Kwa nini tunapenda wanyama wenye sura mbaya?

j

Chanzo cha picha, getty images

Maelezo ya picha, Kila mwaka majaji huko California huchagua mshindi wa shindano la Mbwa Mbaya Zaidi Duniani
  • Author, Isabelle Gerretsen
  • Nafasi, BBC

Kila mwezi Juni huko Petaluma, California, Marekani majaji hutupia jicho safu ya mbwa ili kuamua mshindi wa shindano la Mbwa Mbaya Zaidi Duniani. Shindano hili huvutia mioyo ya wapenzi wa wanyama ulimwenguni.

Swali, kwa nini tunavutiwa na wanyama wabaya?

Kwa mujibu wa mtaalamu wa wanyama kutoka Austria, Konrad Lorenz, binadamu huvutiwa na wanyama wenye maumbo ya ajabu kama, macho makubwa, vichwa vikubwa na miili laini, ili kutoa ulinzi na kuhakikisha maisha ya wanyama hao.

“Maumbo ya ajabu huongeza tabia ya ulinzi, umakini na utayari wa kumtunza na kuondoa uwezekano wa mnyama huyo kutendewa vibaya," anasema Marta Borgi, mtafiti wa wanyama katika taasisi ya Superiore di Sanità huko Roma, Italia.

Pia unaweza kusoma

Tafiti kuhusu wanyama

k

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Wanyama wabaya mara nyingi huwa na sifa kama za watoto wadogo wa kibinadamu ambazo huchochea tabia zetu za kuwalinda

“Ni kama katika maisha ya binadamu, watoto wadogo huwategemea walezi wao kwa riziki na ulinzi, hali hiyo huwafanya watoto kuishi na kukuwa," anasema Borgi.

Utafiti wa 2014 wa Borgi na watafiti wengine uligundua kuwa dhana ya binaadamu ya "uzuri" kuhusu wanyama huanza katika umri mdogo, watoto wenye umri wa miaka mitatu wanaonyesha kupenda wanyama na binaadamu wenye macho makubwa, pua za mviringo na nyuso za mviringo.

Watafiti walifuatilia macho ya watoto wenye umri wa miaka mitatu hadi sita na kugundua kuwa walikuwa wakitazama zaidi picha za mbwa, paka na binadamu ambao maumbo yao yamebadilishwa kwa kompyuta ili kuongeza maumbile yao.

Pia waliwataka watoto kutathmini picha hizo kwa mizani ya moja hadi tano, moja ikiwa "si nzuri" na tano ikiwa "inapendeza sana."

Watoto hao waliorodhesha nyuso za duara zenye paji kubwa la uso, macho makubwa na pua ndogo kuwa nzuri zaidi kuliko zile zenye maumbile ya kawaida.

"Namna kiungo fulani kilivyo cha kipekee usoni kwa mbwa au paka, ni kigezo muhimu kinachoathiri mtazamo wa watoto kuhusu kupendeza," anasema Borgi.

Ingawa viumbe wengi wabaya wamezoea maisha yao ya porini na hutoa faida kwa mifumo ya ikolojia wanayoishi, mara nyingi hawapewi kipau mbele kama paka na mbwa.

“Kuna mambo mengi yanayochochea maamuzi ya watu kupenda wanyama wabaya," anasema Rowena Packer, mhadhiri wa tabia za wanyama katika Chuo Kikuu cha London, nchini Uingereza.

“Hilo kwa kiasi fulani linachochewa na mitandao ya kijamii, kwani watu mashuhuri na wenye ushawishi huonyesha mbwa aina ya pug-pet na bulldogs kutoka Ufaransa kwenye Instagram zao,” anasema.

Tahadhari ya madaktari

K

Chanzo cha picha, ALAMY

Maelezo ya picha, Bulldogs wa Kifaransa ndio aina maarufu zaidi nchini Marekani lakini hukumbwa na matatizo mbalimbali ya kiafya

Lakini madaktari wa mifugo wanawahimiza watu wasichague aina ya mbwa wa brachycephalic, au wale wenye nyuso bapa (flat-faced), kwa sababu wanakabiliwa na matatizo makubwa ya afya.

Mbwa aina ya Pugs na bulldogs wa Ufaransa hupata matatizo ya kupumua, maambukizi ya mara kwa mara ya ngozi na magonjwa ya macho.

Utafiti wa 2022 ulihitimisha kuwa mbwa aina ya pugs, hawezi tena kuchukuliwa kama mbwa wa kawaida kutokana na matatizo ya kiafya, wanakabiliwa na matatizo makubwa ya afya.

Katika majira ya joto, pugs wako katika hatari ya kupooza kwa joto wakati wanapo pambana kudhibiti joto la miili yao.

"Ikiwa unafikiria juu ya mbwa mwitu, wana pua ndefu," anasema Packer. "Hudhibiti joto kupitia pua ambayo inawaruhusu kudhibiti joto vyema na hawatoi jasho kama sisi."

Lakini mbwa aina ya pug wana pua ndogo na njia nyembamba za hewa ambayo hufanya iwe vigumu kwao kupumua na kupoza miili yao wakati wa joto.

Matokeo yake pugs wengi hukoroma, kwa sababu ya udogo wa njia zao za hewa. Na licha ya matatizo mengi ya afya, pugs bado ni maarufu sana.

"Kuna sababu nyingi za kisaikolojia kwa nini watu hupenda mbwa hao licha ya matatizo yao ya kiafya," anasema Packer. “Watu wanawapenda pugs kwani wanapenda kucheza na kutulizana."

"Kuna utamaduni wa watu kupenda mbwa wenye miili midogo. Lakini kwa hakika hiyo inaweza kuwa dalili ya ulemavu wa mgongo na inaweza kusababisha magonjwa mengi ya neva kwa mbwa huyo."

Ingawa maumbile kama vile macho yaliyotuna na nyuso zilizokunjana vinaweza kutufanya tutabasamu, lakini tunapaswa kutafakari upya kuhusu wanya wenye sura mbaya.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Lizzy Masinga