Tetesi za soka Ulaya Jumatano 26.06.2024

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Eberiche Eze

Tottenham wako tayari kumsajili kiungo matata wa Crystal Palace Eberechi Eze, Brighton wanamlenga Kiernan Dewsbury-Hall, huku Arsenal wakiulizia kuhusu Johan Bakayoko.

Tottenham wanavutiwa na mshambuliaji wa Crystal Palace na England Eberechi Eze, 25, na wanaweza kutafuta kuamsha kipengele cha kumuachia katika mkataba wake. (Talksport)

Brighton wanamtaka kiungo wa kati wa Leicester Muingereza Kiernan Dewsbury-Hall, 25. (Telegraph – Subscription Required}

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jadon Sancho

Arsenal wameuliza kuhusu kumsajili mshambuliaji wa PSV Eindhoven wa Ubelgiji Johan Bakayoko. (DHNet – In French).

Tottenham imeshinda Klabu kadhaa za Ligi ya Premia katika kumsajili mshambuliaji wa Glentoran mwenye umri wa miaka 16 George Feeney, ambaye amewakilisha Ireland Kaskazini na Wales katika ngazi ya vijana. (Football.London).

Barcelona huenda wakavutiwa na mkataba wa mkopo wa winga Mwingereza Jadon Sancho, 24, baada ya kufanya mazungumzo na Manchester United. (Sport – In Spanish)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Joao Palhinha

Bayern Munich bado wanavutiwa na kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 28, lakini wanapungukiwa sana na dau la pauni milioni 60 la Fulham. (Telegraph – Suvscription Required), nje

Aston Villa wanafikiria kumnunua winga wa Sporting Lisbon Pedro Goncalves mwenye umri wa miaka 25. (A Bola – In Portugal).

Ipswich wako kwenye mazungumzo na beki wa Uingereza Ben Johnson mwenye umri wa miaka 24 kuhusu uhamisho wa bila malipo mkataba wake wa West Ham utakapokamilika wiki ijayo. (East Anglian Daily Times).

.

Chanzo cha picha, Getty images

Maelezo ya picha, Adrien Rabiot

Manchester United wamefanya mazungumzo na Juventus kuhusu kumsajili Adrien Rabiot, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Arsenal na Aston Villa kumnunua kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29. (TeamTalks).

Nottingham Forest na Brighton wanavutiwa na winga wa Norway wa klabu ya Sogndal mwenye umri wa miaka 18 Edmund Baidoo. (Sky Sports),

Kocha wa Manchester United Erik ten Hag anatarajiwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Fabrizio Romano)

Kiungo wa kati wa Leeds Mhispania Marc Roca, 27, yuko kwenye mazungumzo ya kiwango cha juu na Real Betis kuhusu mkataba wa kudumu baada ya kusajiliwa na klabu hiyo kwa mkopo msimu uliopita. (Football Insider).

West Ham wako tayari kumruhusu mshambuliaji wa Uingereza Danny Ings, 31, kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto na Southampton wameonyesha nia yao. (Football Insider).

Winga wa Hull Muingereza Jaden Philogene, 22, amepeanwa kwa Barcelona kwa mkopo na chaguo la kumnunua. (Sport – In Spanish}