Tetesi za soka Ulaya Jumanne 25.06.2024

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Joshua Zirkzee amekuwa akihusishwa na klabu kadhaa kubwa barani Ulaya baada ya kuwa na msimu mzuri katika klabu ya Serie A Bologna.

Manchester United wanatazamia kukidhi kipengele cha kuachiliwa kwa Joshua Zirkzee huku wakipanga kumuuza Mason Greenwood ili kufadhili mpango huo, nao Everton wakitakiwa kuwasilisha ombi jingine kwa Jarrad Branthwaite.

Manchester United wanatarajiwa kufikia kipengele cha uhamisho cha euro 40m (£33.9m) kwa mshambuliaji wa Bologna Joshua Zirkzee, 23, na pia wamefanya mazungumzo na Lille kuhusu mkataba wa kumnunua beki wa Ufaransa wa U21 mwenye umri wa miaka 18 Leny Yoro. (Sky Sports)

United wanatumai kufadhili usajili wa Zirkzee kwa kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Mason Greenwood, 22. (I Sport)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jarrad Branthwaite

Everton wanatarajia Manchester United itawasilisha ofa nyingine kwa beki wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 21. (Liverpool Echo)

Everton wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Senegal Iliman Ndiaye, 24, kutoka Marseille. (Footmercato – In French)

Manchester United wanatarajia kukubaliana kandarasi mpya na meneja Erik ten Hag kabla ya kuanza kwa ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani mwezi ujao. (ESPN)

Mshambulizi wa zamani wa Manchester United Ruud van Nistelrooy, 47, amefanya mazungumzo chanya kuhusu kurejea katika klabu hiyo kama sehemu ya wakufunzi wa Ten Hag. (Talksport)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Uhispania Joselu, 34, anakaribia kuondoka Real Madrid baada ya kupokea ofa kutoka kwa klabu ya Qatar Al Gharafa. (Athletic – Subscription Required)

Chelsea wameanza mazungumzo na Barcelona kuhusu mkataba wa kumnunua mshambuliaji wa Uhispania Marc Guiu, 18. (ESPN)

The Blues wanaongoza Bayern Munich katika mbio za kumsajili Guiu. (Fabrizio Romano)

Borussia Dortmund wanavutiwa na kiungo wa kati wa Leeds United wa U21 Archie Gray, 18. (Bild – In Germany)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mohammed Kudus

Tottenham wameanza mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Lille wa Canada Jonathan David, 24, ambaye pia anahusishwa na kuhamia Chelsea. (Football Insider)

Mchezaji wa Ghana Mohammed Kudus, 23, amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka West Ham lakini klabu hiyo bado haijapokea ofa ya kiungo huyo mshambuliaji. (Sky Germany)

Napoli itazingatia ofa ya kiwango cha euro 100m (£85m) kwa mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 25, na mshambuliaji wa Chelsea wa Ubelgiji Romelu Lukaku anayetarajiwa kuchukua mahala pake. (Calciomercato – In Italy),

Aston Villa wameungana na Chelsea katika kinyang'anyiro cha kumnunua fowadi wa Hoffenheim Mjerumani Maximilian Beier, 21. (Sky Sport Germany)

Ligi kuu ya England imezionya klabu kuwa kuuza wachezaji kwa kufuata sheria za kifedha kunaweza kukiuka kanuni za kutenda kwa nia njema. (Times - Subscription Required)