Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 30.06.2024

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United imeanza mazungumzo na beki wa kati wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 24, ambaye yuko tayari kuondoka Bayern Munich msimu huu wa joto. (Sky Sport Germany)

Paris St-Germain wako tayari kulipa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya dunia kumsajili winga wa Uhispania Lamine Yamal, 16, kutoka Barcelona. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Manchester City wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ujerumani Joshua Kimmich, 29, na winga wa RB Leipzig kutoka Uhispania Dani Olmo, 26. (Sun)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea wamejadili kumjumuisha mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 23, kama sehemu ya mkataba wa mshambuliaji wa Newcastle United na Uswidi Alexander Isak, 24. (Sun).

Chelsea pia wako tayari kuwapa kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 24, mshambuliaji wa Albania Armando Broja, 22, na beki wa kati wa Uingereza Trevoh Chalobah, 24, kama wachezaji wanaoweza kutafutwa katika dili la Isak. (Football Insider)

Arsenal bado wanavutiwa na Isak na wanaweza kufikia bei ya Newcastle, lakini Gunners wanauwezekano wa kutanguliza usajili wa kiungo wa kati. (Football Transfers)

Pia unaweza kusoma:
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Newcastle wako kwenye mazungumzo ya kiwango cha juu na Nottingham Forest kuhusu uhamisho wa winga wa Uswidi Anthony Elanga, 22, huku kiungo wa kati wa Scotland Elliot Anderson, 21, akielekea upande mwingine. (Talksport)

Beki wa kati wa Senegal Moussa Niakhate, 28, anatazamiwa kukamilisha uhamisho kutoka Forest kwenda Lyon. (Fabrizio Romano)

West Ham wamewasiliana na Metz kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Georgia Georges Mikautadze, 23, na pia wanamfuatilia mlinzi wa Lyon wa Jamhuri ya Ireland Jake O'Brien, 23. (Guardian)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Crystal Palace wanavutiwa na Emile Smith Rowe, ambaye anaweza kuondoka Arsenal kwa pauni milioni 25, lakini kiungo huyo wa kati wa Uingereza, 23, anatamani kusalia na The Gunners. (Sun)

Crystal Palace wako katika hali ya kupungukiwa na kiasi kikubwa cha pesa kutokana na uhamisho unaofuata wa O'Brien kwani walijumuisha kipengele cha kumuuza cha hadi 25% walipomuuza kwa Lyon msimu uliopita wa joto. (Mail)

Beki wa zamani wa Ufaransa Raphael Varane, 31, amewasili Italia kujadili uwezekano wa kuhamia Como baada ya kuondoka Manchester United (Sky Sport Italia - in Italian)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Vasco da Gama wamewashinda wapinzani wao wa Brazil kufikia makubaliano na Philippe Coutinho kuhusu uhamisho wa majira ya kiangazi baada ya winga huyo wa Brazil, 32, kukubali Aston Villa kusitisha mkataba wake. (Globo - in Portuguese)

Leicester City wamekataa ombi la mwanzo la Chelsea la kumnunua kiungo wa kati Muingereza Kiernan Dewsbury-Hall, 25. (90min)

Wolves wamekubali dili la kumsajili mshambuliaji wa Norway Jorgen Strand Larsen, 24, kutoka Celta Vigo. (AS - in Spanish)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambulizi wa Chelsea Muingereza Carney Chukwuemeka, 20, analengwa na AC Milan. (Gianluca di Marzio)

Borussia Dortmund wametoa ofa "kubwa" kwa winga wa Tottenham Muingereza Mikey Moore, 16. (Football Insider)

Dortmund pia wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Italia Samuele Inacio, 16, kutoka Atalanta baada ya kuwashinda wapinzani wake Bayern Munich. (Sky Sport Germany - in German)

Soma zaidi:

Imetafsiriwa na Asha Juma