha picha, Getty Images

  • Author, Emma Sanders
  • Nafasi, BBC Michezo Ujerumani

Baada y a mechi 36 kuchezwa na timu nane kuondolewa, sasa tunaingia kwenye hatua ya mtoano kwenye michuano ya Euro ya ya mwaka huu nchini Ujerumani.

Timu 24 zimesalia wakati zinatazamia kuwa moja ya pande mbili ambazo zitashiriki fainali ya Euro 2024 huko Berlin mnamo Julai 14.

BBC Sport inaangazia mambo machache ya kuangalia katika hatua ya mtoano.

Soma pia:

Je, huu ni mwaka wa Ujerumani?

Mashabiki wa Ujerumani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Matumaini yanaongezeka miongoni mwa mashabiki wa Ujerumani kwamba timu yao inaweza kwenda mbali zaidi

Fursa ya kuchezea nyumbani.

Hakuna kitu kama kushinda kombe la mashindano makubwa katika ardhi ya nyumbani na imani inaongezeja nchini Ujerumani kwamba wanaweza kufanya hivyo.

Mashabiki walipojaa kutazama mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Scotland kulikuwa na matumaini - lakini bado kulikuwa na hisia kwamba Ujerumani walikuwa wanaunda timu.

Yote yalibadilika baada ya ushindi wao wa 5-1 na sasa mashabiki wa Ujerumani wanaamini mambo yanaweza kuwa mazuri.

Gumzo la mashabiki kwenye baa, stesheni za treni na mikahawa kote nchini linaashiria sio watu wengi wanaotilia shaka uwezo wa timu ya taifa ya Ujerumani.

Kuwa na kikosi kilichojaa vipaji, umati wa mashabiki uwanjani, na kocha Julian Nagelsman ambaye mchanga na mwenye mbunifu ni fursa ya kweli kwa Ujerumani kutinga fainali mjini Berlin.

Bao la Ronaldo, Mbappe atampiku?

Kylian Mbappe na Cristiano Ronaldo

Chanzo cha picha, Gety Images

Maelezo ya picha, Ufaransa na Ureno zimekutana katika miaka ya hivi karibuni katika Ligi ya Mataifa na Euro 2020 na zinaweza kumenyana tena nchini Ujerumani

Cristiano Ronaldo alikuwa mfungaji bora katika michuano ya Euro 2020 na na macho yote yanaelekezwa kwake kama kinara wa timu hii ya Ureno nchini Ujerumani.

Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 hakufanikiwa kufunga bao lolote katika hatua ya makundi - mara ya kwanza katika michuano ya Euro au Kombe la Dunia.

Sio kwa kutaka kujaribu, hata hivyo. Amekuwa na mashuti 12 hadi sasa kwenye Euro 2024 - zaidi ya mchezaji mwingine yeyote.

Iwapo timu zote mbili zitafuzu katika mechi zao za 16-bora, Ureno na Ufaransa zitakutana katika robo fainali na unaweza kufikiria Ronaldo angetoka nje kwenda juu Kylian Mbappe.

Kushindwa kuendana na matarajio

Kikosi cha tajika cha Ubelgiji ''enzi hizo'' huenda hakipo tena. Kwa kuwa nchi hiyo imeorodheshwa ya tatu duniani, bado kuna matumaini makubwa kwao kutumbuiza kwenye michuano hii.

Kufikia sasa wameshindwa kufikia malengo.

Sare tasa dhidi ya Ukraine ilitosha kuwafanya mashabiki kufa moyo huku wakidhihaki na kueleza hasira zao licha ya Ubelgiji kutinga hatua ya mtoano.

Kevin de Bruyne alitoa wito katika mkutano na wanahabari Jumatano, akidai Ubelgiji "inahitaji mashabiki".

Je, watawaunga mkono? Au Ubelgiji ina kibarua kigumu kuwashawishi tena?

‘Huwezi kushinda lolote ukiwa na wachezaji chipukizi’

Ferran Torres na Lamine Yamal wa Uhispania inasherehekea baada ya ushindi wa Uhispania dhidi ya Italia kwenye Euro 2024

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lamine Yamal, kulia, ni miongoni mwa wachezaji chipukizi katika michuano ya Euro 2024

Lakini Uhispania huenda ikafua dafu.

Nyota wa michuano hiyo hadi sasa, Uhispania wamerejea kwenye kilele cha soka la Ulaya na wakiwa na wachezaji chipukizi kwenye kikosi chao.

Nico Williams, Lamine Yamal na wenzie wameangazia mashindano hayo kwa kutoogopa na ubunifu wao wa hali ya juu.

Kutoka kwa nutmegs hadi backheel flicks na pasi bila kuangalia, vijana wenye vipaji wa Hispania wameonyesha kuwa wana viungo wanaohitaji kuchukuwa ushindi.

Akiwa na umri wa miaka 16, Yamal wa Barcelona tayari ameshawatia hofu mabeki na hakuna pendekezo lolote analokusudia kupunguza kasi yake hivi karibuni.

Mashabiki wa Uhispania wanavalia fulana zilizo na Williams kwenye mgongoni huku Pedri akidhibiti safu ya kati.

Wachezaji chipukizi wako sawa.

Mashabiki wa Uholanzi wakifanya mbwewe zao

Mashabiki wa Uholanzi

Chanzo cha picha, GEtty Images

Maelezo ya picha, Mashabiki wa Uholanzi wamekuwa wakitembea kwenda uwanjani nchini Ujerumani wakiwa wamevalia kulana zao za kuvutia

Ni mashabiki wanaofanya mchuano kuvutia na kila nchi imefanya juhudi kuwahamsisha mashabiki kuhudhuria kwa wingi katika mashindano ya Euro 2024.

Hata hivyo uwepo wa mashabiki wa Uholanzi unavutia sana nchini Ujerumani kufikia sasa.

Katika miji ya Hamburg, Leipzig na Berlin waligeuza mitaa kuwa rangi ya chungwa, wakitembea, wakicheza na kuimba wakielekea

Wakazi wa Munich wanatarajiwa kushuhudia mbwembwe za mashabiki wakati Uholanzi itachuana na Romania katika mechi yao ya hatua ya 16 bora tarehe 2 Julai.

Austria

Austria inadhihirisha kuwa timu inayotazamwa kwenye Euro 2024, ikiwa imeongoza kundi gumu lililojumuisha Uholanzi na Ufaransa, na sifa nyingi zinakwenda kwa kocha wao - mkufunzi wa zamani wa Manchester United Ralf Rangnick.

Anajulikana kama "Godfather of Gegenpressing", Rangnick ameunda timu inayojituma kwa nguvu, kucheza kwa hamu ya kushinda.

Mnamo Machi, Christoph Baumgartner alifunga bao la haraka zaidi katika kandanda ya kimataifa kwa mkwaju ndani ya sekunde saba dhidi ya Slovakia, na huko Ujerumani wameelekea kufanya hivyo.

Wamefunga katika dakika 10 za mwanzo katika mechi mbili kati ya tatu walizocheza kufikia sasa, hivyo Uturuki itahitaji kuwa macho kuanzia mwanzo katika mechi yao ya hatua ya 16 bora.

Je, Rangnick, ambaye alidhihakiwa na United, anaweza kusumbua soka la Uingereza katika nusu fainali?

Maelezo zaidi:

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi