Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 01.07.2024

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Liverpool, Arsenal na Chelsea zinamtaka mlinzi wa Bologna Riccardo Calafiori, Brighton waponyokwa na mchezaji wanayemlenga huku Manchester United ikionyesha nia ya kutaka kumnunua beki wa Barcelona.

Liverpool, Arsenal, Chelsea na West Ham wote wanavutiwa na beki wa Italia Riccardo Calafiori, 22, lakini watalazimika kulipa zaidi ya £40m ili kumnunua kutoka Bologna. (Express),

Baadhi ya wakurugenzi wa Barcelona bado hawajashawishika kuhusu ubora wa kumsajili winga nyota wa Uhispania Euro 2024 Nico Williams, 21, kutoka Athletic Bilbao . (Sport - kwa Kihispania)

Brighton wamechanganyikiwa baada ya Chelsea kukubali dili la kumsajili kiungo Kiernan Dewsbury-Hall, 25, kutoka Leicester ingawa mchezaji huyo alikuwa amefanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na Seagulls na ada ilikubaliwa kati ya klabu hizo mbili. (Telegraph - usajili unahitajika)

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United hawanania ya kutafuta dili la kumnunua mlinzi wa Barcelona Ronald Araujo licha ya nia ya muda mrefu ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 25. (Football Transfers)

Leicester wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua kiungo wa kati Michael Golding mwenye umri wa miaka 18 kutoka Chelsea . (The Athletic-Usajili unahitajika)

Newcastle wanajaribu kufanya mazungumzo ya kumsaini mlinda lango wa Nottingham Forest wa Ugiriki Odysseas Vlachodimos, 30, kama sehemu ya uhamisho wa kiungo wa kati wa Scotland Elliot Anderson, 21, kwenda City Ground. (Daily Mail)

Mkufunzi wa Newcastle Eddie Howe ameweka wazi katika mazungumzo na bodi ya klabu hiyo kwamba hawatakiwi kumuuza mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 24, msimu huu huku kukiwa na nia kutoka kwa Chelsea . (Fabrizio Romano kupitia Teamtalk)

Tottenham wanatazamiwa kuanzisha chaguo la kuongeza mkataba wa mshambuliaji wa Korea Kusini Son Heung-min mwenye umri wa miaka 31 na klabu hiyo hadi 2026. (Football Insider)

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah